zitto junior
JF-Expert Member
- Oct 7, 2013
- 20,537
- 31,729
Katika miaka ya 1400 walifanikiwa kuikamata constantinople iliyokuwa makao makuu ya byanztium empire ambayo ilikuwa ndio tawi la Dola ya kirumi mashariki ya ulaya na ilikuwa chini ya wakristo ila Mehmed II alifanikiwa kukamata mji huu na kufuta ukristo na kuifanya dini ya kiislam kushamiri mpaka leo yaani uturuki ya sasa na nchi za jirani.
Sasa baada ya kumalizana na tawi hili la mashariki Mehmed II hapo kati aliteka miji mingi tu ya ulaya ila mwishoni kabisa alielekea kuvamia makao makuu ya dola ya kirumi yani Rome ili kuitawala na penginepo kufuta ukristo ulaya nzima maana kama makao makuu ya wakatoliki wakisilimu je nchi gani ya ulaya ingebaki na ukristo??
Alianzia mji wa Otranto hapo italia kwa kuwavamia na kutaka wasilimu walivyogoma alichinja mji mzima na alikuwa amepanga sasa kuelekea Roma na alikua ameagiza majeshi zaidi yatiririke ili kufanikisha adhma yake.... ila usiku mmoja kabla ya kuanza vita ya kuelekea Roma alifariki ghafla na hivyo mpango huo ukafia naye na tokea hapo hakuwahi patikana mtawala wa ottoman mwenye dhamira na uwezo wa kuvamia Roma tena.
Sasa wajuvi wa mambo naomba mtujuze je nini hasa kilimuua Mehmed II aka Mehmet the conqueror shujaa huyu wa kiislam je aliwekewa sumu?? Alisalitiwa?? Aliuawa na wakatoliki ?? Na kivipi jemedari huyu masaa machache kabla ya tukio la kihistoria afariki ghafla maana wajuzi wa mambo wanasema kma sio kifo chake leo hii ulaya nzima ingekuwa imesilimu
Naomba kuwasilisha
Cc Palantir Malcom Lumumba Eiyer MSEZA MKULU na wanajukwaa wote
NB: Mods naomba uzi huu msiufute maana huwa mnazimoderate then mnazifuta hii inavunja moyo sana watu kuanzisha thread za kufikirisha jukwaa hili maana wanatumia muda kutafiti alafu tafiti zao zinaishia kutupwa kapuni.....