Nini kilisababisha Kufa kwa “Kupatana”

Nini kilisababisha Kufa kwa “Kupatana”

Tena wakainunua hadi Zoom Tanzania ikawa chini yao. Shida matapeli ndo wameiharibu. Na wanunuzi nao ni mazombie sana hivi unawezaje kununua kitu kwa mtu aliye mbali na mkoa uliopo afu unamtumia hela kabisa ilhali mzigo haujauona bado.
Jamaa utazani wanashirikiana na matapeli wateja wengi wanalalamika wao hawajali
 
Nini kimesababisha kufa kwa hii App, yaan ilikuja kasi sana.

Ukiuliza wenye nayo leo unaweza usiwapate kirahisi.
Kilichosababisha ni biashara kuhamia kwenye platform nyingine kama facebook na instagram.
Ukumbuke social network ni rahisi zaidi kufikia wateja wengi tofauti na Kupatana. Pia kukosa ubunifu na Marketing strategies ilichangia pia.

Lazima umfanye mtumiaji wa application yako aitumie kila siku. Walishindwa kufanya hivyo. Yani ukishanunua kama ni Gari app unaisahau kabisa. Hii inasababisha app inakuwa na watembeleaji wachache tofauti na matangazo ambayo yanakuwa pushed na social network
 
Kilichosababisha ni biashara kuhamia kwenye platform nyingine kama facebook na instagram.
Ukumbuke social network ni rahisi zaidi kufikia wateja wengi tofauti na Kupatana. Pia kukosa ubunifu na Marketing strategies ilichangia pia.

Lazima umfanye mtumiaji wa application yako aitumie kila siku. Walishindwa kufanya hivyo. Yani ukishanunua kama ni Gari app unaisahau kabisa. Hii inasababisha app inakuwa na watembeleaji wachache tofauti na matangazo ambayo yanakuwa pushed na social network
Hapana huwezi kufananisha web au App na mtu anaetumia Facebook kufanya boosting Facebook tangazo linamfikia mtu yoyote ambaye Hana hela au Hana mpango ila web au App mtu anaingia kutafuta akiwa na hela mkononi watu wanatumia sana google kutafuta bidhaa
 
Online platforms za kuuza na kununua zimeongezeka zaidi wakati Kupatana hawakutaka enda na wakati mfano hata user interface imekua ya hovyo kuliko mwanzo,

Sidhani kama utapeli ni sababu kwa sababu hata insta matapeli wamejaa na bado watu tunaitumia
 
Tanzania bado sana kwenye biashara utume hela alafu hutumiwe mzigo,sahauuu
Lazima utapigwa tuuu
Watu wezi,dhuluma tu hawana ukweli..

Ova
Ni kweli uaminifu mdogo sijui kama inawezekana kama wenzetu wanachokifanya pesa ya mteja inashikiliwa mpaka mteja apate bidhaa yake kwanza pesa ndio inatoka
 
Online platforms za kuuza na kununua zimeongezeka zaidi wakati Kupatana hawakutaka enda na wakati mfano hata user interface imekua ya hovyo kuliko mwanzo,

Sidhani kama utapeli ni sababu kwa sababu hata insta matapeli wamejaa na bado watu tunaitumia
Wewe ndio Umeongea point sasa! Tatizo kubwa kabisa ni user interface ha kupatana, angalia jjji ilivyo imepangiliwa vizuri na inaeleweka
 
Kilichosababisha ni biashara kuhamia kwenye platform nyingine kama facebook na instagram.
Ukumbuke social network ni rahisi zaidi kufikia wateja wengi tofauti na Kupatana. Pia kukosa ubunifu na Marketing strategies ilichangia pia.

Lazima umfanye mtumiaji wa application yako aitumie kila siku. Walishindwa kufanya hivyo. Yani ukishanunua kama ni Gari app unaisahau kabisa. Hii inasababisha app inakuwa na watembeleaji wachache tofauti na matangazo ambayo yanakuwa pushed na social network
Naunga mkono hoja
 
Issue ya utapeli wa malipo ya online umepatikana mwaroboaini.

Let me introduce to you Payguard secure, ni a payment platform salama zaidi yenye escrow ndani yake.

Mteja na mnunuzi mnapokutana online, kubalianeni kukamilisha transaction yenu kupitia payguard secure. Mmoja wenu. Either mteja au mnunuzi anaweza akainitiate malipo haya.

Endapo mteja ataanzisha manunuzi kwenye app. Atabofya kitufe cha "i am buying" ataingiza namba ya simu ya muuzaji wake. Mfumo utafanya KYC ya muuzaji kupitia namba yake. Kisha utaweka taarifa za manunuzi ikiwemo Jina la bidhaa, description ya bidhaa, condition ya bidhaa, bei ya manunuzi ikiwapo usafiri, muda utakaotumiwa kufanya delivery, picha ya bidhaa pamoja na usafiri utakao tumia kufikishiwa bidhaa yako.

Mnunuzi akisha jaza taarifa hizi, atapaswa kubofya button ya submit. Aki submit, taarifa hizi zitamfikia muuzaji wake kwa njia ya sms pamoja na notification kwneye app.

Muuzaji atahitajika kuzipitia taarifa alizojaza mteja kujiridhisha kama ni sahihi. Ataona na picha ya bidhaa ambayo mteja ameiattach. Picha hii mteja anaipata toka kwenye tangazo la muuzaji au kwenye oage ya muuzaji ya mtandaoni. Akijiridhisha kuwa ni sahihi atatakiwa kubofya kitufe cha "Approve Payment". Kama taarifa si sahihi atamwambia mteja wake arekebishe baadhi ya vipengele.

Baada ya kuapprove payment, mteja atapokea control number kwa njia ya sms pamoja na notification kwenye app yake. Mteja atalipa kupitia (tigo pesa au airtel money). Huduma hii iko supported kwenye mitandao hii pekee

Baada ya malipo, muuzaji atajulishwa juu ya malipo yaliyo fanyika. Na kukumbishwa wajibu wake wa kukabidhi bidhaa kwa mteja ndani ya muda waliokubaliana . Wakati huu, pesa ya mteja itakuwa kwenye escrow account kwa kulipindi chote ambacho hii transaction inaendelea.

Baada ya malipo, Mteja atakuwa na option 3.
1. Accept delivery. Baada ya mteja kupokea bidhaa na kujiridhisha kuwa iko sawa. Atapaswa kuclick button ya Accept delivery. Mara tu baada ya kubofya hii button, pesa itakuwa released toka kwebye secure vault kwenda moja kwa moja kwa muuzaji.

2. Mteja kukaa kimya baada ya kupokea bidhaa. Huwa inatokea mara kadhaa mteja kupokea bidhaa na kuignore kubofya kitufe cha Confirm Delivery. Hii inaweza kutokea either kwa makusudi au kwa kupitiwa.

Kwenye changamoto ya aina hii, mfumo utaendelea kusubiri kutimia zile siku walizokubaliana delivery ya bidhaa kufanyika. Masaa kumi na mbili kabla ya siku za delivery kutimia, mteja atapokea sms na notification kumjulisha matumaini ya Payguard kuwa mzigo wake umefika salama, na endapo kama kuna changamoto ariport ndan ya muda huo. Kwani ndani ya hayo masaa 12, Payguard inatarajia kuachia malipo kwa muuzaji

Ujumbe huu utajirudia tena baada ya masaa sita kabla muda wa makubaliano kutimia. Endapo mteja hata confirm delivery wala kuriport changamoto. Mfumo utaassume mzigo unepokelewa na utamlipa muuzaji. (Hii condition ni muhimu sana mteja kuizingatia). Payguard haitabeba lawama baada ya kuachia malipo endapo jitihada za kukumbusha zimefanyika na mnunuzi hakutoa ushirikiano.

3. RISE DISPUTE. Endapo bidhaa haijafika, au imefika lakini inachangamoto au haipo kama mlivyokubaliana. Mteja anahaki ya kurise dispute kwa kubofya button ya rise dispute. Mteja atalazimika kuandika sababu ya yeye kurise dispute.

Baada ya mteja kurise dispute, ujumbe wa sms na notification itamwendea mnunuzi na muuzaji. Utawaarifu muhamala wao wenye control namba **** umeriportiwa kuwa na changamoto. Mfumo utawapa muda wa masaa 72 kuweza kutatua changamoto zao wenyewe. Kipindi chote hiki, muhamala utabakia kwenye secure vault.

Mteja ndiye mwenye uwezo kwa kuondoa shauri endapo wakifikia makubaliano na muuzaji wake ka kuclick button na Resolve dispute. Mteja ajawajibika kuandika makubaliano waliofikia.

Endapo pande hizi mbili zisipokubaliana. Basi wanatakiwa ku escalate mgogoro wao kwenye team ya Payguard. Mtatua mgogoro wa payguard utafungua group ya pande tatu, mteja, mnunuzi na msuluhisi. Msuluhishi atasikiliza malalamiko ya pande zote mbili. Atahitaji ushahidi toka kwa muuzaji na ule wa mteja. Na atalinganisha taarifa hizo na zile ambazo zipo kwenye mfumo wakati wanaanza muhamala. Msuluhishi atafanya maamuzi either ya kurejesha pesa kwa mnunuzi au kumlipa muuzaji kutegemea na uzito wa ushahidi uliokusanywa.

Ndugu zangu. Huduma hii payguard haitafanya bure. Kuna charges kidogo ambazo zitatumika ili kulinda muhamala wako dhidi ya matapeli. Charge hii tunaiita Paygurd fee/ escrow fee.

Kwenye application yako, kuna button imeandijwa Calculator. Ili kufahamu kiwango ambacho Payguard itakucharge. Weka thamani ya muamala wako. Calculator itakupa gharama zetu.

Ila, gharama hizi pia mfumo umetoa option ya kuchagua nani hazilipe kati ya mteja au mnunuzi. Kwa mfano nanunua Saa ya thamani ya sh 100,000. Na fee ikawa ni sh 2000.

Option 1. Mnunuzi alipe.
Hii option mteja atapaswa kulipa sh 102,000/- baadaha muhamala kukamilika. Tutamlipa muuzaji sh 100,000. Shilingi 2000 itabaki kwetu kama gharama zetu kuuliza muamala wako sha sh 100,000

Option 2. Analipa muuzaji.
Payguard inaamini uwepo wake si kwa ajili ya wateja pekee, ipo kwaajili ya kutanua wigo wa masoko ya mikoani kwa wauzaji wa mitandaoni.

Kuna wakati muuzaji yuko tayari kubeba baadhi ua gharama ili kutompoteza mteja.

Wakichagua option hii. Mteja atalioa sh 100,000. Baada ya muamala kukamilika, tutamlipa muuzaji sh 98,000. Tutabaki na 2000 ambayo ni gharama yetu ya ulinzi.

Option 3. Both to share.
Muuzaji na mnunuzi wake wanaweza kukubaliana kushare gharama hizi. Endapo watachagua option hii. Basi mteja atalipa 101,000. Na baada ya muamala kukamilika muuzaji atapokea sh 99,000.

Ni muhimu kujua gharama zetu kabla hujaidhinisha manunuzi kupitia mfumo wetu. Ila nachowahikikishia, gharama zetu ni affordable mno na has value for money.

Mnaweza kujaribu kudownload app hii ya Payguard secure kupitia Playstore na appstore. Tunatarajia kuiingiza sokoni mwanzoni mwa september.

So far. Tunafanya kazi na mitandao miwili pekee, Tigo na Airtel. Tutaendelea kujumuisha mitandao mingine kadri ya soko litakavyohitaji.

Nitaitengenezea thread hii app soon, nakujumuisha picha ya namna inavyofanya kazi.
 
Back
Top Bottom