Nini kilisababisha Kufa kwa “Kupatana”

Nini kilisababisha Kufa kwa “Kupatana”

Jamaa utazani wanashirikiana na matapeli wateja wengi wanalalamika wao hawajali

Mbona wametoa angalizo kwenye site yao pale kuwa mtu asitume hela mpaka apate mzigo. Wanunuzi ndo hawajielewi.

All and all wabongo na biashara za online bado sana.
 
Wali update ikawa na complication nyingi afu wanajua kabsa wabongo hatupendi vitu vigumu gumu..afu baadae watu waka jitokeza kwa wingi wanauza vitu vibovu yani ukienda kukagua mzigo una kuta ni mbovu kabsa .
 
Tena wakainunua hadi Zoom Tanzania ikawa chini yao. Shida matapeli ndo wameiharibu. Na wanunuzi nao ni mazombie sana hivi unawezaje kununua kitu kwa mtu aliye mbali na mkoa uliopo afu unamtumia hela kabisa ilhali mzigo haujauona bado.
Tatizo ni usimamizi wa mauziano. Watu wananunua magari yakiwa Japan bila hata kuonana au kuongea na muuzaji. Mimi nimenunua vitu vingi tu kupitia app ya AliExpress
 
Nje ya mada Kuna kile kipindi cha kupatanisha watu EATV sijui kwa nini yule master aliamua kuacha kilikuwa kipindi kizuri kweli
Ni Chanel Ten kikiongozwa na Frank Mtao mume wa kwanza wa Chuchu Hansi anayeishi na Ray Kigosi. Aliwapatanisha Zay B na Sister P ikashindikana live. Then Dudu Baya na Mr.Nive
 
Huu mtandao tatizo lilianza walipoungana na Zoom. Ikawa ya kijinga kweli ndo mpaka leo.
 
Ni Chanel Ten kikiongozwa na Frank Mtao. Aliwapatanisha Zay B na Sister P ikashindikana live. Then Dudu Baya na Mr.Nive

Unazungumzia NANI NI NANI, Kile ni kipindi cha wasanii kuongelea hustle zao na kazi zao kiujumla na sio kupatanisha. Ile ishu ya Zay B na Sister ilitokea tu, Mambo yalivyokuwa mengi mtaani jamaa kama mdau wa sanaa akawaita studio kumalizana.
 
Back
Top Bottom