Nini kilisababisha urafiki na Besti/ Mshkaji wako kufa?

Nini kilisababisha urafiki na Besti/ Mshkaji wako kufa?

Cute Wife

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2023
Posts
1,906
Reaction score
5,000
Kwema team MMU?

Marafiki ni watu muhimu na wenye manufaa makubwa kwetu, japokuwa wakati mwingine anaweza kuwa kichomi akavuruga maisha yako?

Mimi na rafiki yangu mmoja urafiki ulikufa sababu hakulipa deni langu, kila nikimdai anatafuta vijisababu vya kunikwepa, jamaa ananikwepa mpaka kesho:pepeLaughing:.

Kwa upande wako nini kilisababisha urafiki wako na besti yako/mshkaji wako kufa?
 
Daaah ni stori ndefu, siku nikiipata wasaa nitashusha kisa kizima, ila Kwa ufupi fala kaoa shemeji yake (mchepuko wangu) ilihali alikuwa anajua kila kitu.

Fala namchukia kila siku, kibaya zaidi nilimtumia pesa ya kuchukulia mzigo wa biashara jamaa ndo akafanya ya kuolea.

Sent from my Infinix X6516 using JamiiForums mobile app
 
Sasa Mkuu dada si alikuwa free kuolewa?[emoji1787][emoji1787]
Jamaa alikuwa na wake wawili, kwahyo huyu akawa watatu, wakati mi sikuwa hata na mmoja ndo nltaka kumfanya awe mke, ila mwamba akapita naye.

Ni rafiki wa utotoni mpk ukubwani Kwa maana tulisoma pamoja form 1 had 6, na baada ya hapo tukawa tunafanya mishe pamoja na kabla jamaa hajaanza kuoa oa, katumia sana ghetto langu kuulia kima, ila mwsho wa siku kmmk kapita na manzi wangu, huyu fala siwezi msamehe maisha.

Baada ya tukio alinifanya nisikilize mwezi mzima wimbo wa SumaLee na Joh Makini - Rafiki,
Rafiki mkia wa FISI, ukidiriki atakufilisi

Sent from my Infinix X6516 using JamiiForums mobile app
 
Daaah ni stori ndefu, siku nikiipata wasaa nitashusha kisa kizima, ila Kwa ufupi fala kaoa shemeji yake (mchepuko wangu) ilihali alikuwa anajua kila kitu.

Fala namchukia kila siku, kibaya zaidi nilimtumia pesa ya kuchukulia mzigo wa biashara jamaa ndo akafanya ya kuolea.

Sent from my Infinix X6516 using JamiiForums mobile app
Yupo sahihi maana mwanamke alitaka ndoa na siyo kutumika kama mchepuko
 
Kwema team MMU?

Marafiki ni watu muhimu na wenye manufaa makubwa kwetu, japokuwa wakati mwingine anaweza kuwa kichomi akavuruga maisha yako?

Mimi na rafiki yangu mmoja urafiki ulikufa sababu hakulipa deni langu, kila nikimdai anatafuta vijisababu vya kunikwepa, jamaa ananikwepa mpaka kesho:pepeLaughing:.

Kwa upande wako nini kilisababisha urafiki wako na besti yako/mshkaji wako kufa?
Kwa upande wangu, mshikaji wangu tulikuwa tunaishi maeneo yanayokaribiana. Tulikuwa na utaratibu wa kuambiana kuwa nakuja maeneo ya kwenu utanikuta baa fulani. Sasa siku moja nikamwambia hivyo kuwa nipo mitaa yake hivyo atanikuta baa fulani. Mwenzangu alikuwa anajenga mahala pengine ili baada ya kumaliza ujenzi ahamie huko (sikuwa nalijua hili). Kumbe siku namwambia nipo mitaa yake, mwenzangu amehama kama wiki imepita. Ila akaniambia nimsubiri anakuja. Nilikaa hapo mpaka usiku mkubwa. Nikaondoka. Siku za baadaye nikaja sikia kuwa alihama na siku ile aliyoniweka mitaa aliyohama hakuwa mitaa hiyo. Umbali ulitusaidia kuuvunja ushikaji.
 
Mimi sio rafiki tu nilivunja cicle nzima ya marafiki, niligundua ni wanafiki, mipango yangu kikazi inakwama kwasababu wanatia mkono, nikipata shida wanafurahia moyoni ,taarifa za matatizoyangu zina wafurahisha zaidi kuliko za mafanikio yangu.
Nikasema msinitanie nikapiga block wote nikatafuta watu aina nyingine ya kuwa nao karibu. Mambo ni shwarii
 
Kuna jamaa tumemaliza chuo tupo mtaa tunasota hatuna ajira
Mwamba Mungu kamjalia akapata, aisee tulimpigia simu hakupokea na sisi tukakaa kimyaa, tukajitafuta kimtaaa, miaka ikapita jamaa akapiga simu mwenyewe akasema anakuja kuniona alivokuja akakuta tushajipata na tuko mbali sana ya yeye anahangaikia mshahara wa laki 5 mwezi mzima,
Basi jamaa aliona aibu, kuona alitukataa washikaji kisa ajira sasa kufika anaona hata robo ya tulichonacho kwenye ajira hawezi pata

Urafiki ukafa hivo
Alipiga cm akachoka
 
Back
Top Bottom