Nini kilisababisha urafiki na Besti/ Mshkaji wako kufa?

Nini kilisababisha urafiki na Besti/ Mshkaji wako kufa?

Kwema team MMU?

Marafiki ni watu muhimu na wenye manufaa makubwa kwetu, japokuwa wakati mwingine anaweza kuwa kichomi akavuruga maisha yako?

Mimi na rafiki yangu mmoja urafiki ulikufa sababu hakulipa deni langu, kila nikimdai anatafuta vijisababu vya kunikwepa, jamaa ananikwepa mpaka kesho:pepeLaughing:.

Kwa upande wako nini kilisababisha urafiki wako na besti yako/mshkaji wako kufa?
Wakati mwingine tunapaswa kuvumiliana kwenye madhaifu ili kumantain urafiki wetu.
Ingekua mimi ndio wewe ningemtafuta huyo rafiki hadi nimpate, kisha nikaongea nae mambo mengine kabisa tofauti na deni langu na baada ya hapo naamini urafiki wetu ungedumu.
 
urafiki ulikufa sababu ya ubinafsi. kwako anataka kunywa bia ila kwake unywe pombe kali.
pili kila jambo lako lenye kutaka kupanga ukimueleza anakuwa na kinyongo au kukukatisha tamaa
Kwa maelezo haya, huyo sio rafiki mkuu..... achana nae
 
Daaah ni stori ndefu, siku nikiipata wasaa nitashusha kisa kizima, ila Kwa ufupi fala kaoa shemeji yake (mchepuko wangu) ilihali alikuwa anajua kila kitu.

Fala namchukia kila siku, kibaya zaidi nilimtumia pesa ya kuchukulia mzigo wa biashara jamaa ndo akafanya ya kuolea.

Sent from my Infinix X6516 using JamiiForums mobile app
Kwahiyo ulivunja urafiki sababu ya pesa uliyomkopesha au sababu kaoa shemeji yake ambaye alikuwa loose ball. Kwan inaonekana mpkaa jmaa katupiamo mistari yake ww ulikua haueleweki.
 
Kadri tulivyokua tunakua ndio nikajua jamaa yuko rough sana then si mkweli, anaweza akakulilia shida we ukatoa akiba ukijua hana, kumbe na yeye anakiasi chake cha pesa cha akiba hataki kukigusa “no matter what”. Nikaona huyu si mtu mwema
 
Kwema team MMU?

Marafiki ni watu muhimu na wenye manufaa makubwa kwetu, japokuwa wakati mwingine anaweza kuwa kichomi akavuruga maisha yako?

Mimi na rafiki yangu mmoja urafiki ulikufa sababu hakulipa deni langu, kila nikimdai anatafuta vijisababu vya kunikwepa, jamaa ananikwepa mpaka kesho:pepeLaughing:.

Kwa upande wako nini kilisababisha urafiki wako na besti yako/mshkaji wako kufa?
Kumsaidia kupanda kimaisha, after mafanikio nikageukwa live. I had no choice
 
kwa umbea wangu tu yani full kumteta na siri zake natangaza alinisuuuuta akamalizia i love you but i cant keep you jaman alikua ana roho nzuri msafi mtoaji mtu wa kumtegemea nililia niliomba msamaha nilituma watu akasema tupendane mbali mbali kila nilivojipendekeza waapi ananichangamkia vizuri ila hataki ukarib kabisaaa nammis ampenda kanivumilia megi sana na hii ni stori ya kutunga asanteni.
 
Mimi sio rafiki tu nilivunja cicle nzima ya marafiki, niligundua ni wanafiki, mipango yangu kikazi inakwama kwasababu wanatia mkono, nikipata shida wanafurahia moyoni ,taarifa za matatizoyangu zina wafurahisha zaidi kuliko za mafanikio yangu.
Nikasema msinitanie nikapiga block wote nikatafuta watu aina nyingine ya kuwa nao karibu. Mambo ni shwarii
Huu ulikuwa ujasiri mkubwa sana
 
Jamaa alikuwa na wake wawili, kwahyo huyu akawa watatu, wakati mi sikuwa hata na mmoja ndo nltaka kumfanya awe mke, ila mwamba akapita naye.

Ni rafiki wa utotoni mpk ukubwani Kwa maana tulisoma pamoja form 1 had 6, na baada ya hapo tukawa tunafanya mishe pamoja na kabla jamaa hajaanza kuoa oa, katumia sana ghetto langu kuulia kima, ila mwsho wa siku kmmk kapita na manzi wangu, huyu fala siwezi msamehe maisha.

Baada ya tukio alinifanya nisikilize mwezi mzima wimbo wa SumaLee na Joh Makini - Rafiki,
Rafiki mkia wa FISI, ukidiriki atakufilisi

Sent from my Infinix X6516 using JamiiForums mobile app
Nawe tafuta mnyonge ummegee mkuu
 
Nilipokea simu kwa rafiki mwingine saa nane usiku mazungumzo yalikua hivi "

Forest Hill unalala Sana vipi??ndugu yako Danny yupo na Shemeji My Affair unajua??usingizi ukakata pale pale,
Hadi Leo Mimi na Danny salamu tu,japo tunajuana since vidudu
 
Back
Top Bottom