Nini kilitokea B-hits

Nini kilitokea B-hits

Kwa ile production ya Bye bye,beat kalii,mashairi makalii pale Pancho Latino aliiifanyia haki ngoma ile!Ngoma yangu bora kwa Joh Makini kwa muda wote
Pancho mkali the latino mafia anajua hata matango pori kaifanya vzuri
 
Miaka kama minne iliyopita B-hits ilikuwa kati ya studio zilizokuwa zikitoa hits nyingi chini ya pancho latino mafia na hammy B.
Mtakumbuka ngoma kama
Bado nipo nipo - FA
Dakika moja tu - FA ft AY
Amore- Baby Madaha
Show za joh - joh makini
Closer - Vannessa Mdee
Bye bye - Joh Makini
Leo - AY ft avril
Ndole - Mabeste ft Deddy
Sirudi tena - Mabeste ft Jux
Baadaye sana - Mabeste
Destiny - mrap ft deddy
Msiache kuongea- FA ft jaydee
Unanijua unaniskia - FA
Nangoja ageuke - FA & AY

na ngoma kibao. Mara ghafla wasanii wakahama almost wote.
Siamini kama uwezo wa Pancho au hammy B umeshuka ila kutakuwa na sababu maana siku hizi B-hits haina hits kama zamani
aysee Pancho Pancho panchoooo...Daah jamaa hata beat za michiriku alikuwa anaziwezea sana,kama ile majaliwa ya Omar Omar au Kazi yangu ya dukaniiii oooh ooooh daaaah namkubali sana basi tu...kuna producers sikutaka kabisa wapotee kama vile Pancho,Prof. Ludigo, Hermy B, daaah...game hii
 
Kitambo nilishasikia master jay analalamika kuwa wao kama wao hawana ushirikiano.
Ukikataa kumrekodia mtu bure au kwa bei chee kesho anaenda studio ya huko uswahilini unashangaa katoa wimbo ume hit na bure kabisa na wasanii wote wanahamia huko
Ndio maana master jay alijitoa izi mambo kitambo sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom