Allen Kilewella
JF-Expert Member
- Sep 30, 2011
- 21,470
- 40,593
Wakati bado tunaendelea kuomboleza kifo cha mfanyakazi wa TRA, Marehemu Amani Simbayao, Kuna jambo limenishangaza kidogo.
Kumbe Mwigulu Nchemba yupo. Maana zaidi ya kumkumbuka ninaposafiri na kuona mamia ya mawe huko kwenye barabara ninazopita, yameandikwa "Mwigulu Rais 2015", huwa simsikii akijibu hoja na maswali mbali mbali kwa namna ya uharaka aliouonesha kwenye jambo hili.
Rwanda ni nchi ambayo kijografia, inaifanya kutegemea nchi nyingine ili kupata mizigo yake inayopitia baharini.
Kwa kifupi Rwanda haina bahari na kwa ivo haina bandari ya baharini.
Siku za nyuma Rwanda baada ya DRC ndiyo ilikuwa nchi inayoitegemea Bandari ya Dar es salaam kusafirishia mizigo yake kutoka na kwenda Rwanda.
Lakini baadae Rwanda ikaleta sera kwamba nchi hiyo isiwe tegemezi wa kupitishia mizigo kwenye nchi moja. Hivyo ikaanza kupitishia mizigo yake na Kenya pia.
Lakini ndani ya mwaka mmoja mambo haya yametokea. Kwanza shehena ya mizigo kupitia Kenya imeongezeka na mizigo inayopitia Tanzania imepungua.
Mizigo yenye thamani ya Dola za Kimarekani milioni 121.45 sawa ongezeko la asilimia 361.43 (361.43%) imepitia Kenya ukilinganisha na Oktoba Mwaka jana 2023.
Idadi hiyo ya mizigo kupitia Kenya unaifanya nchi hiyo kuwa ya pili nyuma ya China ambayo imeingiza Rwanda mizigo yenye thamani ya Dola za Kimarekani 142.08 sawa na ongezeko la 34.95% .
Kwa Tanzania uingizaji wa mizigo Rwanda kupitia Tanzania umekuwa ukipungua kwa karibia 39.04% kwa msingi wa mwezi kwa mwezi na kwa mwaka mzima uingizaji mizigo Rwanda kupitia Tanzania umepungua kwa 30.16%.
Ukilinganisha Mwezi Oktoba 2023, Rwanda imepitishia Tanzania Mizigo yenye thamani ya Dola za kimarekani milioni 57.38 pekee.
Wazee wa kushinda 99% nini kinaendelea hapa.