econonist
JF-Expert Member
- Jul 11, 2015
- 20,189
- 29,663
Hao unaosema wamekuwa na mgombea mmoja wamebadilisha wenyeviti mara nne ndani ya miaka 20. Vyama vya upinzani vipo na watu walewale, Mbatia, Lipumba, Mbowe, Mrema nk nk. Wenyeviti wa vyama vya siasa vya upinzani ni madikteta wakubwa. Bahati mbaya wafuasi wao wamejaa mahaba kiasi kwamba hawaoni udikteta huo. Lazima kuwe na ukomo wa mtu kuongoza, tofauti na hapo ni kuanzisha mazalia ya madikteta.
Mbona unajicontradict. Unasema wafuasi wao wana mahaba ya kutaka waongoze. Hivi kuna ubaya gani wafuasi na wanachama wa upinzani wakimpenda mwenyekiti wao na kutaka aongoze.
Hao CCM unaowasema, huwa wanachaguliwa kwa mahaba au itifaki. Yani ukishakuwa rais lazima uwe mwenyekiti wa CCM wanakupenda au hawakupendi. Sasa kwa upinzani ni tofauti, wanachama wakikupenda unachaguliwa tu.
Udikteta upo CCM ambapo Rais Anakuwa Mwenyekiti bila kushindanishwa na yeyote. Na kura inapigwa kiitifaki maafisa usalama wakiwa wamejaa kwenye mkutano.