Chadema haijafa bado ipo hai ila moja ya sababu kubwa inayopelekea Chadema kuwa chama dhaifu ni pale walipoamua kuukana ukweli wao wenyewe kwakutaka kumsafisha fisadi waliyezunguka Nchi nzima kumtukana!!. Ujio wa Eddo 2015 ndani ya chadema uliondoa uaminifu hasa kwa watu wenye uelewa mpana juu ya siasa zetu wakaona Chadema na viongozi wao wakuu hawapo kwaajili ya Tz bali wao kwanza, mpaka Leo ukimfuata mwanachadema ukamuuliza ni sababu zipi ziliifanya Chadema kumpokea Eddo hawawezi kukupa... Kuanzia hapo watu timamu wakaona hamna la maana zaidi ya ubabaishaji mtupu.
Sababu nyingine ni utawala wa Magufuli na uchaguzi wa 2020, magufuli alikuwa na nia hasa yakuiondoa Nchi kwenye mfumo wa vyama vingi kuipeleka chama kimoja. Siku zote uhai wa chama cha siasa ni kufanya siasa na kuuza sera zao kwa wananchi, Chadema na wapinzani wengine hawakupata tena hiyo fursa automatically Nchi ikabaki kusikia sifa na mapambio yanayoimbwa juu ya chama kimoja Cha CCM chini ya Magufuli.
Pia kutokuwa na ukomo wakiuongozi kwa kiongozi mkuu wa chama, hii inadhoofisha na inaondoa uhalisia wa chadema na wanachokipigania hasa ni Demokrasia ipi wanayoitaka wao?, Haiwezekani mtu mmoja ndio akawa Bora kwa vipindi vyote vya zaidi ya miaka 15 bila kuachia ngazi ili Chadema ipate kiongozi mwingine ambaye nae atatoa dira na mwenendo mpya kuhakikisha wanachukua dola.
Ukiwasililiza Chadema wanavyoimba suala la kujenga taasisi imara za kiuongozi kuliko kumjenga mtu au kimtegemea mtu imara kwa mbaali utawaona wapo siriasi lakini hebu tafakari wao Wana hizo taasisi imara? Kama wanazo Kwanini FAM haachi uongozi?, Jibu lao ni jepesi sana eti mwamba tuvushe!! Mara eti hanunuliki kinachoshangaza ni Kumbe Chadema sio chama cha kitaasisi bali ni chama kinachotegemea maamzi ya mtu mmoja. Ili Chadema ichukue dola inahitaji ipate kiongozi kijana tena asiyemwoga.... Huyu Mbowe ni mandonga mtupu aliyepata umaarufu kupitia mgongo wa Dr slaa na kazi nzuri za vijana wa chadema.