Nini kimeiua CHADEMA? Walikosea wapi? Vyama vingine vya upinzani vijifunze kuepuka kibri cha kupendwa


Mbona unajicontradict. Unasema wafuasi wao wana mahaba ya kutaka waongoze. Hivi kuna ubaya gani wafuasi na wanachama wa upinzani wakimpenda mwenyekiti wao na kutaka aongoze.

Hao CCM unaowasema, huwa wanachaguliwa kwa mahaba au itifaki. Yani ukishakuwa rais lazima uwe mwenyekiti wa CCM wanakupenda au hawakupendi. Sasa kwa upinzani ni tofauti, wanachama wakikupenda unachaguliwa tu.

Udikteta upo CCM ambapo Rais Anakuwa Mwenyekiti bila kushindanishwa na yeyote. Na kura inapigwa kiitifaki maafisa usalama wakiwa wamejaa kwenye mkutano.
 
ACT ni chama kipya hauwezi tegemea kiwe na nguvu kama CDM hata kama Zitto ni nguli wa siasa.

Kila mtu ana haki ya kulalamikia utendaji wa chombo cha wengi kama chama cha siasa. Hata dini zikitenda ndivyo sivyo zitalalamikiwa na waumini wao na wasio waumini wao.

Hao wamerudi CCM baada ya kuona chama kinachojiita cha demokrasia hakina demokrasia yoyote ndani yake. Kupitia udikteta mwenyekiti alimpitisha Lowassa kugombea mwaka 2015. Mtu mwenye akili na anayesimamia principle hawezi kaa kwenye taasisi ya namna hiyo.
 

Labda umesahau nikukumbushe mambo mawili, hao akina kitila, mwigamba, msando, Anna mghwira et al, walihamia CCM wakitokea ACT sio CHADEMA usipotoshe.

Pia, nikukumbushe jambo moja, kwanini Lowassa alipewa kugombea urais chadema. Mpango ulikuwa Lipumba, Dr Kulangwa wa NCCR na Dr Slaa wakae pamoja wakubaliane nani agombee urais. Wakashindwa kukubaliana kwenye vikao vyote kila mtu akitaka awe mgombea.

Sasa Chadema walipoamua kumpitisha slaa, siku waliyopanga kumtangaza Slaa akagoma akasema anatakiwa kutangazwa kwa tukio kubwa. Sasa baada ya kuona mbwembwe ni nyingi ndio likatokea suala la Lowassa, . Lowassa ilikuwa last resort na Dr Slaa hakuwa na nguvu ya kupambana na Magufuli.
 
Madikteta wote husema kuwa wanaongoza kwa mandate ya watu. Hukuna dikteta atakayekuambia kuwa anaforce kuongoza. Na vibaraka wa madikteta nao hutoa hizi kauli,
"Hivi kuna ubaya gani wafuasi na wanachama wa upinzani wakimpenda mwenyekiti wao na kutaka aongoze."
Hata Idi Amin alisema anaongoza kwa matakwa ya watu na anapendwa na watu. Hata Nyerere angeamua ile 1985 achaguliwe aendelee na urais angechaguliwa na kuendelea. Lakini aliamua kutoka na kuweka ukomo, kitu ambacho hawa madikteta kwenye vyama vya siasa hawataki kabisa.

Huko unakosema kuna udikteta wanabadilisha wenyeviti wa chama kila miaka kumi.
 

Nimechy, eti CDM imekufa. Haya ndio matamanio ya kila mwanaccm. Siku 2 tatu CDM wakianza mambo yao utasikia vilio vya wanaccm kuwa CDM wanaharibu amani ya nchi. Na ikifika uchaguzi CCM ndio wanageuka vituko kwa kupora chaguzi kwa mbeleko ya vyombo vya dola.
 
 

Mbona unatoa mifano ya marais wa nchi? Wakati wewe unalalamikia viongozi wa chama?. Hakuna udikteta kwenye level ya vyama , udikteta upo kwenye level za nchi.
 
Walivyo na mihemko kama wajumbe wa VICOBA vya uswahilini sijui kama mtaelewana😂😂😂😂

Ukimgusa tu mtu wa chama hicho anapayuka kama yuko kwenye sinagogi:
 
Walivyo na mihemko kama wajumbe wa VICOBA vya uswahilini sijui kama mtaelewana😂😂😂😂

Ukimgusa tu mtu wa chama hicho anapayuka kama yuko kwenye sinagogi:

Chadema imetabiriwa kufa tangu 2019 mpaka leo waliotaka kuiua wanakufa wao wanaiacha.
 

Huwezi kuwa dictator bila nguvu ya vyombo vya dola. Inaonekana ww ni bendera fuata upepo na huu uzi umeshakuzidi pumzi, hivyo unarukia kila neno unalosikia ili ujiokoe.
 
Huko ni safari ya kisiasa, kwanini wakina Msando walitoka CDM kwanza. Tuangalie kiini. Na hiyo habari ya Slaa kugoma sababu ya kutaka mbwembwe nyingi ni porojo tu zisizoingia akilini mwa mtu mwenye akili timamu. Na hata kama angetaka mbwembwe nyingi, ilishindikana vipi? Upitishwaji wa Lowassa ulikuwa wa kidikteta usiofuata misingi. ndiyo uliowakimbiza Slaa chamani, na hilo linaingia akilini.
 
Chadema imetabiriwa kufa tangu 2019 mpaka leo waliotaka kuiua wanakufa wao wanaiacha.
Kumbe bado iko hai? Sasa walivyokua wanalilia uhuru wa kutoa maoni, walivyokua wanalalamika demokrasia hamna mbona saizi uhuru wanao na hali ni mbaya zaidi ila siwaskii wakisema. Ufisadi umezidi, maisha yamepanda bei, tozo kila kona ila yameufyata.

So shida yao ilikua uhuru wa kuzungumzia nini haswa? Au uhuru wa kutukana rais! How pathetic
 

Hoja yako hapa ni ipi, ni CDM au Mandonga?
 
Huwezi kuwa dictator bila nguvu ya vyombo vya dola. Inaonekana ww ni bendera fuata upepo na huu uzi umeshakuzidi pumzi, hivyo unarukia kila neno unalosikia ili ujiokoe.
Kuwa dikteta chamani huhitaji vyombo vya dola. Unahitaji vibaraka, ulaghai na kuhonga vyeo au pesa. na nikuambie tu, nguvu ya madikteta wote duniani haipo kwenye vyombo vya dola, ipo kwa vibaraka.
 

Kupanda kwa bei unasubiri CDM wakusemee, sema ww maana hakuna aliyekuzuia. Au umekaa mahali unasubiri kusemewa na wengine?
 
Mbona unatoa mifano ya marais wa nchi? Wakati wewe unalalamikia viongozi wa chama?. Hakuna udikteta kwenye level ya vyama , udikteta upo kwenye level za nchi.
Nakupa 101 za Udikteta. Udikteta si kwa nchi tu, unaweza tokea ndani ya taasisi yoyote ile. Kama unadhani udikteta ni mpaka aufanye urais bado huijui siasa, na ndiyo maana unatetea udikteta wa wazi.
 
Kuwa dikteta chamani huhitaji vyombo vya dola. Unahitaji vibaraka, ulaghai na kuhonga vyeo au pesa. na nikuambie tu, nguvu ya madikteta wote duniani haipo kwenye vyombo vya dola, ipo kwa vibaraka.

Udictator ni matumizi ya nguvu, na sio ulaghai au kuwa na wapambe. Unapokuwa bendera fuata upepo hizi ndio huwa hoja.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…