Nini kimeiua CHADEMA? Walikosea wapi? Vyama vingine vya upinzani vijifunze kuepuka kibri cha kupendwa

Nini kimeiua CHADEMA? Walikosea wapi? Vyama vingine vya upinzani vijifunze kuepuka kibri cha kupendwa

Kuna wengi sn wanaweza kufikiria nini kilisababisha anguko la Chadema wapo wachambuzi wengi wa masuala ya siasa wanaweza Kuja kuelezea mengi Sana yaliyosababisha anguko la kilichokuwa chama kikuu cha upinzani zifuatazo ni baadhi ya hoja zinazotoa ushahidi juu ya kiini cha anguko la Chadema

Udikteta: Pamoja na kujitabanaisha kama chama kikuu cha upinzani lakini Chadema kilikumbwa na tafsiri batili ya Jina na matendo yake, Chama cha kidemokrasia kinachoendeshwa kidikteta kwa kung'ang'aniwa na mtu mmoja kukiongoza kwa muda mrefu na kukifanya chama kama Mali binafsi ya Familia kwa mfano Mbowe amekuwepo madarakani toka enzi za Mzee mkapa, mkapa aliondoka akamuacha Mbowe kama mwenyekiti baadaye akaja kikwete akamuacha Mbowe kama mwenyekiti

akaja Magufuli akamuacha Mbowe kama mwenyekiti na sasa ni Samia, kwa lugha nyingine ni kwamba CCM imepata wenyeviti wanne tofauti lkn Chadema kikiwa na mwenyekiti mmoja tu naye ni Freeman Alkael Mbowe

Ni kosa kubwa sana kuruhusu mawazo ya mtu mmoja anayekosea Mara kwa Mara kutowajibika pale anaposhindwa
uchaguzi wa Mwaka 2005 ulitosha kabisa kumuondosha Mbowe kama mwenyekiti wa Chadema

Lakini ameng'ang'ania madaraka tu utazani kupe na hatimaye America chama kwa kunyonya damu yote

Mbowe Hana Mamlaka ya kudai katiba mpya kwa sababu yeye mwenyewe ni mvurugaji namba moja wa katiba ndani ya chama chake

tutaendelea kujadili udikteta kama kigezo cha anguko la Chadema namba 2
Sidhani kama Chadema kimekufa bali nakiona kikiwa na makali zaidi kama wakichanga karata zao vizuri !!
 
Udictator ni matumizi ya nguvu, na sio ulaghai au kuwa na wapambe. Unapokuwa bendera fuata upepo hizi ndio huwa hoja.
Udikteta siyo matumizi ya nguvu. Udikteta ni kuwa na final say kwenye maamuzi bila kupingwa. Ulianzishwa na waroma. wakati wa dharura au emergency yoyote, waliwapa maconsular wao nguvu za kidikteta. Hapo waliweza kufanya jambo lolote bila kulazimika kupitia kwenye senate.
 
Kama Mbowe angekuwa na nguvu hiyo basi Mgombea urais a urais wa CDM 2020 angekuwa Nyalandu na sio Lisu. Yeye alimtaka Nyalandu na sio Lisu. Katafute sababu nyingine sio hiki unachojaribu kusema.
 
Hakuna chochote unachomaanisha zaidi ya kuongea utoto.
Kumekucha🤣 wazee wa mihemko. Mlikua mnalilia uhuru wa kutoa maoni ya kulalama tu kutafuta huruma ya wanachi. Mkisimama majukwaani ni kutukana marais eti in the name of freedom of speech. Chadema ikishika nchi saizi hiyo safu itakaaje. Hakuna hata mmoja mwenye uwezo wa kuendesha serikali. Familia tu zimewashinda
 
Kama Mbowe angekuwa na nguvu hiyo basi Mgombea urais a urais wa CDM 2020 angekuwa Nyalandu na sio Lisu. Yeye alimtaka Nyalandu na sio Lisu. Katafute sababu nyingine sio hiki unachojaribu kusema.
Madikteta nao kuna muda wananywea, lakini haiondoi udikteta wao. CDM ni chama kizuri ila hakina demokrasia kabisa licha ya kujiita chama cha demokrasia.
 
Mi nafikiri adui akifa au akikosea ndio vizuri. Mnaanza tena kumkosoa adui si mwacheni ajifie.
 
Kwanini chadema wasiweze?. Mwaka 2015 walipata asilimia 40 ya kura za urais, ina maana walibakia asilimia 10 tu wafikishe 50. Hivi chama chenye margin ya asilimia 10, hakiwezi kupewa madaraka?. Yani pamoja na tume ya uchaguzi kuwa ya rais na upendeleo kuwa wa wazi, bado chadema ilifanikiwa kuzoa asilimia 40.

Hivi fikiria kwanini mwaka 2020 mizengwe ilikuwa mingi dhidi ya chadema? Issue ni kwamba ukiachia chadema nafasi ikafanya siasa kwa uhuru , tume huru hakuna kubambikiana kesi, utakuja kuniambia. Mazingira ya sasa yana ifavour CCM sana.
Ni kweli ukitaka kujuwa Chadema kwanini walipata hizo 40% ni kwa sababu walimchukuwa mtu maarufu wa CCM lakini wao kama wao wajaribu tuone watapata ngapi. Mimi sina shida na Chadema hoja yangu watu hawajui tofauti ya CCM na Chadema ni mambo gani makubwa wanatofautiana? kwa maana kisera mimi sijui ndio inawapa watu shida. CCM sio wakamilifu wanashida sana lakini mtu wa kawaida anaona huyu namjuwa huyo anayetaka nchi sijui hata sera zake na ukweli kabisa naomba kujuwa tofauti kubwa baina ya CCM na Chadema ni nini?
 
Hoja yako hapa ni ipi, ni CDM au Mandonga?
Hoja yangu ni Chadema ni chama kikubwa lakini hawajui wanasimamia nini, Mimi sijui nini wanasimamia wana sera gani iwe kiuchumi, kijamii, kielimu hata sera za nje wanasimama wapi tujue huyu CDM na huyu CCM, hawana sera wanatumia muda mwingi kupinga lakini bila solution wa wanalopinga. Hata waje waseme mkituchagua sera za kilimo kitabalika tutafanya moja mbili tatu... hakuna
 
Kiukweli CHADEMA haijafa, sema imekuwa "dormant".

Siku CHADEMA ikipata mwenyekiti mpya mwenye kujitambua na mwenye misimamo mikali, hakika CHADEMA watachukua madaraka ya hii nchi.
 
Hivi kumbe CHADEMA imekufa halafu msajili bado hajaifuta kwenye daftari? Hawa CCM nao maboya tu, wanqjadiliana pembeni na Chama marehemu?
 
Dr Slaa huyu huyu zuzu asiyejielewa? Angekuwa na msima walau 10% ya Mbowe angalau angekuwa 'mtu', mtu kadindisha kuunga mkono 'juhudi' licha ya kuharibiwa na kufilisiwa investments kibao unadhani ni wangapi wanaliweza hilo.
Lowassa businesses zake zimeguswa kidogo tu kaufyata na kurudi tena akapokelewa kwa bashasha ikulu Jiwe akiuhesabu kuwa ni ushindi wa ndugu.
Slaa kaijenga Chadema kuliko mwanachama yeyote!! Ni kipindi Cha ukatibu mkuu wake ndipo tumeona hamasa na msisimko wa watu kuipenda na kuitambua Chadema. Mbowe ni mandonga mkimya...
 
CHADEMA ulikufa kwa mtutu na kunyimwa Haki ya kikatiba ya kushinda uchaguzi!

Kinachofanyika kwa Sasa ni kutibu majeraha Yao kwa maridhiano AMBAYO yanaendelea!!
 
Kumekucha🤣 wazee wa mihemko. Mlikua mnalilia uhuru wa kutoa maoni ya kulalama tu kutafuta huruma ya wanachi. Mkisimama majukwaani ni kutukana marais eti in the name of freedom of speech. Chadema ikishika nchi saizi hiyo safu itakaaje. Hakuna hata mmoja mwenye uwezo wa kuendesha serikali. Familia tu zimewashinda

Hakuna mtu Atashindwa kazi alivyoweza Magufuli na JK.
 
Hoja yangu ni Chadema ni chama kikubwa lakini hawajui wanasimamia nini, Mimi sijui nini wanasimamia wana sera gani iwe kiuchumi, kijamii, kielimu hata sera za nje wanasimama wapi tujue huyu CDM na huyu CCM, hawana sera wanatumia muda mwingi kupinga lakini bila solution wa wanalopinga. Hata waje waseme mkituchagua sera za kilimo kitabalika tutafanya moja mbili tatu... hakuna

Huna ujualo zaidi ya kupiga siasa mfu hapa jukwaani, ndio maana unaongea haya unayongea. Sera za CDM na ilani yao vyote vimekuwa vikiwekwa public, lakini unasubiri propaganda za CCM ndio unakuja kujengea hoja huku mitandaoni.
 
public wapi? mbona mnakuwa wakali mkiulizwa ukweli. CDM ndio sababu kuu ya kutaka mikutano wamepewa ruhusa sasa kama kuweka public inatosha mikutano ya nini? wewe sema hata point 3 tofauti ya CDM na CCM. Hakuna haja ya matusi weka sera huko public ni wapi nipe link niweze kupitia.
 
Naona unatembea na hisia zako mara kutukanwa, mara hakuna sera. Uko hapa jukwaani toka 2015, hujaona sera wala ilani za CDM, unataka mimi nikuwekea link. Kama hukuona muda wote huo, hata ukiwekewa leo utasoma au unashupaza shingo?
 
Kama wana siasa wa chadema ndio attitude yao hiyo basi hata huko kwenye majukwaa mnaenda kufanya nini kama unaamini watu wanazijuwa sera zenu ni wazi mnasafari ndefu sana na siasa imewapita pembeni badala kunishawishi mimi nikuelewe unataka kufanya ni jukumu langu la kusoma sera za CDM🤣. Nataka nikwambie ukweli sijui miaka yote hiyo Chadema wanasimamia nini kwenye itikadi zao. Wahafidhina? mlengo wa kulia? kushoto? au liberal hapo tu sijui ila najuwa wakosoaji wazuri sana ila hawana mbadala. Sababu umeona profile yangu nadhani utaona nimeandika sana kukosoa CCM sana tu ila CDM wana tabia wao hawataki kusikia ukweli kuwa wanashida sana na wao bahati mbaya hawataki ukweli.
 
Hakuna mtu anahitaji ww uelewe sera za CDM, hizo za CCM unazozijua baki nazo hizo hizo boss.
 
Back
Top Bottom