Nini kimejificha nyuma kuahirisha matengenezo ya mfumo wa Luku?

saidoo25

JF-Expert Member
Joined
Jul 4, 2022
Posts
624
Reaction score
1,456
Jioni ya leo Agosti 17,2022 Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) limetoa tangazo la kuahirisha zoezi la matengenezo kinga kwenye mfumo wa LUKU kama ilivyotangazwa mapema hivi leo asubuhi.

Tangazo la awali lilisema Tanesco kuzima mfumo wa kununua Luku kwa siku 4 kuanzia Agosti 22 hadi 25 kuanzia saa 4 usiku hadi saa 1 asubuhi.

Ndio tunajiuliza maswali mengi mlioko jikoni mtusaidie nini kilisababisha kutolewa tangazo hilo na nini kimesababisha kuahirisha zoezi hilo la matengenezo maana hazikutolewa sababu kwenye kuahirisha.
 
Mnafanya Tanesco jimbo is uchaguzi ......
 
Inaonesha jinsi taasisi, wizara, viongozi n.k wasivyounganika kujua kesho, wiki ijayo, mwezi, robo mwaka, mwaka ujao, 2025 n.k wamepanga kufanya nini kama taifa .

TANESCO wana yao, wizara ya fedha na mipango ina mpango kazi wao, Ofisi ya Rais wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa pia wana yao, maDC na MaRC wanakurupuka na maelekezo yao, Bunge pia lina lake jambo ..... ni kusubiri tamko au maagizo na wala wakuu wahusika hawawezi kulitazama jambo ktk upana wake.

Yaani hakuna mfumo wa utawala, serikali na taasisi za umma na binafsi zinazofanya mambo kwa pamoja.

The Tanzanian government has announced that on August 23, 2022, a population and housing census will be held, which was last
 
Walikuwa wanafanya sensa...

Wangapi ni watii kwao wakosikia agizo la Tanesco watawahi kununua umeme.

Wangapi ni waoga wakitishiwa kidogo wanatii bila kusubiri dedilaini.

Wangapi hawajui kinachoendelea.

Wangapi ni maligendari hawajajigusa kuwahi kununua umeme kuondoa keos ya foleni na jam kwenye mitandao ya kununulia umeme.

Sensa yao imekamilika wameshapata data walizokuwa wanahitaji aina ya wateja walionao.

Wako mbioni kuleta product mpya ya umeme kulingana na aina ya wateja...

😉.
 
Serikali inayoishi kwa kuzingatia mtiririko wa matukio nje ya mipango ndo huwa ivo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…