Nini kimelikumba Jeshi letu? Imekuwaje linatumika kwa ajili ya kampeni za CCM?

Nini kimelikumba Jeshi letu? Imekuwaje linatumika kwa ajili ya kampeni za CCM?

Lord Denning

JF-Expert Member
Joined
Jun 3, 2015
Posts
23,491
Reaction score
57,973
Taasisi tuliyoitegemea zaidi kuwa ya mwisho kama tegemeo kwa Watanzania inaoneka nayo imebebwa na maji ya Chama cha Mapinduzi.

Taasisi iliyotegemewa kwa weredi, umakini na kuwa bold dhidi ya siasa na wanasiasa sasa inaonekana imekuwa compromised.

Inasikitisha sana kuona helicopter za Jeshi letu aina ya Mi 17 zikitumika kwenye kampeni za Chama cha Mapinduzi.

Inasikitisha zaidi sasaivi vijana waliopo kwenye Makambi ya Jeshi wanatolewa kwenda kujaza watu kwenye mikutano ya CCM.

Jeshi linapofikia hapa ni dhahiri kuwa Watanzania hatuna tena Jeshi la Wananchi. Tuna kikundi cha Wanajeshi kinachotumika kwa maslahi ya CCM.

Tumekwisha
Chini ni picha za ndege Jeshi aina ya Mi 17 ambayo moja yake CCM wameichukua kwa matumizi yao.
NATO+DAYS+2023+(137).jpg
IMG-20250901-WA0002.jpg


Updates;
Hadi Helocopter tulizonunua kwa ajili ya Jeshi letu kutoka Ufaransa nazo zinatumika kwenye kampeni za CCM. Mbaya zaidi zinapigwa hadi machata na stickers za CCM.

Kweli JWTZ limetusaliti Watanzania
Screenshot_20250905-222928_Facebook.jpg
 
Hahaha unafurahisha sana.
Sasa jeshi ni la ccm litatumiwa na nani kama siyo ccm?

Niliwaambia achaneni na vyama anzisheni majeshi ya ukombozi kama M23, Taliban, Hamas, Houthis.

Angalieni Syria imejikomboa kutoka mikono dhalimu ya Al Asaad, hawakufunga Novena wala hawa kusali, walipigania uhuru wao.

Nyie mnadanganywa na demokrasia wao ccm wana majeshi na yanawalinda na kulinda maslahi yao.

Amkeni.
 
Acha kua na overexpectation na majeshi yetu,ile ni sehemu ya ajira kama zilivyo ajira nyingine na ni watu kama watu wengine,ni vile tu huwaoni kwenye majukumu ya kila siku kama yalivyo majeshi mengine kama polisi,uhamiaji n.k.
Pole sana mleta mada.
 
Kwani Haujui kwamba Samia Suluhu Hassan Bado ni Rais wa JMT na ndiye Amiri Jeshi Mkuu?

Jeshi lazima limpe Ulinzi Hasa nyakati hizi ambazo Mh Rais yupo katikati ya watu wengi(Mass)

Mnalaumu vitu hata havina kichwa hata mguu!
Ishu sio kumpa ulinzi ishu zinaonekana zikiwa na kampeni
 
Taasisi tuliyoitegemea zaidi kuwa ya mwisho kama tegemeo kwa Watanzania inaoneka nayo imebebwa na maji ya Chama cha Mapinduzi.

Taasisi iliyotegemewa kwa weredi, umakini na kuwa bold dhidi ya siasa na wanasiasa sasa inaonekana imekuwa compromised.

Inasikitisha sana kuona helicopter za Jeshi letu aina ya Mi 17 zikitumika kwenye kampeni za Chama cha Mapinduzi.

Inasikitisha zaidi sasaivi vijana waliopo kwenye Makambi ya Jeshi wanatolewa kwenda kujaza watu kwenye mikutano ya CCM.

Jeshi linapofikia hapa ni dhahiri kuwa Watanzania hatuna tena Jeshi la Wananchi. Tuna kikundi cha Wanajeshi kinachotumika kwa maslahi ya CCM.

Tumekwisha
Chini ni picha za ndege Jeshi aina ya Mi 17 ambayo moja yake CCM wameichukua kwa matumizi yao.
View attachment 3461094View attachment 3461100
Jamani acheni uchochezi wa kijinga, nilikuwa nakodoa macho sehemu iliyoandikwa JWTZ kwenye helicopter, sijapaona. Ni ndege ya jeshi gani?
 
Back
Top Bottom