Nini kimemkumba Lawrence Masha? Nimeshangaa sana kukutana na hii video ikizunguka mtandaoni eti yupo kwa huyu anayejiita Pastor, Kiboko ya Wachawi sijui.
Naelewa kwenye maisha kuna kupanda na kushuka lakini inakuwaje mtu msomi kama Masha mwenye Shahada ya Uzamili ya Sheria (LL.M) kutoka Kituo cha Sheria cha Chuo Kikuu cha Georgetown na Shahada ya Kwanza ya Sheria (LL.B Hons) kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, anaishia kwenye masuala kama haya!
Je, anatumiwa na huyu anayejiita mchungaji au ni tangazo hili?
Masha alikuwa mtu mzito sana kwa kweli. Amewahi kuwa Mwenyekiti wa Lyson Law Group na Tanga Cement, Managing Partner Gabriel & Co na IMMMA , Waziri wa Mambo ya Ndani na Mbunge wa Nyamagana. Lakini pia alikuwa Mwenyekiti Mtendaji wa FastJet pamoja na nyadhifa nyingine nyingi alizokuwa nazo.
Pia soma;
1. Lawrence Masha: Kutoka Uwaziri hadi kukusanya takataka Dar
2. Lawrence Masha amiliki asilimia 68 ya hisa Kampuni ya Fastjet Tanzania
3. Lawrence Masha! Mpambanaji anayekaribia kupoteza pambano
4. Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Lawrence Masha akamatwa na Polisi
5. Logical conclusion ni kuwa Lawrence Masha siyo msafi
6. Lawrence Masha ajivua uanachama wa CHADEMA. Adai hawana nia ya kushika dola!
Masha, nadhani ni mmoja wa watu waliokuwa na 'bahati mbaya' sana na serikali ya awamu iliyopita. Mwingine jamaa anaitwa Gonzaga, yule 'mtoto wa mjini' kwa wanaomjua.
Gonzaga alipewa kesi ya kudukua mifumo ya TRA, akatupwa mahabusu na kesi yake ikawa haiendi. Sijui hadi sasa imefikia wapi, naye sijui yuko nje au mahabusu.
Hawa wawili walidaiwa 'kuichezea' ile kesi ya 'samaki wa pombe'. Kwamba waliwaonesha njia na kutoa msaada wa kisheria hadi jamaa wakashinda kesi na kulipwa fidia.
Hao watu wawili kwa nyakati tofauti walifuatwa na Pombe akiwa Waziri wakati huo, na kuombwa waiache hiyo kesi, kwani ni turufu yake akiwa katika wizara hiyo.
Wakati huo alikuwa Wizara hiyo kama 'adhabu' baada ya 'fujo' alizowafanyia viongozi wenzake akiwa Ujenzi. Hivyo, Uvuvi nako alitaka afanye 'maajabu' pia ili kufunga watu midomo.
Kwa hiyo, kwa Masha baada ya IMMA kupigwa bomu, ilikumbana na vita nyingi za kikodi hadi ikatetereka hasa. Na kutimuliwa kwa Fast Jet kulimaliza vingi kwake kiuchumi.
Kwa mtu kama Masha kupitia hayo, ni pigo kubwa kwake. Amepoteza vingi na mapato yake yameshuka sana, na nadhani hilo lilimletea shida ya kindoa pia na mkewe Stellag
Masha, naweza kusema yeye na Gonzaga (yule mtoto mjini, kwa mnaomfahamu) walikuwa na 'bahati mbaya' na serikali ya awamu iliyopita iliyohitimishwa na msiba.
Gonza alipewa kesi ya kudukua mifumo ya kodi na kuwa akiingiza hela 'ndefu' kwa kila dakika. Alikuwa ni mtu wa mwanzoni sana kudakwa na kutupwa mahabusu na kesi yake ikawa haiendi.
Hawa watu wawili, walikuwa wakidaiwa kuwahi 'kuchezea' kesi ya 'Samaki wa Pombe', hadi kufanya serikali ishindwe na kulipa fidia. Ni kesi iliyoibuliwa na Pombe akiwa Waziri kwenye Uvuvi.
Kwa wakati huo Pombe, kama alikuwa kwenye 'adhabu' kwenye Uvuvi, baada ya kutibuana sana na viongozi wenzie alipokuwa Waziri kwenye Ujenzi. Kwa sifa za Ujenzi, alitaka aje nazo Uvuvini.
So, kesi ya samaki Ilikuwa ndiyo turufu yake, kwani kupandisha nauli za vivuko na kuileta boti isiyoweza kutia nanga bandarini, haikuwa sifa nzuri, japo boti ilikuwa ya ruti za nyumbani kwa Rais.
Inaelezwa kuwa, aliwafuata kwa nyakati tofauti hao jamaa wawili kuwaomba waiache hiyo kesi ili 'atoboe' nayo impe sifa. Lakini, jamaa waliendelea kutoa msaada wa kesi na serikali ikaanguka.
Masha, IMMA yake mbali na kupigwa bomu la kutupa kwa mkono, lakini kulikuwa na vita nyingine za bwana kodi, kabla Fast Jet kutimuliwa nchini. Hapo Masha, akalazwa chali.
Baada ya uchumi kuyumba na siasa kumsahau, nadhani kwake tukio hili ni kama kiki yake ya kurejea vichwani mwa watu, hasa ukizingatia mwaka ujao tuko kwenye uchaguzi mkuu.
Na kwa hiki kilicho kwenye hii video, nadhani ni namna ya kumwonesha Mwenyekiti wa CCM kuwa asimsahau, naye yupo.
Ova