Nini kimemkuta Waziri wa zamani na Wakili Msomi, Lawrence Masha hadi kufika kwa “Kiboko ya Wachawi”?

Hii ya kuwataja wake za watu madhabahuni imekuwa fasheni, kuna mwingine alifannya kitu kama hiki Arusha siku si nyingi
 
Na wengi tunapitia hapa
 
Masha, naweza kusema yeye na Gonzaga (yule mtoto mjini, kwa mnaomfahamu) walikuwa na 'bahati mbaya' na serikali ya awamu iliyopita iliyohitimishwa na msiba.

Gonza alipewa kesi ya kudukua mifumo ya kodi na kuwa akiingiza hela 'ndefu' kwa kila dakika. Alikuwa ni mtu wa mwanzoni sana kudakwa na kutupwa mahabusu na kesi yake ikawa haiendi.

Hawa watu wawili, walikuwa wakidaiwa kuwahi 'kuchezea' kesi ya 'Samaki wa Pombe', hadi kufanya serikali ishindwe na kulipa fidia. Ni kesi iliyoibuliwa na Pombe akiwa Waziri kwenye Uvuvi.

Kwa wakati huo Pombe, kama alikuwa kwenye 'adhabu' kwenye Uvuvi, baada ya kutibuana sana na viongozi wenzie alipokuwa Waziri kwenye Ujenzi. Kwa sifa za Ujenzi, alitaka aje nazo Uvuvini.

So, kesi ya samaki Ilikuwa ndiyo turufu yake, kwani kupandisha nauli za vivuko na kuileta boti isiyoweza kutia nanga bandarini, haikuwa sifa nzuri, japo boti ilikuwa ya ruti za nyumbani kwa Rais.

Inaelezwa kuwa, aliwafuata kwa nyakati tofauti hao jamaa wawili kuwaomba waiache hiyo kesi ili 'atoboe' nayo impe sifa. Lakini, jamaa waliendelea kutoa msaada wa kesi na serikali ikaanguka.

Masha, IMMA yake mbali na kupigwa bomu la kutupa kwa mkono, lakini kulikuwa na vita nyingine za bwana kodi, kabla Fast Jet kutimuliwa nchini. Hapo Masha, akalazwa chali.

Baada ya uchumi kuyumba na siasa kumsahau, nadhani kwake tukio hili ni kama kiki yake ya kurejea vichwani mwa watu, hasa ukizingatia mwaka ujao tuko kwenye uchaguzi mkuu.

Na kwa hiki kilicho kwenye hii video, nadhani ni namna ya kumwonesha Mwenyekiti wa CCM kuwa asimsahau, naye yupo.

Ova
 
Tumpe pole tu kijana watu. Tumuombee arudi kwa Mwenyezi Mungu, ajiondowe huko kwa wapigaji, hao ndiyo wanammaliza kabisa sasa.
 
Kama kaenda kwa utashi wake na siyo kutafuta kiki za kisiasa basi kaingia chaka, hakuna nabii hapo....

Wife huwa anapenda kuweka chaneli ya vipindi vyake usiku, ukisikia maongezi anayofanya kwenye simu na watu wanaojifanya kumpigia, kwa akili ya kawaida utagundua mapema ni usanii na utapeli tu unaoendelea pale, wengi wanaompigia wanakuwa wamefiwa muda huo wanaompata hewani.

Igizo huwa linaanzia kwa nabii kiboko ya wachawi kutaja majina na tarehe za kuzaliwa za wahusika, kumtaja mchawi aliyemuua marehemu ambaye mara nyingi ni mmoja wa wafamilia hasa mama, kumtishia mchawi aseme ukweli au afe, na linaishia kwa kumfufua marehemu.......lakini ukisubiri kesho yake usikie habari mtaani kujua kama kuna mtu alikufa na kufufuliwa na kiboko wa wachawi hutasikia hata moja pamoja na marehemu kama wanne kufufuliwa usiku huo mmoja.

Hawa matapeli wanaojiita manabii na mitume wanapotosha sana watu hasa wanawake wasiotaka kuumiza akili zao kutafakari mambo.​
 
Natamani walokole wanijibu haya maswali:
1. kuna umuhimu gani wa nabii mfukuza wachawi kulindwa na bodigadi?
2. Hivi ukiwa mlokole ni lazima uwe maskini (angalia hali za waumini wake!)?
3. Hivi nabii hawezi kuwa kiboko ya umaskini? ukiwa muumini wake wewe ni mwendo wa utajirisho tu?

Halafu na ninyi wachawi mmekosa uzalendo na utaifa, Unahangaika kuroga Choka mbaya
si watafute kina GSM, MO, BAKHRESA, ROSTAM
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…