NetMaster
JF-Expert Member
- Sep 12, 2022
- 1,454
- 4,925
Afrika iliweza kushuhudia wiki chache zilizopita bunge la Uganda likipitisha muswada wa kutokomeza ushoga kimafia, Wengi tukaona Uganda awe mfano wa kuigwa na tukawapongeza sana kwamba ndio taifa la kuigwa katika suala la kulinda maadili yetu ya kiafrika.
Kilichobaki ilikuwa ni kumpasia pasi museveni amalizie kupitisha muswada huu uwe sheria, ilibaki tu saini ya Rais Museveni kufanya muswada huo uwe sheria, Kila mtu alijua Museveni ataipitisha fasta tu maana hata katika hotuba zake na vyombo vya kimataifa hamungunyi maneno wala kukwepesha, wala haogopagi chochote kusema hakuna watu wanaomkera kama wanaofanya mapenzi ya jinsia moja na anatamani wasiwepo kabisa kwa namna yoyote.
La haula!! Museveni kagoma kusaini muswada huo, kaomba upitiwe upya, Museveni tunaemjua huyu au !?
Wabunge walipedekeza muswada huu adhabu za vifungo vya gerezani na kifo kwa wale wanaobaka lakini Museveni kwa sasa kapendekeza kuwe na rehab, rehab ni kama zile sober house za wenye uraibu.
Hakika ni kitu cha kushangaza maana ikumbukwe Raisi huyu alikuwa ni kichwa cha treni kuwa mstari wa mbele kutamani kabisa kuutokomeza ushoga hata kwa mbinu za kimafia , nini kimetokea mpaka kawa hivi ??
Conclusion: Hivi vitu viwe kimya kimya tu kama hapa bongo unawekwa ndani miaka 30 kimya kimya, kwa sasa kupiga kelele kwa wanaotoa misaada ni kutafuta attention unnecessary, ni mwendo wa kimya kimya tu