Nini kimemsibu Mulamula?

Nini kimemsibu Mulamula?

Ilikua swala muda tu why mulamula...

Mosi Balozi liberata ni mtendaji mzuri ila sio mwanasiasa mzuri kuna issue nyingi za kisiasa zinahusu diplomasia ambazo alitakiwa azitolee ufafanuzi kama mwanasiasa ila alishindwa mfano, issue ya Royal tour baada ya kupokelewa tofauti na watanzania wengi wakilitazama kama jambo la kufuja kodi, balozi waziri hakuwahi kulielezea swala hilo kwa namna ya kutuliza mambo akiwa kama mwanasiasa.Mfano mwingine Rais kunyweshana juice na Rais mwenzie wa kiume hili nalo lilipita hivi hivi wakati tulitarajia wajuvi wa maswala haya kutoka chuo cha diplomasia ama wizara ya mambo ya nje, wajiachie lakini ndo kama hivyo ikawa bora liende, ishu ya kupanda basi msibani ambayo ilichukuliwa kwa uzito mdogo wakati kiuhalisia ilishusha hadhi sana ya mpendwa wetu Rais watu anawaongoza wali mdown look kwa kweli, kwenye wizara ya foreign serious hili swala lilitakiwa kupewa clarification ya uzito sana why this and not that, ila ndo kama hivyo wizara ya bibie iliona sawa tu.

Swala la pili ni umri, mulamula ana miaka 66 sasa, uwezo wake umejidhihirisha kupungua kila inapoitwa leo amekua akisahau sana mambo na ameshindwa kuzungumza vitu kwa ufasaha hivyo kuishia kucheka cheka tu.

3.Kushindwa kuwajibika kama sehemu ya maamuzi, collective guilty huyu mama aliwahi kujitoa kwenye maamuzi fulani ya serikali kuhusu usalama wa nchi ya Msumbiji hii kitaalamu alipuyanga sana hapa hata mzee mkuchika alimshangaa huyu bibie, maamuzi ya serikali hata kama yametolewa na kichwa kimoja hua ni maamuzi ya wote nilitegemea mama amuache soon baada ya kutoka Msumbiji ila sijui kwa nn amenkawiza kimtindo.


4.Wanawake wana mambo mengi sana ikiwemo wivu na husuda kuna tuhuma mwanamama alishindwa kuratibu picha ya namba moja wa kwetu na familia namba moja ya US, badala yake akatokea yeye kwenye picha ile adhimu, unaambiwa kule Zanzibar ilitembea misonyo na kujiapiza sio kwa nchi hii(😂😂😂hapa mnisamehe nimeandika kama Mange sababu hii ni udaku japo ile picha ya waziri na Biden plus Flotus kweli ipo.😂😂)


5. Tano na mwisho hili sasa ndo la msingi zaidi japo tuna haki ya kumtaka hiRais akiteua atoe sababu na akitumbua pia atoe sababu. However Kwa vile hatujawahi kudai rais atoe sababu za kumteua fulani, siku akitumbua pia hatuna uhalali wa kudai kupewa sababu.

Imperium locuta; causa finita est

Authority has spoken, the matter is settled.
 
Skul bas na Gilasi vimemponza Mulamula
Hiyo school bus unayosema, mbona marais wengine, akina Ruto na marais wengine nao walipanda.

Mbona hatujasikia kuwa huko Kenya nako, kumewaka moto, kutokana na issue hiyo?

Lazima kutakuwa na kitu, nje ya hivi ambacho kimesababisha dada yetu wa "ishomile" atumbuliwe
 
Samia - wateule wangu lazima upate ruhusa



  • Viapo ni kulinda kutetea na kuiheshimu katiba ya jamhuri ya muungano wenye pande mbili
  • Kujua mamlaka yana ukomo wake, kwenda juu au chini lazima uombe ruhusa toka ngazi ya juu
  • Siri za baraza la mawaziri zizingatiwe, tukiamua hakuna tena kwenda kinyume kuwa una maoni yako
 
Umeongea na kuandika upotoshaji wa kimakusudi kwa kuonyesha kutokuwa na uelewa wa kutosha, Hoja ilizoweka hapo juu Ni za uongo na kinafiki Sana,

Hoja ya usafiri alioutumia mh Rais wetu mpendwa mama Samia suluhu Hassani pamoja na viongozi wengine wengi tu waliokwenda kwenye mazishi ya Malkia wa uingereza yaliratibiwa na kusimamiwa na nchi mwenyeji katika kurahisisha usafiri na suala Zima la ulinzi na usalama kwa Hawa viongozi wetu, kwa kuwa Kama viongozi wetu wangetumia mfumo wa misafara kwa kilo mmoja Basi ingetumia muda mrefu Sana kumalizika wote na hata suala la ulinzi lingekuwa gumu Sana hasa kwa kuzingatia kuwa Ni Kama viongozi wote wa serikali na nchi walikuwa pale, hivyo hoja yako uliyotoa hapo juu inakosa mashiko

Hoja ya pili ambayo mh Rais wetu mpendwa alipokuwa kule msumbiji Napo Naoona umeamua kupotosha na kuandika uongo wako hapa kwa kuficha ajenda zako za kinafiki, kwani suala Hilo nilishalieleza Sana humu kwa wapotoshaji Kama wewe, kwamba ifahamike kuwa mh Rais wetu mpendwa hakutumia glas aliyotumia mwenyeji wake, Bali glasi ilibadilishwa na akapewa nyingine na msaidizi wake hatua chache alipotoka alipokuwa Amesimama mwenyeji wake, hata namna mh Rais wetu mpendwa alivyoipokea ilionyeshwa vyema japo kwa vipofu Kama wewe na mliojaa mihemuko na kukosa umakini unaweza usiona chochote kile na ukaja kupotosha hapa Kama ulivyofanya sasa

Mwisho ifahamike kuwa suala la uteuzi na utenguzi wa viongozi wa kuteuliwa na mh Rais wa nchi linabaki mikononi mwa mh Rais pekee , yeye ndiye anayeweza kufahamu kwa wakati gani na mazingira yapi mtu fulani ataweza kufaa katika nafasi fulani na kumudu majukumu yake kuendana na matarajio yake Rais, kwani Leo ndio Mara ya kwanza kufanya hivyo? Kwani mawaziri wangapi walikuwa katika wizara hiyo na wakapumzishwa na kupisha wengine? Kwani Leo ndio Mara ya kwanza kufanywa utenguzi na uteuzi mpya?

Tumuache mh Rais wetu mpendwa mama Samia suluhu Hassani afanye kazi na watu au viongozi anaoona wanastahili kumsaidia kwa wakati huu katika kuwatumikia watanzania

Kazi iendeleee Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka

Lucas Mwashambwa, kijana mzalendo na mpenda nchi yangu
Walamba Asali washavamia uzi
 
Sababu ulizozitoa zote ni sahihi na ongezea na hii, kwa nini alialikwa na Biden na kuandaliwa chakula cha dhifa ya Kitaifa white House juzi Kati yeye kama yeye badala ya VP aliyekuwepo huko au Rais?

Najaribu kuwaza tuu.

Hahaha wivu unawasumbua hahahah[emoji23][emoji23][emoji23][emoji19][emoji23]
 
Mulamula ametumbuliwa. Maswali ni Mengi lkn yapo mawili makubwa yaliyoaibisha nchi yetu kimataifa, yamkini yamesabishwa na makosa ya balozi zetu (zilikuwa chini ya Mulamula) kushindwa kuratibu mambo vizuri?

1. Je, ni ile kadhia ya mama kupandishwa school bus kwenye mazishi ya malkia?

2. Je, ni ile clip iliyoaibisha nchi kwa kumuonesha mama akigonga glasi na Rais Nyusi kisha akamnywesha Rais Nyusi na kunywa mwenyewe kwa glasi ileile?

Au tuhuma hizi zina ukweli?

View attachment 2375381
View attachment 2375383

Tuna haki ya kuuliza na kujua maana wanakula kodi na tozo zetu.
Kwa level yake hivyo ni vijisenti tu!!
 
Imperium locuta; causa finita est

Authority has spoken, the matter is settled.

Authority ya dhuluma? Hiyo meli Mungu ataizamisha ipo siku tu, na siajabu muda umeshafika!
 
Sidhani ni issue ya school bus kwasababu marais wote walipandishwa kwenye bus ispokuwa tu kiranja wa dunia alitumia usafiri wake.
... waingereza walitumia akili sana! Sipachi picha kiranja wa dunia angechanganywa kwenye bus; hayo maombi ya misaada na shida ambazo angeliliwa sasa; ingekuwa balaa. Angefika msibani kachoka sana mzee wa watu!
 
Inahusika na ujumbe wenu kwenda New York kwenye general assembly na kukaa kwenye hoteli ya kifahari wakati huku mnang'ang'ana na tozo. Kuna clip ipo sosho midia!!!
... ndio ile habari ililetwa humu baadhi ya viongozi wa Afrika warekodiwa wakitumbua maisha aghali Marekani?
 
JPM alimtumbua kisa alimshinikiza aende kwenye kikao kimojawapo huko ugaaubuni JPM akamwambia nitaenda, muda ukakaribia Mulala akamkumbusha tena JPM kuwa tunaomba hakikisho lako Mhe. Rais kama unaenda au huendi, JPM akamjibu Mlamula kuwa nitakwambis..

Mlala kama mkuu wa protocal ikabidi amshirikishe marehe Che Nkapa, ndo Nkapa akampigia JPM kumuuliza 'Hivi we unajua una kikao nje na kwa we bado Rais mpya inabidi uende lau ujitambulishe huko kwa wenye dunia yao?'

JPM akamjibu Nkapa kwa upole kuwa nitaenda mzee wangu..

Kwa hasira JPM akamgeukia Mlamla..'we umenishtaki kwa Mkapa ili iweje? sasa SIENDI we nend wewe na huyo Mkapa wako na sitaki kufanyakazi na wewe tena na nisikuone hapo Ifisini ahahaha

Nakumbuka usiku ule Mulamula akampigia mkapa yaliyojili ..Mkapa akaogopa akasema we achana naye Mwehu huyo..ahahaha
😀 😀 😀 😀 😀mwana akaona anataka kupelekeshwaa
 
Nimesoma sehemu amenunua jumba marekani wanadai hiyo ndio sababu
Wenda ni kweli ila huyo mama amefanya kazi muda mrefu nje ya nchi kwenye masuala ya diplomasia hivyo mkwanja atakuwa nao. Bongo ukifanikiwa uswahili unakuwa mwingi hoja hapo wangeibua ufisadi alioufanya ningeelewa ila kuchukia mafanikio ya mtu ni roho mbaya tu mawazo ya kimasikini.
 
Wenda ni kweli ila huyo mama amefanya kazi muda mrefu nje ya nchi kwenye masuala ya diplomasia hivyo mkwanja atakuwa nao. Bongo ukifanikiwa uswahili unakuwa mwingi hoja hapo wangeibua ufisadi alioufanya ningeelewa ila kuchukia mafanikio ya mtu ni roho mbaya tu mawazo ya kimasikini.
Huku utajiri ni dhambi
 
Back
Top Bottom