Nini kimepelekea Kadinali Pengo kuondolewa kwenye tovuti ya Jimbo Kuu la D'Salaam?

Nini kimepelekea Kadinali Pengo kuondolewa kwenye tovuti ya Jimbo Kuu la D'Salaam?

Hata mimi nimeiona sasa. Sijui kulikoni.
Wahusika watatufafanulia.Ila binafsi namkubali ARCHBISHOP JUDE THADEUS RUWAICHI kwa utume na uinjilishaji wake. Tangu nimwone jimboni Mwanza mwaka 2012 akitoa kipaimara katika parokia yetu kwa jinsi alivyowauliza walengwa maswali nilianza kumfuatilia mpaka leo.Jaribu kuingia website ya TEC fuatilia katika misa mbalimbali mahubiri yake. Fuatilia anavyovaa ( He embraces simplicity ).
Ruwaichi ni mzuri Sana kwenye utume na uinjilishaji sijawahi kuchoka kumsikiliza akihubiri
 
Nikweli ulichoandika Pengo anatoka madarakani huo niutaratibu unafanyika kwaajili ya kumuidhinisha Ruwaichi kushika madaraka ya juu ktk Kanisa Katoliki Tanzania, wanaanza kumwondoa kwenye maamuzi ya kikanisa taratibu mpaka muda walioupanga ukifika basi atapumzika kazi nyingi za kikanisa na atabiakia nancheo cha Kadinali mstaafu.

Sent using Jamii Forums mobile app
hapana,sio kushika madaraka ya juu ktka kanisa katoloki Tz,,kwa kanisa katoliki hakuna askofu wa jimbo aliyejuu ya mwingine,akofu yuda anakua askofu mkuu wa jimbo kuu Dar na sio Tanzania.
wapo maaskofu wakuu wengi tu Tz kadri ya majimbo yao.
 
aisee huyo Ruwaichi napenda sana namna yake ya kuzungumza. Anajiamini na anasema ukweli tupu..... IBADA NYINGI SANA ZA KUSIMIKWA MAASKOFU, MAZISHI YA MAASKOFU, NA IBADA ZA KIASKOFU JAMAA HUWA ANAPEWA NAFASI YA KUHUBIRI. Nilimuna Arusha wakati Lebulu anastaafu.
 
Huyo angalia
 
Attachments

  • 1553584650689.png
    1553584650689.png
    167.5 KB · Views: 26
SOURCE: Website ya Jimbo Kuu la D'Salaam

Nimeshtushwa kuondoloewa kwa Kardinali Polycarp Pengo kwenye website ya Jimbo Kuu la D'Salaam.

Ukiisoma inaonyesha Jude Thadaeus Ruwa'Ichi ndiye Askofu Mkuu wa Jimbo hilo na Eusebius Nzigilwa ni Askofu Msaidizi.

Jamani nikumbusheni. Je, inawezekana Kardinali Pengo ameshaondolewa jimboni ni mimi tu ndiyo sina taarifa?

Je, kuna mjadala wowote humu JF kuhusu kuondolewa Pengo labda umenipita?

Wana JF naomba ufafanuzi maana mantiki sijaielewa.

Website hii hapa:

Archdiocese of Dar-es-Salaam – Roman Catholic
Umeangalia picha ya pili toka kushoto kona ya kushoto kwako? Ni nani huyo? kama kweli upo serious!
 
aisee huyo Ruwaichi napenda sana namna yake ya kuzungumza. Anajiamini na anasema ukweli tupu..... IBADA NYINGI SANA ZA KUSIMIKWA MAASKOFU, MAZISHI YA MAASKOFU, NA IBADA ZA KIASKOFU JAMAA HUWA ANAPEWA NAFASI YA KUHUBIRI. Nilimuna Arusha wakati Lebulu anastaafu.
Archbishop Jude Thaddeus Ruwaichi yuko vizuri sana hata mimi namkubali sana huyu mkapuchini. Yuko simple but tough. Hupendelea kuvaa kanzu lake lile la kijivu la kikapuchini kuliko mavazi ya kiaskofu. Hawatofautiani simplicity na Cardinal Sean Patrick O'Malley OFMcap wa Boston
 
Mimi siyo mkatoliki lakini huyo askofu namsikilizaga sana... ni mzungumzaji mzuri, hachoshi ukimsikiliza. Mwingine ni yule wa dodoma sijui anaitwa nani ila hao jamaa ni wazuri sana kwenye kuzungumza.
 
Back
Top Bottom