Viongozi wa upinzani wanalalamika kuwa wanapambana sana kutupigania Watanzania ila sisi hatuko tayari.
Kwamba kijana ni Bora aende akaangalie mpira dakika 90 Tena umbali mrefu kuliko kutumia dakika 2 kujiandikisha mtaani kwake.
Mwanzoni ilikua ni kwamba labda chama tawala kimekosa mvuto wa kushawishi watu kuandikishwa kwenye daftari na labda kwenye kupiga kura BUT inapotokea hata vyama pinzani vina struggle to pull out the crowd kujiandikisha TU basi kunae shida mahala.
SASA ndugu zangu hususani nyie wa vyama vya upinzani Hapa kuna tafiti tano za kitaaluma zinazojadili kwa nini vyama vya upinzani vinakosa mvuto kwa vijana kiasi cha kushindwa shawishi hata zoezi la uandikishaji wapiga kura katika daftari.
Na kwamba kabla ya kulaumu dola, tafiti hizi zitawapa njia na majibu kwanini mna struggle.
1. Barrett, M. & Pachi, D. (2019). Multilevel factors influencing youth political engagement.
Tafiti hii inaeleza kuwa vikwazo vya kimuundo na kisiasa vinavyotokana na mazingira ya kisiasa vinawakatisha tamaa vijana kushiriki siasa rasmi, yakiwemo mazingira ndani ya vyama vya upinzani. Wanaona siasa kama michongo fulani wa wao kutumika tu ili kunufaisha "wahuni" fulani kwa hiyo wanaona CCM na CHADEMA wote ni walewale tu yaani. soma (uk. 231).
2. Fahmy, Eldin (2003). A Disconnected Generation? Encouraging Young People’s Political Participation in the UK. Youth and Policy, 81, uk. 1-20.
Utafiti huu unahusisha kutoshiriki kwa vijana katika siasa na vikwazo vya kijamii na kiuchumi, pamoja na kutokuwa na imani na taasisi za kisiasa. Yaani kijana hawezi kuwa hajala afu ukampangishe foleni kisa tu ni kamanda aisee, hata akienda amini amefata ID ya kukopea Pesa X. Never kwa sababu anampenda Bonifasi.
3. Henn, M. & Foard, N. (2014). Youth political engagement and disengagement in Britain.
Huyu mtafiti yeye anaonyesha kuwa kizazi kipya kimekata tamaa na miundo ya kisiasa ya jadi, yakiwemo vyama vya upinzani, kutokana na mtazamo kuwa havitekelezi kwa ufanisi masuala yao na kimefumbatanisha siasa na uongo uongo na hata easiest way kusema wewe ni muongo watasema tu "oyaa acha siasa..." (uk. 112).
4. Grasso, M. et al. (2018). Youth political development and political socialization. Utafiti huu unasisitiza jinsi mazingira ya kijamii na kisiasa yanavyoumba ushiriki wa kisiasa kwa vijana, ikionyesha kuwa vyama vya upinzani mara nyingi hushindwa kuendana na masuala muhimu kwa vijana, jambo linalopunguza mvuto wao. Yaani mna deal na vijana kwenye matukio yanayowa favor tu kisiasa but som core issue aaaah (uk. 235).
5. Andolina, M. et al. (2003). Influences on youth civic engagement.
Utafiti huu unazingatia ushawishi wa familia, shule, na marafiki katika kutengeneza mitazamo ya kisiasa kwa vijana na kupendekeza kuwa kutoshiriki kwa vijana katika vyama vya upinzani kunatokana na ukosefu wa maadili ya kisiasa kutoka kizazi kimoja hadi kingine.(uk. 319).
Ukisoma vema utagundua mambo kadhaa moja wapo ni kwamba vijana wengine wanaona wanasiasa wote mna akili zinazofanana (which is partially true) na kwamba nyie endeleeni na issue zenu na na wao na issue zao na ikifaa kabisa bora zimwi likujualo kuliko zimwi jipya.
Mnataka ku change a status quo ila maneno na matendo yenu vijana wanaona bora wabaki na walichokizoea.
Nlikutumia case study mfano ni Boniface Jacob alikua Meya Ubungo for almost 10 years, leo Ubungo kuna shida ya maji afu bila kutumia hata akili lawama anampa mwanasiasa aliyepo sasa wakati alikuwa na almost 10 good years Ubungo kama Meya, Mkuu wa Baraza la Madiwani ambae kimajukumu yeye ndio mpitisha bajeti kabisa ya Manispaa ili ampe MED atekeleze ila leo anaweza ruka hata mita 10000 kisiasa kwamba huhusiki na shida za maji ndani ya Ubungo/Kino.
Haya mambo na mengine ndo vijana wanaona ebana eeeh endeleeni navyo. Msilaumu, mlipanda hii mbegu nyinyi wapinzani.