LGE2024 Nini kimetokea kiasi kwamba Wananchi hawataki kujiandikisha hadi wanafatwa majumbani na wanatoa majibu ya dharau kwa wahamasishaji?

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024
Baada ya siku zakujiandikisha vituoni kukamilika nashauri serikali iongeze walau siku3 za waandikishaji kuwafata watu kwenye makazi/kazi zao kama ilivyokuwa sensa.Vinginevyo Hali ni mbaya
Wazir Mchengerwa Mwenye kifua kwenye mambo ya uchaguzi kashaongeza
 
Wanafatwa majumbani na wagombea "kula", ndiyo, "kula", siyo kura.

Ulitaka wasifatwe majumbani? Si wanapewa somo la uraia?
Halafu mnawalaumu waarabu kwanini hawawasaidii wapalestina. Hicho unachofanya ndicho waarabu wanafanya
 
Shida ipo. Wananchi wako bize na shughuli zao za kujitafutia mlo.
 
Halafu mnawalaumu waarabu kwanini hawawasaidii wapalestina. Hicho unachofanya ndicho waarabu wanafanya
Hahaha.....hakuna anayetaka kujihangaisha kwa sababu ya mtu mwengine
 
H
Hizi sababu nyingi ulizotaja ziko Tanzania tu? Nenda Kenya uone vijana wao au nenda USA uone vijana wao walivyo active linapokuja swala la uchaguzi wa viongozi wa Nchi.

Sema tz ni kama alivyosema Rais Moi
 
Wapinzani wantupigania au wanajipigania? Mtu unampigia kura awe mbunge au diwani.anaenda bungeni anakula Bata miaka mitano na kiinua mgongo Cha milioni 250 .wewe kabwela unaendelea kula mihovo na maharage .😂😂😂😂😂😂.huyo uliyemchagua anakuja kukukamua Kodi kama ng'ombe wa kisasa.Angalia wakina Mdee and COVID 19.wanakula Bata wewe unaendelea kupiga makalele eti hawatakiwi bungeni😂😂😂😂. mwenye nacho huongezewa bana.unachagua kiongozi ambaye hana uwezo wa kujenga hoja Ili iwe nini kwa mfano ? Hivi mtu ambaye hakuenda shule au ameishia la sabaana uwezo wa kuchaugua kiongozi wa kumletea maendeleo kweli?akipewa debe la mahindi anaona amepewa dili 😂 😂 😂
 
H

Hizi sababu nyingi ulizotaja ziko Tanzania tu? Nenda Kenya uone vijana wao au nenda USA uone vijana wao walivyo active linapokuja swala la uchaguzi wa viongozi wa Nchi.

Sema tz ni kama alivyosema Rais Moi
Wengine wanasingizia eti mwenge ndio unasababisha Vijana wa bongo wanakuwa watulivu. Shubaamit nyi mlitaka walete vurugu kama wale wahuni wa kenya
 
Wapinzani wengi wa bongo ni hawajielewi wao wanatumika viongozi wanafaidi matunda,pesa za ruzuku na marupurupu kibao wanayohongwa na serikali.

Upinzani ni biashara ila watu watakuja kushtuka baadae sana.

Viongozi ndio wanafaidi na chawa wao
 
WaTanganyika wa leo wamejanjaruka! Walitaka Tume huru ya uchaguzi... Ikaletwa kituko.
 
Ukweli ni kwamba wananchi wamechoshwa na wababaishaji waliopewa dhamana na chama changu CCM Kwa siku za karibuni!

Ccm hii ya machawa inayogawa baiskeli na piki piki ni ccm mbovu sana haijawahi kutokea!!

Mwenyekiti anatoa rushwa ya wazi kabisa bila soni kabla ya uchaguzi no dhahiri wamekiharibu chama na Sasa Tiss inapaswa kuandaa chama Cha kukipa madaraka 2025 na sio kwa huu utopolo!!
 
Chama Gani sasa kishike madaraka 2025? Cha upinzani? Hapana aisee.sijaona mimi.watu wanataka kuvunja misingi ya nchi ndo uwape nchi? Hapana.Angalia kule Ukraine kwa kumchagua msanii zelensky nchi imeharibika kabisa kwa sababu kavunja misingi ya nchi.leo wapinzani hawataki mwenge wa uhuru,hawataki muungano,hawataki umoja wa kitaifa Bali majimbo,nk .hao utawapaje nchi kwa mfano
 
Baada ya uchaguzi "Kiongozi" na "uongozi" unakuwa ni Mali binafsi ya "muwekezaji" na sio "wawekezaji"
 
Wizi wa kura na matokea ya uchaguzi kupindishwa
Kimsingi mimi sioni umuhimu wa kupga kura mpaka tutakapokuwa na Tume Huru ya uchaguzi

Yaani unaenda kupga kura kushindana na mgombea wa ccm ambapo uchaguzi upo chini ya Wizara ya Tamisemi,

Ni sawa na kucheza mechi na timu ambayo refa ni nahodha wa timu unqyoshndana nayo, akishirikiana na linesman na kamisaa wa mechi halaf utegemee kushinda
 
Wako busy mechi ya Simba na yanga jumamosi ijayo baada ya hapo mabishano yake hadi wiki nyingine.

Inawezekana hii ratiba za mechi ya Simba na yanga ilipangwa ili kuwatoa watu kwenye reli; watakapostuka muda wa kujiandikisha umepita.

Wakitoka hapo wanakuja kulialia kwenye key boards. Wameibiwa kura..

Wanasiasa wajanja wanaendelea kuitafuna Tanganyika wajinga wanaendelea kulala usingizi wa pono.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…