Nini kimetokea mpaka kufa kwa uzalishaji wa Ngano hecta 350,000 kule Bassotu Manyara?

Mkuu bado unakaa huko? Niliishi bonga kipindi Fulani hivi
 
Kwa nchi kama Tanzania, kusema tuna uhaba wa ngano au hata pengine mafuta ni aibu. Tuna ardhi bora sana ya kilimo. Tatizo hatujawekeza sana huko. Kuna kipindi kilimo kilipewa kipaumbele, kabla kilimo hakijaimarika tunavuka kwenye viwanda.

Nafikri watunga Sera wetu wanatakiwa kua makini na kutambua nini kinatakiwa kupewa kipaumbele, kwa wakati gani na kwa nini.

Kwa hesabu za haraka haraka, viwanda huja baada ya kilimo kuimarika.
 
Kuna wazungu wamechukua hilo shamba la basuto wanafukua barabara zote za shamba ili kuanza kilimo cha ngano,bila shaka mwaka kesho wataanza kilimo....shamba limeharibika sana mpka waweke miundombinu sawa
80% hapa tz inatoka Ukraine, Sasa hii vita wazungu wanaona mbali wanajua watapiga hela acha sisi tuendelee kufungua nchi.

Sent from my TECNO BB2 using JamiiForums mobile app
 
Ndo maana upigaji KILA mwaka na mwakani watazipiga zaidi,Ningepata namna ya kukwepa kodi ningefurahi sana.
Ripot ya CAG ni SAwa na ngonjera zisomwazo KILA mwaka kuwaumiza wananchi.
Hakuna mtu amewahi fungwa eti kapiga.Wanafungwa vibaka wa kuiba kuku sababu hawana pesa za kuhonga,jela ni kwa ajili ya watu masikini tu sababu hawana pesa ya kununua UHURU wao.
 
Ukinunua ndege utapata kiki zaidi kuliko kuinua kilimo, mwanasiasa anaangalia kiki kwa maumivu ya kodi zetu
 
Halina mchango wa kura wakati wa uchaguzi mkuu, kipaumbele chetu ni kuchukua madaraka na hilo shamba lingekuwa na wapiga kura ungeziona nguo za kijani hapo mwaka mzima zikipishana.
 
Mkuu awali ya yote pongezi kwa uzi huu
Si basutu pekee kule west Kilimanjaro kuna ngano pia inalimwa na serekali imekaa kimya
Swala la PSRC ile ya Nkapa kuhusu ubinafsishaji wa mali za uma ndio tatizo na sera zetu za ubabaishaj
 
Mulbadwa vs nafco
 
Huo mfano wa Mbowe na bavicha ndo matatizo ya waafrika hayo.
Watu wanaongelea uchumi wewe unatuletea mambo ya mabakuli.

Sent from my TECNO BB2 using JamiiForums mobile app
 
Ninakumbuka wa Canada walitoa mchango mkubwa sana katika kukiendesha kilimo hiki. Enzi zile kulikua na mabasi ya Mtei kutoka Arusha mpaka Katesh. Katesh ulikua ni mji kabisa watu walikwenda kula starehe na kupata mahitaji.
Ni kweli. Wadada wazuri wa nchi hii walidhuru eneo hilo na kutoa burudani. Nadhani hata wewe wakati ukiwa mbichiiii ulikuja huku.

[emoji38][emoji38][emoji3][emoji3]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Njowepo umeleta mada nzuri sana, Jamii Forums tunahitaji mada kama hizi ambazo mjadala wake unaweza kuleta tija katika kutatua changamoto zilizopo na kuleta impact katika uchumi wa nchi yetu. Ni seme tu huu ni mmoja ya miradi ambayo kama nchi ni wakati muafaka sasa Waziri wa Kilimo na team yake waangalie namna ya kufufua miradi hii mikubwa ya kilimo ya kimkakati kwa njia ya PPP (Public-Private Partnership) kwa mazao ya Ngano, Alizeti, Mpunga n.k. Ukiacha maeneo haya ya Hanang, pia kuna haja ya kufufua mashamba makubwa ya Ngombe wa Maziwa kule West Kilimanjaro, Pia Ngano inaweza kulimwa maeneo hayo, pamoja na Mufindi, Njombe n.k
 
Unaweza kutoa chozi ukisoma wadau humu wanavyochambua mambo.

Kuna pahala sisi huku Africa nafikiri hatuko sawa licha ya kutaliwa.

Ni kwa kiasi gani Serikali inakimbilia kujenga Miundombinu ya Kisasa mijini kwa gharama kubwa ikiwa kuna sehemu kama Kigoma , Ulanga-Mahenge na kote ambako watu wanazalisha mazao mengi lakini kutokana na kutofikika kwa urahisi , watu wamekata tamaa wameamua kulisha tu matumbo yao.

Vijana hawaogopi kutumia fursa ,tatizo kwenye Kilimo kwa hapa kwetu kumesahaulika na sidhani kama kuna Mwanasiasa ana muda na Kilimo.Ni ujuha wa hali ya juu Nchi kamaa hii kukosa mafuta ya kupikia..huo ni uchawi wa mchana kweupe sana.

Nenda West Kilimanjaro kuna vijana wanalima Karoti ,Nyanya na viazi Ulaya lakini katazame Barabara ya West to Bomang'ombe ni lami lakini ni uozo ule..Barabara nyembamba kama uzi.Sehemu kama hizo na zingine ambazo ndio kabisa hazina hata nukta ya lami zilipaswa kusambazwa Barabara na za kiwango cha lami na Reli pia ili kutufanya tuhame huko mijini tujikite na Kilimo.

Ukitaka kujua sisi tunashida angalia Mkoloni alipeleka Reli kila pahala pailipokuwa na mazao na uzalishaji maligahfi. Lakini njoo utazame akili zetu sis wenye Uhuru.

NSSF ,PSSF wanajenga majengo kiwizi wizi kwa fedha zetu za michango wanaacha kwenda kuwekeza kwa Vijana..majengo marefu na hakuna watu wanakaa humo.

Wanajijengea njia zao Baharini wapite wakati wa jioni wakiwa wamechoka,thamani ya hizo barabara ni umejenga Barabara za kutosha kuunganisha miji yenye uzalishaji bila ubabaishaji.

Vijana tuamke tujikite huko taratibu ..japo kuna ugumu.Serikali haiwezi komboa mtu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…