samurai
JF-Expert Member
- Oct 16, 2010
- 11,495
- 24,223
Utamaduni wa Wazungu ni kufanya kazi, ubepari umelenga kuhakikisha kila mtu anafanya kazi. Baada ya WWII Mfalme wa Holland alifungua kiwanda cha kutengeneza vitenge ili vijana wapate kazi.
Soko la vitenge limelengwa Africa, usishangae kufa kwa viwanda vya Mwatex na Sungura Tex, fitina ya soko la vitenge ni kubwa na jamaa wanafanya uchunguzi na propaganda nyingi.
Tungekuwa imara sisi Tanzania tungengeneza vitenge kwa East na South Afrika kutokana na pamba tunayolima.
Hizo tools tatu tulizoongea hapo juu ndio chanzo cha yote hayo kutotokea Africa..
Elimu iko limited na bepari ili isimkomboe Mwafrica maana wao pia wanafahamu elimu inaweza kuwa prime mover na push ya vitu vingi.
Technolojia, ukilimit elimu na technolojia pia haiwezi kukua, hata wale wenye vipaji nje ya elimu wako limited na mifumo ambayo iko controlled na mabepari wa dunia..
Utamaduni, kupitia media ambazo wao ndio controller wanahakikisha tamaduni hazikui zaidi ya zao za magharibi kukua na kutumeza huku...hili ni sambamba na entartaiment kuhakikisha wote tunacopy kwao kwa wao kubland vya kwao na kupuuza vyetu.. Lugha kuu ya dunia kiingereza na wote lazima tusome tuongee kienglish na elimu zote lazima zitumie hiyo lugha....na mkakati ni kutokomeza hata hizi lugha za makabila kwa watu kuoana huku na kule na automatically kuziua lugha na kubaki na kiswahili ambacho kitamezwa na kienglish..