Nini kimetokea mpaka kufa kwa uzalishaji wa Ngano hecta 350,000 kule Bassotu Manyara?

Nini kimetokea mpaka kufa kwa uzalishaji wa Ngano hecta 350,000 kule Bassotu Manyara?

Hivi ni sera ipi nzuri ili kulifikisha taifa katika maendeleo makubwa ya kiuchumi na kijamii.?

#MaendeleoHayanaChama
Hakuna sera tofauti na Ubepari pure au Ubepari wa kijamii kama vile vyama vya ushirika nk..

Na sera ya Ubepari usiefanya Kazi lazima ufe hakuna kulia msaada wa serikali 🤣🤣..

Mwisho kwa Tzn hii pia tunahitaji msaada wa Katiba nzuri Ili kuwajibishana na kufungiana speed governor..

Hai make sense Waziri anakuja kushughukikia eti mzozo wa zahanati au Rais anaambiwa hatuna vyoo vya stand,this is stupid inamaana taasisi za chini zimekufa.
 
Hii Nchi kama tumeshindwa tuu kupanga miji au makazi yetu ndio tutaweza hayo masuala yanayohitaji akili kubwa?

Huwezi sikia kiongozi akisema labda Kwa sasa tuna watu maskini kadhaa na nataka by certain time interval niwe nimewapunguza by this much, huwezi kuwasikia hao..

Kauli ya mwisho niliwahi kuisikia kwa Kikwete akisema amekusudia kupunguza umaskini wa kipato kwa watu without measurable timeframe and figures yaani inakuwa ni kauli ya jumla jumla tuu.
 
Viwanda vilivyokufa baada ya Tanganyika kupata uhuru

1. Kiwanda cha matairi general tyre cha Arusha
2. Kiwanda cha viberiti Moshi/kilimanjaro
3. Kiwanda cha tambi za majiko na vibatari dar es salaam
4. Viwanda vya pamba mwanza,singida na shinyanga

Na vingine vingi sana

Katika haya wafuatao ni wakulaumiwa vikali

1. Mwinyi
2. Mkapa
3. Msoga
Kiwanda cha UHURU ubungo
 
Wewe kwenu wapi Dar.

Unaijuwa Unga Limited Arusha, au unaisikia tu? Unafikiri ilikuwa inanunua inasaga unga wa bwimbwi?Dar pale gerezani kuna wahindi hakuna zao ambalo walikuwa hawanunui na kulisaga. Uko wapi wewe? Ushaona unga wa ngano wa serikali? Hiyo 90 unayoongea wewe hata NMC ya serikali ilikuwa imeshakufa.

Msitake kudanganya watu kijinga, hii ni JF mkadanganyane jobless corner zenu huko.
Ukiongea uwe na uhakika, mimi kwetu ni dar ila iringa nilikuwa nimeenda kimasomo.
Nmc ilikuwa haijafa kipindi hicho na walikuwa na ghala kubwa iringa mjini. Ulizia wenyeji wa iringa waliokuwepo kipindi hicho.
Unamjua marehemu boymanda? Yeye alikuwa analima ngano njombe.
 
Hapa ndipo tunafeli,tutengeneze utaratibu wa kupata soko la nje hasa Egypt na Sudan ndio tuwekeze kwenye kilimo..

Ishu kubwa hapo ni soko maana mziki wa ngao sio wa kitoto
kila siku naona post za kumsifia bashe kukiwa na soko watu watalima tu.
Hii vita imetufumbua macho bado kwenye kilimo tupo nyuma
 
Ngano zamani sana ilikuwa inanunuliwa sehemu mbili, Unga Limited Arusha na serikalii NMC pale oppossite na TAZARA ambapo kwa sasa ni Bakhresa. Hizo zilikufa hata Nyerere hajang'atuka.
Unabisha nini na unakubali nini, hivi unafahamu nmc ilikuwa ina ghala kubwa iringa mjini, hiyo nmc iliyokuwa tazara ilikuwa inanunua mazao dar.
Wakati mwingine punguza ujuaji.
 
Unabisha nini na unakubali nini, hivi unafahamu nmc ilikuwa ina ghala kubwa iringa mjini, hiyo nmc iliyokuwa tazara ilikuwa inanunua mazao dar.
Wakati mwingine punguza ujuaji.
Nabisha mengi sana, kuwa NMC bado ilikuwepo 1990. Nabisha kuwa Serikali ilishindwa kuinunua ngano.

Huyo alilima ngano ya kutengenezea Pombe, siyo ya chapati.
 
Ukiongea uwe na uhakika, mimi kwetu ni dar ila iringa nilikuwa nimeenda kimasomo.
Nmc ilikuwa haijafa kipindi hicho na walikuwa na ghala kubwa iringa mjini. Ulizia wenyeji wa iringa waliokuwepo kipindi hicho.
Unamjua marehemu boymanda? Yeye alikuwa analima ngano njombe.
Wewe NMC ilikuwa kwisha, miguu juu. Labda yalibaki majnego na yale ma silo yao pale Iringa, mpaka mwaka juzi nimeenda yalikuwepo.

Uanfikiri kufa kwa NMC ni kama binadam atakwenda kuzikwa? Kufa ndiko huko, kuwa kaput hakuna kinachoendelea. Mliacha lini kuyaibia na kuyafilisi masirika ya umma?
 
Inasikitisha sana,
Mimi ni mtoka bara Afika.

Kwa ujumla huwezi ukai-define tabia ya mtu mweusi. Lakini ni mtu asiyejali. Maisha yake ni patapotea.

Akipata ajira, ndiyo inakuwa shida kabisa.

Lile neno "Mali ya umma" ndiyo inakuwa "point of reference" kwake.

Hata kiti anachokalia kikiharibika kidogo tu, basi atakisukuma pembeni asubiri ofisini itengeneze.

Kwa kweli inasikitisha. Uwajibikaji ni ziro.

Wazungu wanatujua vizuri sana. Na, bila kupepesa macho, wanatuchukulia kama tulivyo. They know us, and thus deal with us accordingly but cautiously!!
 
Nabisha mengi sana, kuwa NMC bado ilikuwepo 1990. Nabisha kuwa Serikali ilishindwa kuinunua ngano.

Huyo alilima ngano ya kutengenezea Pombe, siyo ya chapati.
Mimi naongelea kitu nachofahamu wewe unabisha ili mradi uonekane unajua
 
Wewe NMC ilikuwa kwisha, miguu juu. Labda yalibaki majnego na yale ma silo yao pale Iringa, mpaka mwaka juzi nimeenda yalikuwepo.

Uanfikiri kufa kwa NMC ni kama binadam atakwenda kuzikwa? Kufa ndiko huko, kuwa kaput hakuna kinachoendelea. Mliacha lini kuyaibia na kuyafilisi masirika ya umma?
Unasema nmc ilifirisika ambacho ni chombo cha serikali lakini unapinga serikali ilishindwa kununua ngano hivi unajielewa.
Ningekuelewa kama ungesema nmc ilishindwa kununua ngano sababu ilifirisika.
 
Back
Top Bottom