Nini kimewasibu chama kikuu cha upinzani Tanzania?

Nini kimewasibu chama kikuu cha upinzani Tanzania?

Chagu wa Malunde

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2015
Posts
8,746
Reaction score
5,772
Najiuliza sana wala sipati jibu, kuna nini kimewasibu wa Chadema? Chama chenu kinaonekana kukubali kushindwa kabla hata refa hajapuliza kipyenga.

Wabunge pamoja na wanachama wanawakimbia. Jana lile nyomi kule Tarime ni aibu kwa chama chenu.

Mmekuwa kama mmepigwa shoti ya umeme na kuduwaa. Hamna hata cha kutuambia mna plan gani ya kujinasua?

Watu mitaani na vijiweni wanasema laana ya Dr Slaa inawatafuna. Ndio kusema bila Dk Slaa kupewa zile classified documents na wazee wa kazi na kuibua madudu msingekuwepo. Maana najiuliza ili chama chenu kipate nguvu lazima nchi iwe na ufisadi wa viongozi wa CCM?

Hamna sehemu kwa sasa ambapo mnaona panapwaya ili mkitetemeshe CCM?

Ngome yenu kubwa kipindi kile ilikuwa Tarime, Arusha, Kilimanjaro, Mwanza na Mbeya. Kwa sasa hizi sehemu zote hamna ushawishi.

Mwanza mlishapoteza, hata Wenje asijaribu tena. Kilimajaro mmepata labda wabunge wawili, mara hampati kabisa na kwa dalili hizi mnakufa kifo cha mende maana Tarime hamna chenu.

Mlikosea, mnatakiwa kuwaomba radhi wananchi ambao waliteseka wakidhani kuwa nyie ni watu wema kumbe wapigaji tu.
 
Wenzio huko Lumumba wanawaza Corona maana hali inazidi kuwa mbaya wewe unaropoka kuhusu Chadema, hao Chadema mkipewa mshindane nao bila msaada wa polisi mtawaweza?!

Sasa mmechanganyikiwa hata hamumjui adui yenu ni nani!.

Pambaneni na adui mmoja mkimaliza ndio mgeukie mwingine (japo CDM ni mpinzani ila kwa akili zenu mbovu mmewaona adui zenu), mshika mawili moja humponyoka.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ushindani wa kisiasa umewashinda. Kiwango Cha uelewa wa siasa Safi kwa watanzania kimeongezeka, na hayo ndio màtokeo na matunda ya sera ya elimu bila malipo.
 
Tume huru ya uchaguzi itaweka kila kitu sawa. Nilitarajia badala ya kuandika huu upuuzi hapa ungehoji hao CCM wamepata wapi kibali cha kukusanyika, wakati kuna Katazo.

Muda wa kufanya siasa za kipuuzi mnapata wapi wakati mnajua fika Chadema haina uhaba wa nyomi?
 
Tume huru ya uchaguzi itaweka kila kitu sawa. Nilitarajia badala ya kuandika huu upuuzi hapa ungehoji hao ccm wamepata wapi kibali cha kukusanyika, wakati kuna Katazo. Muda wa kufanya siasa za kipuuzi mnapata wapi wakati mnajua fika cdm haina uhaba wa nyomi?
Jambo la muhimu ni kuwa ni kuzingatia masharti ya kukeep social distancing. Na hayo yalizingatiwa mr.
 
Leo mko zamu wangapi..chama cha kijani ni wepesi kama karatasi..kinacho wababa ni mbeleko za policcm na tume ya bwana mkubwa tofauti na hapo..hakuna sera zaidi ya kununua wapinzani wenu.

#MaendeleoHayanaChama

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Leo Waitara ndani ya gamba kufanya siasa waziwazi na kupokea kadi za Chadema Dodoma. UVCCM wamekusanya watu eti wanatoa elimu ya Corona lkn hawana tahadhari hata kidogo.

Yetu macho.
 
Tume huru ya uchaguzi itaweka kila kitu sawa. Nilitarajia badala ya kuandika huu upuuzi hapa ungehoji hao ccm wamepata wapi kibali cha kukusanyika, wakati kuna Katazo. Muda wa kufanya siasa za kipuuzi mnapata wapi wakati mnajua fika cdm haina uhaba wa nyomi?
Magufuli kawambia hajakataza mikutano km diwani au mbunge anataka mkutano afanye hivyo uchaguz hautahairishwa.


Akili za kuzaliwa zinajenga
 
Magufuli kawambia hajakataza mikutano km diwani au mbunge anataka mkutano afanye hivyo uchaguz hautahairishwa.


Akili za kuzaliwa zinajenga
Mbona Polepole na Bashiru wanafanya wao ni wabunge au madiwani wa wapi?
 
Najiuliza sana wala sipati jibu,kuna nini kimewasibu wa Chadema?
Chama chenu kinaonekana kukubali kushindwa kabla hata refa hajapuliza kipyenga.
Mlikosea mnatakiwa kuwaomba radhi wananchi ambao waliteseka wakidhani kuwa nyie ni watu wema kumbe wapigaji tu.
Duh...!.
Mimi kazi yangu huwa ni kuuliza tuu
Trend Reading: Wanaohamia CCM wasibezwe! Wanaona mbali, 2020 Majimbo yote kurejeshwa. Je tunarejea nchi ya Chama kimoja? - JamiiForums

Je, CHADEMA inaweza kushinda 2020? Is it serious, credible & mature enough opposition?!. - JamiiForums
P
 
Tuseme kwamba uliyoandika ni sahihi. Sasa naomba unijibu hili swali. Ni kwanini CCM sasa hivi ina hofu sana katika uchaguzi? Hao wananchi unaodai wameiweka kando CHADEMA, mbona katika chaguzi huwa hamuwaamini kama wataonesha mapenzi yao kwa CCM na chuki yao dhidi ya CHADEMA?

Dunia ilishuhudia CCM ya Magufuli ilivyopora ushindi katika uchaguzi wa serikali za mitaa na pia katika chaguzi za marudio. Kama ni kweli CHADEMA ni choka mbaya, inakuwaje basi CCM daima inahitaji Okisijeni ya Dola? Na hili kakiri Katibu Mkuu wa CCM Bashiru. Amekiri kwamba bila nguvu za dola, CCM itang'olewa madarakani kama ilivyokuwa KANU. hayo si maneno yangu, ni vya Katibu Mkuu wa CCM.

Kwa hiyo Tambo za CCM ni propaganda tu za kuwatisha wananchi na CHADEMA. Kuhusu Slaa, alijaribu kuisambaratisha CHADEMA siku ile mbele ya vituo 5 vya televisheni, kwa udhamini wa CCM. Wananchi walimpuuza na kuipa CHADEMA ushindi mkubwa haijawahi kutokea, licha ya uporaji wa CCM.
 
Upumbavu na upuuzi wa wanasiasa wa Tanzania ni kutojali maisha ya watanzania kama wanavyojali matumbo yao. Kuna isue ya Covid 19 wajinga wajinga flani wanaohisi wanajua siasa wanarisk maisha ya watanzania kisa matumbo yao.

Haya maswali yaende kwa wanasiasa wote wapuuzi wa nchi hii

MNADHANI HALI IKIWA MBAYA WATU WAKAFA NDIO MTAPATA KURA?

MNADHANI MAISHA YA WATU YANA THAMANI SAWA NA TAMAA ZENU ZA MADARAKA?

MNADHANI HALI IKIWA MBAYA UCHAGUZI UTAKUA NA THAMANI?

Wanasiasa wa Tz bila kujali ni wa chama gani acheni ujinga.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom