Nini kina sababisha siku za hedhi kupitiliza kama huna mimba?

Nini kina sababisha siku za hedhi kupitiliza kama huna mimba?

Ni muhimu kufahamu tatizo hili limekuwa la muda gani, na mp yako inachukua siku ngapi kuisha, wewe una umri gani, huwa unapata siku zako kila mwezi au la? Mambo mengine ni ya uchunguzi zaidi kwenye njia yako ya uzazi.Hivyo kwa ufupi nakushauri uonane na gynacologist.

mp yangu inachukua siku 3 ya 4 inaruka na kumalizikia ya 5. umri wangu ni kati ya 25-29. huwa napata siku kila mwezi. niimwona gyno ndio akanipa hvo vidonge tajwa hapo juu lakn tatizo bado halijaisha
 
mp yangu inachukua siku 3 ya 4 inaruka na kumalizikia ya 5. umri wangu ni kati ya 25-29. huwa napata siku kila mwezi. niimwona gyno ndio akanipa hvo vidonge tajwa hapo juu lakn tatizo bado halijaisha

unatumia njia yoyote ya uzazi wa mpango?
 
Ok,unfortunately mambo mengine hayawezi kuulizwa kwenye mtandao kutokana na ethics! Ushauri wangu ni kurudi tena kwa gyna kwani kwa kawaida unaweza kuwa ulipewa matibabu hayo ya mwanzo na kwa kuwa hayajasaidia ni vizuri kurudi tena na yeye atajua cha kufanya (kama vile kufanya uchunguzi zaidi wa njia yako ya uzazi n.k). Kama unatumia njia nyingine za contraception kama 'secretary' alivyotaka kufahamu (IUD?) ni vizuri ukamueleza daktari.
 
Masaa 24 unabadilisha mara 3 tu? Labda sijakuelewa. Labda ndio maana imelowa mno. Jaribu kubadilisha kila baada ya masaa manne uone tofauti. be careful Hayo mapedi yanakuuza bacteria baada ya muda Fulani. Kama hauna maumivu makali au upungufu wa Damu sioni tatizo.



HABARI ZA MCHANA JF DOCTOR
Mwenzenu nina tatizo moja, nikiingia mp huwa napata damu nyingi sana. naweza kubadili pedi mara 3 kutwa halafu huwa zimelowana chapachapa. lakini huwa siumwi tumbo wala kiuno. last year nilikwenda kufanya check up muhimbili, nikaambiwa kuwa nina tatizo la hormonal imbalance, nilipewa vidonge ambavyo nilimeza for 3months, kiukweli ndani ya huo muda nilipata nafuu ila baada ya dawa kuisha hali ile ilirudi. je kuna tiba mbadala? kwani hii hali inanibore sana. asanteni sana
 
Mkuu Nyakwaratony,

Pole,
Ningependa kujua mambo kadhaa.

-Ni muda gani damu inatoka hivi na ni muda gani toka kuacha vidonge hivi?
- Kati ya mzunguko na mzunguko je huwa damu inatoka?
-Unatumia njia yeyote ya uzazi wa mpango(hasa vidonge vya majira)
-Je, una watoto?
-Pamoja na tatizo hili huwa je, kuna wakati maziwa yanatoka yenyewe?
- Hapa MNH ulifanya vipimo gani?
-Ulijaribu kumuona daktari mara baada ya kuona tatizo linaendelea?alikushauri nini?

Pamoja na maswali hayo ningependa kukukumbusha kuwa ni vyema kuweka umri bayana kuliko border line(25-29)

"Damu kutoka nyingi" ni VERY subjective, kwa kuwa umetumia kigezo cha pedi(INGAWA SI SAHIHI SANA) ni vizuri kujua, mwanzoni(kawaida huwa unatumia pedi ngapi).
 
HoneyBee ngoja nikufafanulie niliweka pedi sa 1 asubuhî, kufika sa 4 nikawa nimelowa chapachapa nikabadili. kufika sa 8 mchana tena chapachapa nikabadili hapo nikakaa mpka sa 2 usiku. umenielewa?
 
Last edited by a moderator:
Ok,unfortunately mambo mengine hayawezi kuulizwa kwenye mtandao kutokana na ethics! Ushauri wangu ni kurudi tena kwa gyna kwani kwa kawaida unaweza kuwa ulipewa matibabu hayo ya mwanzo na kwa kuwa hayajasaidia ni vizuri kurudi tena na yeye atajua cha kufanya (kama vile kufanya uchunguzi zaidi wa njia yako ya uzazi n.k). Kama unatumia njia nyingine za contraception kama 'secretary' alivyotaka kufahamu (IUD?) ni vizuri ukamueleza daktari.
asante kwa ushauri.
 
hippocratessocratess nakujibu kama ifuatavyo
- hii hali ninayo kama 5 years

- nilishawahi kuchoma sindano moja tu tena ilikuwa mwaka 2006, tangu hapo sijatumia aina yoyote za uzazi wa mpango tofauti na mipira.
- nina mtoto 1 wa miaka 8

- nilipima vipimo vya hormon na ultrasound
- sijarudi tena kwa dr. kwani nipo mkoani.
- nina miaka 27.
naomba unifafanulie kipengele cha mwisho sijakuelewa kabisa. asante
 
Last edited by a moderator:
Asante nimekuelewa. Kwa maelezo yako sidhani kama kuna tatizo especially sababu unakaa saa nane mpaka usiku bila kubadilisha pedi. kubadilisha pedi baada ya masaa matatu ni kawaida Sana , kila mtu anableed tofauti. Kama huna tatizo lingine linaloambatana na kutokwa damu sidhani Kama una tatizo lolote. Damu zinatoka hivi mwanzo hadi mwisho wa period au zinapungua kadri siku zinavokwenda?




HoneyBee ngoja nikufafanulie niliweka pedi sa 1 asubuhî, kufika sa 4 nikawa nimelowa chapachapa nikabadili. kufika sa 8 mchana tena chapachapa nikabadili hapo nikakaa mpka sa 2 usiku. umenielewa?
 
kuna wanawake wengini sikuzao huchukua muda mrefu kukata hadi siku 7 au 8, je wadau hii inasababishwa na nini?
 
Kupiliza kwa hedhi katika hali ya kawaida inaweza kusababishwa na huu mfumo wa vichocheo kubadilika.
Mabadilko haya huweza sababishwa na msongo wa mawazo.

Hata hivyo fertization huweza kutokea kama kawaida lakini implantation ikashindika kutokana na sababu kadhaa, mfano matayarisho hafifu ya mji wa mimba(uterus)ambayo pia huweza sababishwa na irritation ktk uterus na baadhi ya contraceptives au infection au upungufu wa vichocheo kwa ajili maintenance ya embryo katika uterus.Yaani ni kama kuna kani mbili ya kwanza inayoifanya embryo ibaki katika uterus na ya pili ni ile inayoing'oa.Kani hizi ni matokeo ya vichocheo.
Sasa kama kani ya pili imezidi basi inatokea spontaneous abortion na embryo huweza kutoka pamoja na damu na hivyo mhusika asigundue kama alishika mimba na imetoka ,lakini anafikiri kuwa hedhi imechelewa


The same thing has happened to my wife. Yeye amekosa period kama miezi miwili mfululizo then akaanza kusikia tumbo linauma chini ya kitovu.

Tukashauriana aende hosp akapige utra sound,apime mkojo. Kwa mujibu wa dokta akashauri apime mkojo tu akakuta unainfection alipewa dawa akatumia but still anasumbuliwa na tumbo na kutoa uchafu mara kwa mara. Sasa sijajua huo uchafu ndio matokeo ya hiyo sponteneous abortion au laa?

Nasubiri majibu yako ndugu ni muhimu sana.
 
''jamani mimi ni msichana mwenye umri wa miaka ishirini na saba, tokea wiki iliyopita, nimepatwa na hili tatizo japo awali ilikuwa siku nne au tatu sasa naona zimezidi, kwa anayejua tiba, ushauri, nisaidieni wakuu ili shemeji yenu apate huduma''
 
Pole sana.

Japo mimi si dokta lakini ni wazi hii
si hali ya kawaida pia ni vizuri ungetaja
tarehe iliyoanza kutoka ili Ma-dr wakija


Wapate mwanga zaidi na nini kizuri cha
kufanya lakini nina maswali:-

Je hii hali ni mara ya kwanza kwako ?
Utapona kupitia wataalam wa hapa.
 
umetemmbea na mume wa mtu???????????????????
 
Back
Top Bottom