Wengi wao huwa wanaajiriwa kabisa na hayo mashirika kwa kazi hiyo ya kuvujisha taarifa
Sasa sababu zinazowafanya hao agents kushirikiana nao zinaweza kuwa
1. Kupata fedha: Maisha ni magumu jamani na tamaa za watu nyakati hizi zipo juu sana hivyo mtu akifuatwa kuvujisha baadhi ya taarifa kwa kupewa mapesa wengi hawachomia, Ndio maana tunatakiwa kuweka wazalendo wa kweli kwenye nafasi nyeti vinginevyo tunajiua wenyewe kama nchi.
2.Shinikizo: Wengine wanashinikizwa kutoa hizo taarifa yaani utake usitake lazima utoe, Hii mara nyingi inatokea pale ambapo mhusika anakuwa anauchafu mwingi alishawahi fanya au ana makosa yenye ushahidi wakumfunga. Sasa mashirika ya kijasusi yakipata uwo ushahidi watautumia kukufanya kuwa kibaraka wao ndio maana tunatakiwa kuweka watu clean kwenye nafasi nyeti kama urais, uwaziri, wabunge, RC, DC, etc.
Kuna mtu alimiminiwa mvua za bullets ila aka survive sasa kama baadhi ya mashirika yakipata ushahidi wa waliohusika na mbaya zaidi wahusika wakawa wapo serikalini, Wanaweza watumia wahusika kutoa siri kwa makubalioano ya kutotoa ushahidi.
Ndio maana Gvt inapofanya yake wanasema don't leave a footprints behind ina maana kubwa sana hiyo.
3.Itikadi:Wengine wanachochewa na itikadi yaani unakuta shirika lina support itikadi fulani na kuweka viongozi wake huko sasa hawa wafanyakazi wa serikali nao wanaitikadi zao hivyo kupitia itikadi wanaweza bwana na viongozi wao wa dini wakatoa info ndio maana kwa kulijua hilo hapa kwetu viongozi wa dini wengi ni watu wa mfumo.
4.Udanganyifu: Kuwafanya watu waamini kuwa wanasaidia shirika lao kumbe wanatoa taarifa kwa adui.
Hawa ndio wajinga zaidi yaani wanakuwa manipulated kuamini kuwa kutoa kwao taarifa wanaisaidia nchi yao kumbe virce versa is true.