Nini Kinachowachochea Watoa Taarifa au Mawakala Kushirikiana na Mashirika ya Upelelezi?

dgombusi

Senior Member
Joined
Sep 3, 2017
Posts
141
Reaction score
200
Nini hasa kinachowachochea watoa taarifa (informants) au mawakala (agents) kushirikiana na mashirika ya intelijensia?

Tunajua kuwa kazi ya intelijensia na upelelezi inategemea sana taarifa zinazokusanywa kutoka kwa vyanzo mbalimbali.

Ni sababu zipi zinazowafanya watu hawa kuwa tayari kushirikiana?
 
ukijua maana ya informer wala hutapata shida ya hiki unachouliza
 
Je, ni kwa sababu ya:
  1. Malipo ya kifedha au faida nyingine za kiuchumi?
  2. Uzalendo na kujitolea kulinda usalama wa taifa?
  3. Shinikizo au vitisho kutoka kwa mashirika ya upelelezi?
  4. Urafiki au mahusiano binafsi na maafisa wa upelelezi?
  5. Matamanio ya binafsi kama vile kupata kinga dhidi ya mashtaka?
 
Nini hasa kinachowachochea watoa taarifa (informants) au mawakala (agents) kushirikiana na mashirika ya intelijensia?

Tunajua kuwa kazi ya intelijensia na upelelezi inategemea sana taarifa zinazokusanywa kutoka kwa vyanzo mbalimbali.

Ni sababu zipi zinazowafanya watu hawa kuwa tayari kushirikiana?
Kazi
 
ukijua maana ya informer wala hutapata shida ya hiki unachouliza
ni nini hasa maana ya neno "informer"? Hata hivyo,
hoja yangu kuu ni kuangazia nini hasa kinawachochea watoa taarifa hawa kushirikiana na mashirika ya intelijensia.
Sababu zipi zinakuwa nyuma ya uamuzi wao wa kutoa taarifa?
 
Kazi ni muhimu, lakini tunataka kujua ni nini kinachowachochea watoa taarifa kushirikiana na mashirika ya intelijensia. Hii ni kuhusu motisha na sababu binafsi zaidi ya kazi.
 
Kama unaelewa ngeli vizuri unaweza kujisomea hapa

ukishaelewa basi jua kuna maslahi kwa kila taarifa wanayotoa kwenda sehemu husika

Screenshot_20250120-113839.jpg
 
Kazi ni muhimu, lakini tunataka kujua ni nini kinachowachochea watoa taarifa kushirikiana na mashirika ya intelijensia. Hii ni kuhusu motisha na sababu binafsi zaidi ya kazi.
Sisiyefanya kazi na asile,,maneno haya yanabeba maana kubwa sana.
 
Wengi wao huwa wanaajiriwa kabisa na hayo mashirika kwa kazi hiyo ya kuvujisha taarifa
Sasa sababu zinazowafanya hao agents kushirikiana nao zinaweza kuwa
1. Kupata fedha: Maisha ni magumu jamani na tamaa za watu nyakati hizi zipo juu sana hivyo mtu akifuatwa kuvujisha baadhi ya taarifa kwa kupewa mapesa wengi hawachomia, Ndio maana tunatakiwa kuweka wazalendo wa kweli kwenye nafasi nyeti vinginevyo tunajiua wenyewe kama nchi.
2.Shinikizo: Wengine wanashinikizwa kutoa hizo taarifa yaani utake usitake lazima utoe, Hii mara nyingi inatokea pale ambapo mhusika anakuwa anauchafu mwingi alishawahi fanya au ana makosa yenye ushahidi wakumfunga. Sasa mashirika ya kijasusi yakipata uwo ushahidi watautumia kukufanya kuwa kibaraka wao ndio maana tunatakiwa kuweka watu clean kwenye nafasi nyeti kama urais, uwaziri, wabunge, RC, DC, etc.
Kuna mtu alimiminiwa mvua za bullets ila aka survive sasa kama baadhi ya mashirika yakipata ushahidi wa waliohusika na mbaya zaidi wahusika wakawa wapo serikalini, Wanaweza watumia wahusika kutoa siri kwa makubalioano ya kutotoa ushahidi.
Ndio maana Gvt inapofanya yake wanasema don't leave a footprints behind ina maana kubwa sana hiyo.
3.Itikadi:Wengine wanachochewa na itikadi yaani unakuta shirika lina support itikadi fulani na kuweka viongozi wake huko sasa hawa wafanyakazi wa serikali nao wanaitikadi zao hivyo kupitia itikadi wanaweza bwana na viongozi wao wa dini wakatoa info ndio maana kwa kulijua hilo hapa kwetu viongozi wa dini wengi ni watu wa mfumo.
4.Udanganyifu: Kuwafanya watu waamini kuwa wanasaidia shirika lao kumbe wanatoa taarifa kwa adui.
Hawa ndio wajinga zaidi yaani wanakuwa manipulated kuamini kuwa kutoa kwao taarifa wanaisaidia nchi yao kumbe virce versa is true.
 
Ni kweli, kuna sababu nyingi zinazowachochea watoa taarifa kushirikiana na mashirika ya intelijensia, na umeainisha vizuri baadhi ya motisha kama fedha, shinikizo, itikadi, na udanganyifu.

Hii inaonyesha kwamba hizi ndizo sababu zinazotumika na mashirika ya intelijensia,
kupitia maofisa wao, kuwa-manipulate watoa taarifa na kuwafanya kukubali kutoa taarifa.
 
Mleta mada kuna uzi niliutupia humu . Utajifunza na kupata majibu ya swali lako 100%. Fanya kuutafuta.
 
Kuna watu wana katabia tu wamezaliwa nako hawawezi kukaa na siri😂😂😂 ni wambea tu from their mother's wombs😂😂😂
 
MICE: .Money. Ideology.Coercion.Ego

Hizo ni sababu muhimu za kuelewa jinsi watu wanavyoshawishika.

“MICE” ni THEORY OF MOTIVATION inayoelezea (Money, Ideology, Coercion, Ego) kama mifumo ya kushawishi, na envy (wivu) ni ugonjwa wa roho unaoweza kuathiri maamuzi.

Pia, kuna theory nyingine inayoelezea zaidi, inaitwa FIREPLACES. Hii inajumuisha mifumo ya motisha kama:
  1. Financial: Malipo ya kifedha au vitu kama zawadi.
  2. Ideology/Moral: Imani au maadili yanayopingana na ya wengine.
  3. Revenge: Kulipiza kisasi kwa mtu aliyeumiza.
  4. Excitement: Hamasa au furaha inayopatikana kwa kufanya kazi ya mtoa taarifa.
  5. Protection: Kulinda familia au binafsi kutokana na hatari.
  6. Lifestyle: Kuboresha maisha kupitia faida za kuwa mtoa taarifa.
  7. Access: Kupata nafasi ya kujua siri au kulenga malengo binafsi.
  8. Coercion: Kupokea shinikizo au vitisho ya kisiasa au kijinai.
  9. Ego: Kuthaminiwa au kujivunia kwa kufanya kazi hiyo.
  10. Sentence: Kupunguza kifungo au kuharakisha kuachiliwa huru.
 
Back
Top Bottom