Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Inavoonekana siku hizi wamekuwa wengi kuliko zamani sasa je sababu hizo ulozitoa ni sahihi?kutofanya mazoezi wakati wa mimba yaani kubweteka. labda uambiwe na doctor unahitaji bed rest. kula sana vyakula vya protin, unajua mtoto akiwa mkubwa atashindwa kutoka hata ukijifungua salama utachanika sana. usile sana mayai ukiwa na mimba. mwanamke mfupi mara nyingi anakuwa na maumbile ya mgongo mafupi sasa mtoto akiwa mrefu na mnene lazima kisu. hata warefu wengi tu wanafanyiwa operation. pia kuna jambo ambalo haliepukiki, mwanamke kuwa na nyonga ngumu. kuna wanawake wengine wamezaliwa wakiwa na nyonga ngumu kwasababu labda genes za kiume zilizidi kuliko zile za kike, kama nyonga haiko flexible vizuri, hata kama utakuwa mrefu namna gani utapigwa kisu. omba Mungu usifanyiwe operatin kwasababu ni kitu kibaya, unauguza kidonda na unabaki na kovu la maisha, pia wakati wa masika nasikia huwa wanaugua....its terrible. Mungu awasaidie.
Inategemea,Mi nilijifungua kwa operation kutokana na PLACENTA PREVIA
Inavoonekana siku hizi wamekuwa wengi kuliko zamani sasa je sababu hizo ulozitoa ni sahihi?
mie ilikua sababu mtoto mkubwa na nilifanyiwa twice pia kimaumbile ni mfupi., so ni kweli inategemea.
ni kweli kuwa unga wa ulezi unasababisha mtoto kuwa mkubwa?
Je ulaji wa CHIPS hauwezi kuwa sababu ya ongezeko hilo?huo ni uongo mkubwa. Kuna watu wanadanganya wenzao. Huwezi kunambia imbalance ya genes inafanya nyonga kuwa ngumu! Not proved not true. Vinavyosababisha siku hizi ni option ya mama(siku hizi wengi wanaomba?!), nyonga ya mama kuwa ndogo(nutritional deficiency), mtoto kuwa mkubwa zaidi, fetal distress, placenta previa, mtoto kukaa vibaya, cord prolapse, obstructed labour, mama mfupi(posibility ya nyonga ndogo, lakini hapa kuna maajabu yake), congenital malformation(eg hydrocephalus) previous operation na nyinginezo. Lakini siku hizi kuna suala la hela hivyo hospitali nyingi za private wanajiongezea kipato zaidi. Pia wadada wa siku hizi wanaogopa flavour ya uchungu ko wanaomba kupasuliwa.
Mkuu Jacobus,
Pamoja na maelezo mazuri ya usungilo, Nyalotsi, na wengineo, ningependa pia kusema Sababu zipo nyingi kama vile
Sababu zinazotokana na mama;
-Njia ya uzazi kuwa ndogo.
-Mama kuchoka kusukuma.
-Obstructed labour, prolonged labour.
-Damu kutoka wakati wa ujauzito katika matatizo ya Placenta Previa, na mara chache Abruptio Placenta au Ruptured Uterus.
Mtoto:
-Fetal distress.
-Mtoto kuwa mkubwa sana.
-Malpresentation(kwa kawaida mtoto hutanguliza kichwa na hivyo basi anapotanguliza kiungo kingine chochote, kuna hatari katika kujifungua kawaida).
-Mimba ya watoto wengi(multiple pregnancy) lakini hasa mtoto mmoja akiwa hayuko katika presentation ya kawaida na ECV imeshindikana-kulingana na mahali husika.
Imani/Mila🙁Myths)
-Kuogopa kuwa sehemu ya uke itakuwa kubwa.
-Kutotataka kusikia uchungu wa uzazi.
mkuu naomba niunganishe,
naomba unieleze kidogo what is abruption placenta na je husababishwa na nini??nilipata tatizo hilo wakati wa kujifungua na lilisababisha mtt wangu kufa.please naomba unisaidie kuelewa.
thanks.