Nini kinafuata baada ya shule ya msingi kufutiwa matokeo, hatima ya wanafunzi inakuaje?

Titicomb

JF-Expert Member
Joined
Jan 27, 2012
Posts
12,823
Reaction score
21,210
Shule ya msingi ikifutiwa matokeo au ikishikiliwa (withheld) matokeo kwa kosa la uongozi wa shule kufanya udanganyifu nini kinafuata ili watoto waweze kuchaguliwa kuendelea elimu ya upili( secondary)?

~ Watarudia mitihani?
~ Watapewa muda gani kujiandaa na mitihani?
~ Kuchaguliwa shule za sekondari nafasi zao zitakuwaje? Hii inaleta usumbufu sana kwa wazazi na wanafunzi ambao hawahusishwi katika kupanga kufanya udanganyifu.
~ Wakirudi shule gharama atabeba nani?
~ Je, serikali itawasaidia wazazi wasibebeshwe mzigo wa gharama za ziada?

Mwenye uzoefu au taarifa sahihi atuelekeze hapa.

Watu wa wizara husika tunaomba maelezo juu ya hili muweze kupunguza taharuki kwa wazazi na walezi ambao wana watoto wahanga wa tukio hili ambao hawana uzoefu wa kukumbwa na kadhia hii.
 
Hatimae serikali imesikikiliza na kufanya maamuzi sahihi kwa kuwapa watoto nafasi ya kurudia mitihani.
Watoto wanarudia mitihani kesho tarehe 21/12/2022 na 22/12/2022.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…