Nini kinaikumba Japan? Mwakani India inaipiku na kuwa Taifa la tatu lenye uchumi mkubwa Ulimwenguni

Maendeleo ni uwekezaji, hata kama una population billion na huja invest on them (Kuwaelimisha) hakuna kitu watafanya.
 
Pia Japan imejaa wazee! Mambo ya uzazi wa mpango usio na mpango umejibu.
Mbaya zaidi, Japanese wanajiona watu maalumu hawana utamaduni wa kukaribisha wageni - ni wabaguzi.
Mbona Uingereza na Germany zote zimepitwa na India pia na zimejaa wageni?

Hiyo sio sababu ya msingi ,elewa kwamba wamefikia kiwango Cha Juu zaidi Cha Maendeleo with full employment of resources,only technological innovations will determine their fate.

On top of that Elimu Huwa Ina kawaida ya kufanya watu wasizaane ,elewa hilo.
 
Hicho ni kidi Hicho ni Kisingizio export market haijapungua Duniani inazidi kuongezeka
 
Hizo sio sababu za msingi ,sababu kuu ni negative population growth,hata huko USA itafikia siku Moja in case sera za kuzuia wahamiaji zinaendelea maana hao ndio wanaochochea Nguvu kazi Mpya na ongezeko la watu.

Nchi zote ulizotaja hapo Juu zinahitajia Nguvu kazi na Zina import ilimradi tuu uwe skilled kwenye gani za kipaombele ,the same to Canada, Australia nk
 
kwani kuna umuhimu gani kunapoongezeka pato la taifa ikiwa wananchi ni dhofu hali!!!

serikali zijitahidi kupunguz kodi,misaada ya nje na ijikite kuwaongezea thamani watu wake kwa kuwapa elimu.
Kwa Utafiti wangu,Elimu inaounguza Kasi ya kuzaliana matokeo yake ni kupungua Kwa Nguvu kazi ndicho kinawakumba Japan na Western Europe na kimeanza kuwakumba China Kwa Sasa.
 
Social vs economic reasons
 
Tutafika huko miaka ijayo.Projection inasema by 2100 tutakuwa miongoni mwa mataifa 10 yenye watu wengi Duniani and the economy so ni circle tuu ndio maana Kwa Sasa huwezi ikosa 🇹🇿 kwenye top 10 ya Uchumi,uwekey, population growth kwa Africa.
 
- Sababu za japan kushuka kiuchumi ipo Ki demographia zaidi, ina idadi kubwa ya Wazee ambao ni tegemezi japo pia wanatumia sana Robotics kwenye uzalishaji

- India imewekeza sana kwenye viwanda vyake vya nyumbani, hawaencourage habari ya kuagiza vitu kutoka nje, na nchi yoyote ikisimamia hapo lazima ikuwe kiuchumi
 
Kuwa na GDP kubwa Haina maana uko vizuri kwenye welfare ,elewa hilo ila unakuwa na Nguvu za kiuchumi.

Itachukua mda Kwa Watu wa India kuwa na welfare nzuri Kwa sababu wao ni wengi sana so wanatakiwa wawe na Uchumi mkubwa mara 2 au zaidi ya walionao Japan ndio pengine wanaweza kuwa na welfare nzuri Kwa watu wake.
 
Kwanza Japan haijashuka uchumi ila Kasi ya ukuaji ndio Iko slow kiasi kwamba inapitwa na wenye Kasi kubwa.

Ila sababu Yako ni ya msingi.
 
India wanauchumi mkubwa lakini raia wake wengi ni masikini na bado technolojia Yao Iko chini sana.

Japan watu wengi wanaishi maisha mazuri na technojia yao iko juu sana.
Hatua waliyofikia India ndio safari ya ahadi hiyo,huwezi pata hicho unachosema bila kuwa na Uchumi mkubwa.

Watu ndio mtaji mkubwa
 
Wabongo bana kwa kushindanisha nchi za wengine kiuchumi. Yani sisi wenyewe tu hata kunya hatunyi ipasavyo.
View attachment 3160277
Hata Nchi yetu tunaishindanisha mbona? Kwa Sasa tuko top 10,miaka 15 iliyopita hatukuwepo.

Nina uhakika kufika 2030 tutakuwa tumewapita kina Ivory Coast,Angola na tutakuwa tuko sawa na Kenya na kabla ya 2032 tutakuwa tumewapita Kenya na kuwa wa 6 Afrika Kwa Uchumi mkubwa .

Nachoweza kukuhakikishia ni kwamba kabla ya 2040,Kuanzia kina Morocco hao watakuwa mkiani na Tanzania na DRC zitachukua nafasi hapo Juu.
 
India ina idadi kubwa sana ya watu na birth rate yao inazid kuongezeka kila kukicha Ndio maana Magufuli(RIP) akasema mzaliane akiamini population ikiwa kubwa basi uchumi utakuwa mkubwa
Huyu mzee alikuwa na maono.
 
Nguvu Kazi ya taifa hakuna tena..
 
Thubutruuuuuuuuu na muda huo japan anasubilia tu apitwe ...?? Hata huyo mchina alimpita ki bahati nasibu tu maana baada ya kupata tsunami ndio iliwezekana .......ile tsunami iligonga kama theruthi ya japan nzima ........ na kama isingekuwa madhoruba yanayoikumba japan.........basi hilo ni mpaka yesu angerudi ndio ingepitwa
 
Hatua waliyofikia India ndio safari ya ahadi hiyo,huwezi pata hicho unachosema bila kuwa na Uchumi mkubwa.

Watu ndio mtaji mkubwa

India anapopulation kubwa sana na tayari mfumo wao niwakizamani, kuwafanya wengine kuwa slave na wengine matajiri.
Wengi masikini kutumikia wachache mabwanyeye, na sio akili ya kuboresha life standard ya watu kiujumla.

Itawachukua miaka mingi kuwafanya watu wake wawe na life standards kama ya wajapani, lakini pia wahindi wanakufa sana hovyohovyo ilihali life span ya wajapani iko juu sana maana umasikini ni kama haupo, njaa na maradhi ya hovyohovyo hawana pia.

Kumbuka pia Japs ( wajapani) walipigwa Sana mabomu na kusambaratishwa miaka ya 1945 Wakiitwa "Giant of Pacific" lakini imewachukua miaka michache kujijenga upya na kuchagua kuishi low profile.
Still bado Japs wanaresources zote kuweza kufika wanataka kuliko India ni vile tu wameamua kuwa low profile, huwezi kukuta product za mhindi Japani lakini unaweza kukuta products nyingi sana za Mjapani India.
Toyota iko India, Suzuki Iko India, mitsubishi ipo India, Hitachi ipo India, Komatsu ipo India, Kobelco India, nk lakini huwezi kuikuta Tata Japani.
 
Ukuaji mzuri wa uchumi ni ule unaoendana na maisha Bora ya watu.

Huwezi ukasema Una uchumi mkubwa huku watu wako wengi ni masikini.

Uzuri WA hawa wenzetu kila kitu kipo under control na kunakuwa na pre-plan + plan ( short term na long term).
Hao Japs tunaowasema wanajua nini wanafanya, na hata hiyo issue ya population si-ajabu kwenye secret papers zao tayari kuna plan, wameamua kuwa low profile.

Ogopa nchi ambayo ilishamaliza ujinga ujinga wote kama kama wizi, rushwa, ubinafsi, maradhi, umasikini, ujinga.
Africa tuna maneno mengi sana, tunapaswa Kwanza kumaliza Ujinga, umasikini, maradhi, wizi, ubinafsi nk halafu ndio tukuze uchumi, huu uchumi wa kwenye makaratasi ilihali watu wako bado wajinga, wezi, wala rushwa, wanakufa bado kwa malaria na kipindupindu ni upumbavu tu.
 
Ukuaji mzuri wa uchumi ni ule unaoendana na maisha Bora ya watu.

Huwezi ukasema Una uchumi mkubwa huku watu wako wengi ni masikini.

Uzuri WA hawa wenzetu kila kitu kipo under control na kunakuwa na pre-plan + plan ( short term na long term).
Hao Japs tunaowasema wanajua nini wanafanya, na hata hiyo issue ya population si-ajabu kwenye secret papers zao tayari kuna plan, wameamua kuwa low profile.

Ogopa nchi ambayo ilishamaliza ujinga ujinga wote kama kama wizi, rushwa, ubinafsi, maradhi, umasikini, ujinga.
Africa tuna maneno mengi sana, tunapaswa Kwanza kumaliza Ujinga, umasikini, maradhi, wizi, ubinafsi nk halafu ndio tukuze uchumi, huu uchumi wa kwenye makaratasi ilihali watu wako bado wajinga, wezi, wala rushwa, wanakufa bado kwa malaria na kipindupindu ni upumbavu tu.
 
Kwani saizi alivyopitwa alikuwa hasubiri? Kati ya India na Japan Nchi gani Ina middle resources nyingi na Nguvu kazi?
 
Kwani saizi alivyopitwa alikuwa hasubiri? Kati ya India na Japan Nchi gani Ina middle resources nyingi na Nguvu kazi?
Wewe jua japan kuwa juu ni mpango wa mungu.............haiwezekani watu bilioni na usheeeeee uwapambanishe na watu milion sijui kumi na kitu sijui ishirini na kitu harafu watoke msuli sawa.......wewe mwenyewe uogopi??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…