Harusi nyingi huwa hazina furaha sana kwa wanandoa. Furaha huwa kwa wageni wachache. Kwa sababu zifuatazo.
1. Ratiba huwa ndefu na very intensive. Kuanzia asubuhi saloon, kanisani, hadi ukumbini. Kwa foleni joto na heka heka za Dar unafika ukumbini umeshisha choka.
2. Ratiba za ukumbini. Muda mrefu mmesimama. Templates ni zile zile, maharusi kuingia ukumbini, zawadi, nasaha, chakula, hupati muda wa ku enjoy.
3. Madeni, mara nyingi hadi siku ya harusi mifuko inakuwa imetoboka na unanuka madeni.
Mimi nili enjoy siku ya iliyofuata baada ya harusi. Ambapo nilitoka na mke wangu na marafiki zangu wachache na wake/wapenzi wao.
Tulikuwa couple nane tukaenda kisiwani huko ndo tukafanya shangwe za kweli.
Tulikunywa, kula, kuogelea, kucheza mziki, kula madenda, kulana n.k. Naikumbuka sana siku hii, was one of my wonderful day hapa duania.