Nini kinakuvutia zaidi katika simu janja(smartphones) kutoka kampuni ya Samsung?

N unyama uliopitiliza
 
Hii ni software ya Xiaomi na hii ni moja ya themes zake. Samsung ndio anaiita Color parlete kwenye simu zake.
Nilikuwa tu nataka nikuoneshe tu kuwa hata Mchina hayo mambo anayo. View attachment 2550216
Caller app na sms app za hao unaowatangaza hawana tofauti na tecno, kifupi hakuna unyama wowote humo, njoo samsung ujionee raha ya kupiga simu na txt... feature mingi unyama sana
 
Caller app na sms app za hao unaowatangaza hawana tofauti na tecno, kifupi hakuna unyama wowote humo, njoo samsung ujionee raha ya kupiga simu na txt... feature mingi unyama sana
Kwa kweli nimeona unapigia sana kelele suala la call app na message app, hivi vitu hata sionagi umuhimu wake kwenye UI, ni mambo madogo sana ambayo hayana effects kwenye matumizi yoyote yale ya kila siku. Google ndio amelazimisha Xiaomi atumie Google caller na message app kwenye simu za Xiaomi za Global version na hata sioni shida hapo.

Ninapoongelea uzuri wa UI vitu visivyo na msingi kama calling na messaging apps hata siviweki akili I[emoji706][emoji706]
 
Hii nimeipenda ndugu, ni aina gani nyingine ya simu wana hayo maujanja ya kuwa na akaunti zaidi ya moja kwaajili ya sms, social networks n.k?
 
Hii nimeipenda ndugu, ni aina gani nyingine ya simu wana hayo maujanja ya kuwa na akaunti zaidi ya moja kwaajili ya sms, social networks n.k?
Simu za Xiaomi zina feature inaitwa "Dual Apps" inayokuwezesha kutengeneza copy ya app Fulani na kuzitumia zote mbili kwa kutumia account tofauti. Kwa mfano unaweza kuunda copy ya WhatsApp na ukazitumia zote mbili kwa account tofauti. Sio WhatsApp tu, ni application nyingi sana unaweza kuunda copy yake.

Uzuri zaidi hii feature inaweza kumake sense zaidi ukiitumia sambamba na feature ya "Second Space" ambayo nayo ipo kwenye simu za Xiaomi. Hii inakupa phone layout nyingine kabisa na kufanya iwe kama unatumia simu mbili tofauti ndani ya simu moja. Zile apps zako za siri unazificha Second Space na ili uingie Second Space itahitaji password yako, ukiingia Second Space unazikuta sasa apps zako zote ulizozihamishia huko.
Kwa hiyo unaweza kutengeneza copy ya Facebook halafu hiyo copy unaihamishia Second Space huku kwenye normal phone layout unaacha ile original app. Ndio hivyo, unazitumia kwa account mbili tofauti na hata haziingiliani, unyama sana[emoji91][emoji91]

Simu kama "Xiaomi Redmi Note 10" ina hizo features na bei yake ni around 450,000/= hivi hapa Tanzania, na simu zao nyingi zenye MIUI 12 kwenda juu zina hizo features
 
Vizuri, sasa utawezaje kuzuia sms ya mchepuko isionekane kwenye original app yako?
 
Vizuri, sasa utawezaje kuzuia sms ya mchepuko isionekane kwenye original app yako?
Kama SMS zako za faragha zinaingia kwenye original app maana yake hiyo original app ndio unapaswa kuificha kwenye second space na copy yake ndiyo unaiacha kwenye home screen.
Zile namba za mchepuko unatakiwa kuzisave kwenye account ya app ambayo umeificha Second Space, na namba za kawaida ndio uzitumie kwenye hii app ambayo ipo kwenye normal home screen.
Maana yake ni kwamba mchepuko akituma message, hizo message zitaingia Second Space na mke wako hatoweza kuziona, ni wewe tu unaweza kuzifungua kwa kutumia password yako uliyoiset special kwa ajili ya Second Space.

Ile account ambayo ina SMS salama zisizo za siri ndio unaitumia sasa kwenye normal home screen
 
Samahani mkuu, mimi mbona internet kwenye secure folder haifanyi kazi, yani ukijaribu kuingia kwenye browser inagoma hata ku-create account WhatsApp au Twitter kwenye secure folder bado internet inakataa, nini tatizo ?
 
Samahani mkuu, mimi mbona internet kwenye secure folder haifanyi kazi, yani ukijaribu kuingia kwenye browser inagoma hata ku-create account WhatsApp au Twitter kwenye secure folder bado internet inakataa, nini tatizo ?
Secure folder, unamaanisha Second Space ya Xiaomi au ni simu ya kampuni gani unatumia
 
Hii ndio kampuni nataka kuhamia kwasasa niweke makao huko enyi wana Samsungians wenzangu watarajiwa naomba mnipokee na kunipa ushirikiano.

Simu ambayo nasave sasa kuja kuinunua ni Samsung Galaxy s23 Ultra. Hii chuma nitainunua kwa ikibidi hata kwa kukopa. Ni simu ambayo features zake zimenikuna sana mtima.

Na kwa waliotumia samsung galaxy s22 ultra wanielezea, then i believe hii itakuwa ni the best top kwa ile iliyotangulia sababu ya maboresho ya features.

Sent from my JKM-LX1 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…