Simu za Xiaomi zina feature inaitwa "Dual Apps" inayokuwezesha kutengeneza copy ya app Fulani na kuzitumia zote mbili kwa kutumia account tofauti. Kwa mfano unaweza kuunda copy ya WhatsApp na ukazitumia zote mbili kwa account tofauti. Sio WhatsApp tu, ni application nyingi sana unaweza kuunda copy yake.
Uzuri zaidi hii feature inaweza kumake sense zaidi ukiitumia sambamba na feature ya "Second Space" ambayo nayo ipo kwenye simu za Xiaomi. Hii inakupa phone layout nyingine kabisa na kufanya iwe kama unatumia simu mbili tofauti ndani ya simu moja. Zile apps zako za siri unazificha Second Space na ili uingie Second Space itahitaji password yako, ukiingia Second Space unazikuta sasa apps zako zote ulizozihamishia huko.
Kwa hiyo unaweza kutengeneza copy ya Facebook halafu hiyo copy unaihamishia Second Space huku kwenye normal phone layout unaacha ile original app. Ndio hivyo, unazitumia kwa account mbili tofauti na hata haziingiliani, unyama sana[emoji91][emoji91]
Simu kama "Xiaomi Redmi Note 10" ina hizo features na bei yake ni around 450,000/= hivi hapa Tanzania, na simu zao nyingi zenye MIUI 12 kwenda juu zina hizo features