JUAN MANUEL
JF-Expert Member
- Nov 26, 2010
- 7,808
- 16,972
Juzi Niko kwenye daladala,saa 11 asubuh,jamaa Mmoja,akiwa anashuka akamwambia sister Mmoja,"we dada SI ulisema unashuka tegeta?ndio hapa?"mdada akawa anasimama anachungulia chungulia nje,maana ni asubuh sana,jamaa aliposhuka,Sasa abilia wanamshangaa yule dada,baadae dada akasema,yule vipi mbona ananishobokea,anafikiri nimepotea,mie sijapotea,nacheka kama Kuna gari ya postal!Peace be to you all,
Usiniulize utafiti nimefanya wapi, kwani wewe huna macho ?! Ebo !! Jambo hili liko bayana kabisa.
Tofauti na zamani siku hizi wanawake hawana mvuto wa kike, wengi sura ngumu, zilizokunjamana pia wengi ni shapeless wengi vitambi kama wanaume hata miondoko ni kama wanaume, sauti nazo zimekua ngi ngi nga nga ule unyororo wa sauti za kike kwisha.
Nini chanzo cha haya yote. Yani wanawake wanazidi kua kama wanaume hata kwa tabia, sasa hivi ni kawaida kukuta mwanamke anapeleka mtungi (anakunywa pombe kali) konyagi kavu kavu wakati wote ni mashahidi zamani walikua wanakunywa soda.
siku hizi hata ukimsimamisha mwanamke umtongoze anakukata jicho kavu kama fundi saa, ile kuona kaaibu kuchuma vijani mwanamke akitongozwa hakuna tena, kwanza hata kutongoza hakuna ni kumuita unaelewana location imeisha hiyo.
Hata woga hawana tena, unakuta mwanamke anaangalia movie ya mazombie katoa macho tena anachomekea "hilo likubwa lao silipendi, waliue tu" zamani wanawake walikua waoga.
Nini chanzo cha mabadiliko haya ?
Yule dada mweupe,umbo la kike,lakini swaga zote na uhuni kama dume!!ilinikata stimu vibaya sana.
Siku hz hata wapo wanaume wanakuwa na swaga za kike!
Mtu ananenepa nyonga inakuwa kubwa,juu kidogo!akitembea a Arusha mikono kama shangingi!!!(simaanishi V8,kwa mliozaliwa juzi,namaanisha,shankupe,au lishangazi).
Kwa vijana wa kiume,fuga hata ndevu basi,harafu hata ushikaji wa cm usishike na kuperuzi cm kama demu!!
Huwa nawaona vijana kwenye daladala,Wana chart kama mademu!!