Unajua Nchi hii Mwinyi kaipokea haina hata fedha za kulipia Meli ya mafuta iliyotia nanga Bandarini, Mkapa akiwa Waziri wa mambo ya nje, Msuya akiwa wa fedha na Warioba akiwa PM wamewahi mara kadhaa kuelezea hali ilivyokuwa wakati Mwinyi anaingia
Kuna wenzenu walikaririshwa eti aliua Uchumi, aliua uchumi gani wakati kakuta huwezi kupata bidhaa yoyote bila ya kibali cha Mjumbe wa nyumba 10, Mashirika na mataifa makubwa yote yametususa, ndani uzalishaji na viwanda vimefungwa kwa kukosa malighafi na masoko
Tatizo lenu ni ushamba wa kupima uwezo wa Rais kwa kusikiliza uwezo wake wa kujisifu na kuji mwambafai yeye na Wapambe wake au kufoka foka hadharan kujidai ndio uchapakazi na uzalendo
i.e Mwinyi Ndio Rais pekee wa Nchi hii ambae hata mara moja huwezi kumsikia akijisu alifanya hivi na vile
Tuliza akili usome reforms za Msingi alizofanya Mwinyi kuitoa Nchi kwenye Shimo la Ujamaa wa Nyerere ndio ujue
Nakupa machache tu kwa kuanzia
1) Reform ya kuanzisha TRA ilianzia kwa Mwinyi
2) Vision 2025 ilianzia kwa Mwinyi 1994 ( Kasome Kitabu cha Mzee Mkapa kaeleza kwa kifupi sana)
3) kufuta Azimio la Arusha lililoamini Umaskini ndio uadilifu
4) Uanzishwaji wa Soko huria na kuhusisha Sector Binafsi kwny shughuli za kiuchumi
5) kupunguza Wafanyakazi Serikalini ili wabaki namba inayoendana na uhalisia na kuwezesha Serikali kujiendesha na kuweza kuwalipa
6) Demokrasia imeanza kuota na kumea wakati wa huyu Muungwana kiasi cha hata watu kukosoa Serikali wakiwa Mita 5 kutoka geti la 'usalama wa Taifa'
7) Kuanzisha Mfumo wa Vyama vingi ( kuna baadhi wanajifai eti Nyerere ndio aliamuru vyama vingi viruhusiwe, kama alikuwa na nguvu ya kushinikiza vyama vingi ilikuaje akose nguvu ya kutetea kutofutwa azimio lake la Arusha akabaki analalama pembeni)
Hakuna Rais aliefanya Uamuzi mgumu kwny Nchi hii kama Mwinyi
Angekuwa Muoga wa matusi ya Nyerere angeacha na kizazi chenu kitafunwe na Ujamaa kama kizazi chetu
Magufuli asingekua rais...hata ubunge angeuskia kwenye bomba. Vile vichwa havikupenda watu mbumbumbu...walikua ni intellectuals tupu. Tulianza kukosea kwa Mzee Ruksa.