Kwa hiyo,hili nalo lahitaji ufaham wa hali ya juu au elimu ya chuo kikuu?!
Au wanapoongelea madhara,unahisi nini! Kama kufa,kupo tu. Hakukwepeki.
Ua kuna mambo kadhaa ndo huongelewa:
- Maandalizi yake: kuna sehemu za kawaida sana,ambapo ukiangalia,kuanzia kumenywa,sahani,kachumbali, ni uchafu tu. Na walaji,waliozoea maisha ya shida,hawaoni taabu. Utajua kulingana na bei.
-Mafuta yanayopikiwa: chips kama chips, ndio kupikwa,hunyonya mafuta mengi. Ila,kama tatizo lingekuwa mafuta,wangekufa wengi. Kikubwa mtambue kwamba ikiwa hivo,basi hata walaji wa chapati,ni marehemu.
Kuna mafuta yanarudiwa,hadi rangi inabadilika. Wengine wanaenda mbali na kudai kwamba,kuna mafuta ya transfoma hutumiwa,na sifa kubwa ikiwa hayaishi haraka kama haya ya kawaida.
-La tatu na la mwisho, ni chakula hiki kina virutubisho gani kuujenga mwili!? Kimeongelea hiki tu,ila mfano mwingine ni wali. Unaambiwa hauna manufaa wala madhala mwilini. Ni kujaza tumbo tu.