Nini kipo nyuma ya chips?

Nini kipo nyuma ya chips?

Huwa najiuliza mara nyingi sana kwa nini chips zinasemekana kuwa na madhara.

Chips ni viazi ulaya vilivyokaangwa kwenye mafuta ya kupika.

Lakini ukipika viazi hivyo kwenye mboga au chakula kingine kama wali/pilau hamna mtu atakuambia vina madhara.

Hayo mafuta yanayotumika kukaanga ukiyatumia kupikia au kukaanga chakula kingine hamna mtu anayasema hayo mafuta.

Lakini tatizo linakuja hayo mafuta yakikaanga viazi vilivyokatwa vipande (chips) ndo vinakuwa na madhara mara nguvu za kiume, mara mambo kibao.

Watu wenye uelewa na hili tafadhali nielewesheni hapa
Si chips tu, jihadhari na vyakula vya kukaangwa huwa na mafuta yaliyozidi kiwango, pilau nayo haina tofauti na chips kwani huwa na mafuta mengi.
 
Kwa hiyo,hili nalo lahitaji ufaham wa hali ya juu au elimu ya chuo kikuu?!

Au wanapoongelea madhara,unahisi nini! Kama kufa,kupo tu. Hakukwepeki.

Ua kuna mambo kadhaa ndo huongelewa:
- Maandalizi yake: kuna sehemu za kawaida sana,ambapo ukiangalia,kuanzia kumenywa,sahani,kachumbali, ni uchafu tu. Na walaji,waliozoea maisha ya shida,hawaoni taabu. Utajua kulingana na bei.
-Mafuta yanayopikiwa: chips kama chips, ndio kupikwa,hunyonya mafuta mengi. Ila,kama tatizo lingekuwa mafuta,wangekufa wengi. Kikubwa mtambue kwamba ikiwa hivo,basi hata walaji wa chapati,ni marehemu.
Kuna mafuta yanarudiwa,hadi rangi inabadilika. Wengine wanaenda mbali na kudai kwamba,kuna mafuta ya transfoma hutumiwa,na sifa kubwa ikiwa hayaishi haraka kama haya ya kawaida.
-La tatu na la mwisho, ni chakula hiki kina virutubisho gani kuujenga mwili!? Kimeongelea hiki tu,ila mfano mwingine ni wali. Unaambiwa hauna manufaa wala madhala mwilini. Ni kujaza tumbo tu.
Mh kweli wali hauna faida mwilini kweli?
 
Hata mihogo siyo mizuri ila mihogo hailiki sana kama chips. Mihogo inatumika pengine kwa chai tu na watu hawali mingi. Chips inatumika kama chakula halafu texture ya viazi inanyonya mafuta mengi.
Waulize wanachuo kati ya chips na mihogo nn wanakula sana?
 
Kaanga chips hakikisha mafuta yamejichuja vizuri.

Siku hizi kuna mashine za kuhoka chips bila mafuta.

Kama unawajuwa KFC nunuwa chips kwao ndio utajuwa chips zinatakiwa ziweje.

Wee kwa hiyo za kfc hazina madhara? Basi Marekani tatizo la kuzidi uzito lisingekuwepo. Au kwa kuwa hapa mnazila chips za kfc kama mtoko na sio kama chakula cha kila siku na ndio sababu huoni madhara yake kwa uharaka?
 
Kwanza sio chakula cha kondeni. Hichi kiazi kimebuniwa tu. Pili kinakunywa mno mafuta. Tatu kwa kuwa sio chakula cha kondeni kwa mujibu wa bibilia. Hakina baraka
Asante bwana pastor kwa kuturejesha Eden 😂!

Yes hivyo viazi havijawahi kuwepo dunia sawa na wale kuku ambao ukimweka chini atakusubiri hadi uje umchukue.
 
Huwa najiuliza mara nyingi sana kwa nini chips zinasemekana kuwa na madhara.

Chips ni viazi ulaya vilivyokaangwa kwenye mafuta ya kupika.

Lakini ukipika viazi hivyo kwenye mboga au chakula kingine kama wali/pilau hamna mtu atakuambia vina madhara.

Hayo mafuta yanayotumika kukaanga ukiyatumia kupikia au kukaanga chakula kingine hamna mtu anayasema hayo mafuta.

Lakini tatizo linakuja hayo mafuta yakikaanga viazi vilivyokatwa vipande (chips) ndo vinakuwa na madhara mara nguvu za kiume, mara mambo kibao.

Watu wenye uelewa na hili tafadhali nielewesheni hapa
Vitabu vya dini vinasisitiza kufanya chochote kwa kiasi.
Kula chips kwa kiasi.
Hata hivyo visvyotumia mafuta navyo kula kwa kiasi.

Mengine ni wivu tu.
 
Huwa najiuliza mara nyingi sana kwa nini chips zinasemekana kuwa na madhara.

Chips ni viazi ulaya vilivyokaangwa kwenye mafuta ya kupika.

Lakini ukipika viazi hivyo kwenye mboga au chakula kingine kama wali/pilau hamna mtu atakuambia vina madhara.

Hayo mafuta yanayotumika kukaanga ukiyatumia kupikia au kukaanga chakula kingine hamna mtu anayasema hayo mafuta.

Lakini tatizo linakuja hayo mafuta yakikaanga viazi vilivyokatwa vipande (chips) ndo vinakuwa na madhara mara nguvu za kiume, mara mambo kibao.

Watu wenye uelewa na hili tafadhali nielewesheni
Dkt Janabi shughulikia
Dkt Janabi.
 
Back
Top Bottom