Vijana wa kibongo wake/waume wa kibongo kukimbilia kuolewa, ndio ndoto kubwa kwao sababu ya kutokua na ndoto zao wanaanza kutimiza ndoto za watu wengine( wazazi, ndugu, marafiki).
Demu akifika 30 anaitwa mzee hawezi kuolewa, ana force kuolewa na mtu yoyote yule pasipo kujipanga mwisho, anajikuta kaingia sipo yanaanza majuto.
Kuzaa majaliwa na mipango ikae sawa sababu malezi sio kitu rahisi, uwezo wa kipato, mtu sahihi, muda sahihi, watu wamekimbilia kuzaa kulea kumewashinda, watoto wamejazana mtaani, wezi vibaka, wadangaji kibao, mama, baba na mtoto wote mnadanga.
Hizi ni mind set za kiafrica ambazo lazima tuachane nazo, mzazi usilazimishe mtoto aoe au aolewe mwache afanye kwa muda wake, kuzaa sio lazima timiza malengo yako ndoto zako kwanza, hili uzao wako usipitie majuto ya kuzaliwa na wewe uhakika wa elimu, afya..
Kila mtu afanye maisha kwa namna yake, ashinde mechi zake, usiiishi ndoto za mtu mwingine hata kama ni mzazi wako.
Hatuwezi wote tukafanya vitu vinavyonana tukapata matokeo tofauti.
Big up kwa salama na jay dee, mungu awajalie mkipata watoto kheri mkikosa kheri vilevile, hakuna kesi wala dhambi.