Nini kipo nyuma ya ukuaji na ongezeko la watu wasiokuwa na dini?

Very true and well elaborated.....now I do believe you must be knowing that there is a difference between Faith and religion as this is vivid and obvious as per the statement you have given above.
 
Heri uamini yupo uende usimkute kuliko uamini hayupo uende umkute.
 
Sababu mimi ninayo ona sana ni kwamba mungu yupo ila walewaliopewa wawasilishe habari yake ndio wanaochanganya habari na ndio inafikia mpaka watu wanashindwa kuamini kwa mfano haya makanisa mengi tuu yamejitengenezea system zao za kuwasilisha hizi habari amabapo ukifikiria hazina maana na wakati mwingine unaweza kujiuliza inatokea vipi Mfano mtu anakuambia Mungu alisema tusiue tena baadae anawapa amri wengine waue ukiuliza majibu yanakua mengi mfano mzuri, N hii ishu sio kwetu tuu ilianzia kwa hao waisraeli waliopewa uelewa wake mara ya kwanza na wakabadilisha yakawa mengine'

Pili watu wanachanganya changamoto za kidunia na Mungu yaani kila kitu wanamtupia Mungu sasa ukifikiria hivi lazima ujiulize mfano mtu ni maskini anaeda kanisani anaomba still bado haendelei anasema ni shetani sasa unajiuliza kama Mungu tunaomba ili atusaidia inakuwa vipi tena shetan anafanya maisha yetu yanakua magumu

Tatu ni uumbaji au kuwa na story zisizo kuwa na uelekeo mmoja amabao unatoa picha halisi ya matukio ya kuungaisha kuna maswali mengine magumu na hayana majibu na hata hawa wanaosema wanajua neno la mungu wanatoa mafunzo tofauti amabayo pia yanaishai gizani mfano'
Tunaambiwa walikuwa watu wawili tu duniani wakazaa watoto kama familia sasa watu wengine wakatokea??
Kwanini kuna race tofauti tofauti kama wote tulitokea kwa mtu mmoja??
Kama shetani aligomabana na Mungu kwanini hakumuua a kumuacha aje asumbue kiumbe chake pendwa mpaka kufikia hatua ya kuchomana moto??

Kwamimj ninaamini Mungu yupo ila aliumba ulimwengu kauwekea forces zake atakaesurvive kwa aina yoyote ile ndio ataendelea uwe mpagani , uwe jambazi ile siku ya mwisho ikikukuta umeomba msamaha na mwisho huenda akawepo au asiwepo kama asipokuwepo basi ukifa ndo umetoka sasa bahati mabaya akawepo na hukua amini hapo ndio kazi
 
Nikiwaza siku ya mwisho matendo yetu yataoneshwa kwenye tv naishiwa nguvu
Hakuna kitu kama hicho, watu wa dini wamejaribu kutumia mbinu zote kututisha Ila hakuna siku ya mwisho.

Siku ya mwisho ni pale jeneza likishushwa na wakulungwa kutupia chepe za uhakika, tena wana haraka sijui huwa ni kwa nini.

Dini hizi za Caucasians na Arabs ndio zitupeleke mbinguni, kweli jamani?
 
Yan we mchungaji wako awe gwajima alaf akwambie zinaa mbaya hivi utamwelewa kweli na wakat unajua kabisa ye mwenywe ana video yake kabsa kule site pendwa ya wahuni XXXVideo? Lazma tu uone dini ni usanii.
 
Kama Mungu anadhihakiwa na kudharauriwa hivi hadharani

Ni dalili za wazi mwisho wa dunia haupo mbali sana
hivi dunia ilaianza kuisha lini maana tokea malaika wanaumbwa walimkataa na kufuata mambo yao , waisaraeli mika hiyo ya kina musa ndo kabisa vita kila kona walipigana waliua ndugu zao ..hebu tupo dunia ilianza kuisha lini au ilianza kuisha pale walipowekwa watu tu duniani? au
 
Ni dalili nzuri ya watu kujitambua na kujikomboa kifikra. Ni muhimu kuwa na Mungu lakini siyo dini. Dini ni mifumo ya kiimani iliyotungwa na wanadamu ili kukidhi matakwa yao binafsi. Hata wewe ukiamua unaweza kubuni dini yako ukawahamasisha watu kisha ukapata wafuasi(wa muda na wa kudumu).

Sent from my VF-795 using JamiiForums mobile app
 
Hivi kama kweli una akili timamu utaenda kanisa la gwaji boy?! Mla kondoo, watoto na mali zake?!
Kama kweli ...utaenda kanisa la Anglican linaloruhusu ushoga na ndoa za jinsia moja?!
Au katoliki ambao wanaenda njia moja na Anglican?!
Au uislamu uliojaa visasi, kuuwa, kunyima haki za wanawake waliowaleta duniani na kuwalea?!
Dini ni perfume kupunguza harufu ya maovu, husuda, wivu, tamaa, mauaji na matendo machafu ya binadamu, inakupa sense ufanyacho hata kama ni kibaya eti utasamehewa tu, kama walokole na namna hiyo wakitoka kusali na kunena ni gesti au popote kupigana miti tu..!
 
Upagani ni jina la kutaja imani za dini ambazo ama zinaabudu miungu mingi au ni dini za jadi.

Context yangu ni watu kupoteza ushawishi na kutokuwa katika dini.
Upagani ni kikundi chochote cha watu, kiimani ambacho siyo "popular" ' hakina mawanda mapana ya kijografia, mfano, bara moja hadi lingine.' Na chaweza kuwa kinaabudu Mungu mmoja au miungu.
 
Ukuaji wa manabii wa uongo unakatiisha tamaa watu. Ukimuahidi mtu utamponya ukimwi, mwisho wa siku afe, unakatisha tamaa ndugu.
 
Binafsi yalivyonipata nilimtafuta Mungu. Nimeleta hoja hii baada ya kuona ushawishi umepungua kwa walio wengi.
Mi naona unapoishi wewe usijumuishe kote makanisa mengi sana yanajaa watu mbaka nje so jiongelee wewe binafsi unayefata kuchunguza watu badala ya kusali πŸ™„πŸ™„
 
Dini ililetwa na mzungu, kwanini mpaka leo bado kuna watu hawajielewi wakati walioleta dini kwa asilimia kubwa wameisha itupa kule
Inasikitisha sana na fikra zako hizo eti wazungu walileta na wameitupa???!! Tembea uone nchi za kizungu usiongee habari za vijiweni halafu msipende kukremisha ukristo ni uzungu dah??!!! Mbaka leo bado unaakili hizi Mungu akusaidie sana
 
Mengi tu, kibwetere alipiga kiberiti waumini

Juzi mwamposa kaua zaidi ya watu 20 kwenye kukanyaga mafuta na still watu wanazidi kujazana kwenye matamasha yake, do you think they use common sense effectively?
Mbona uongelei uislam watu wanakufa maka 500000 kwa kukajagana na mbaka leo misikiti mingi mashariki ya kati inatapakaa damu huoji unakazana na kanisa tuuuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…