Mbona unajichaganya sasa?
Mkristo ukizini umetenda dhambi au hujatenda?
Kama hujatenda sawa.
Ila kama umetenda dhambi si ni uasi wa sheria? Kutokusikiliza sauti ya Mungu ndani yako si ndo kutenda dhambi?
Tatizo ndugu yangu huelewi kuhusu mambo ya sheria na pia huelewi kuhusu mambo ya neema(kuongozwa na roho).
Unanifanya nianzie mbali sana.
Watu wanaotumia Biblia kama muongozo wako makundi mawili.Kundi la kwanza ni lile kundi linalofuata agano la Mungu na wanawaisrael Sinai.Kundi hili ni lile ambalo linatambua dhambi kwa kupitia amri ambazo Musa alipewa mlimani sinai. Kundi hili linaamini kuhesabiwa haki na Mungu kunapatikana kwa kuepuka kutenda yale yaliyokatazwa na Mungu kupitia Musa. Well wako sahihi lakini je inawezekana kumpendeza Mungu kwa kuzishika AMRI zake?(Hili ndo kundi unalolitambua wewe)
Kundi la pili ni la wale ambao wapo chini ya Agano la Neema.Watu hawa wametambua kuwa ni impossible kuzishika hizo AMRI ili upate kuhesabiwa haki.Namna pekee ya kumpendeza Mungu ni kumruhusu yeye mwenyewe akuongoze kwenye kila maamuzi unayokutana nayo mbele yako. Na kundi hili ndilo haliongozwi na sheria.Linaongozwa na Roho wa Mungu ndani yao.
Nakupa mfano
Jamaa mmoja (John) alikuwa na familia yake lakini alikuwa mlevi mbwa na hataki kununulia hata watoto wake nguo.Jirani yake (Chale) akachukua pesa za jamaa bila jamaa kujua akawanunulia nguo watoto wa jamaa na kuwalipia ada.
Kwa watu wanaoongozwa na sheria Chale amefanya dhambi,ingekuwa ni heri kwa chale awaache tu watembee uchi kuliko alichokifanya maana ameiba hivyo ametenda dhambi.
Kwa watu wanaoongozwa na Roho chale hakufanya dhambi kwa sababu upendo kwa wale watoto umemsukuma kufanya alilofanya ili kwasitiri wale watoto.(Note Chale amewasaidia hawa watoto kupata haki yao kutoka kwa baba yao)
Kwenye Biblia Daudi alikula mikate ya hekaluni ambayo kwa sheria ya Musa lilikuwa ni kosa kubwa sana lakini hakuhesabiwa dhambi kwa sababu alifanya jambo kubwa zaidi la kuokoa uhai wake na wa wale aliokuwa nao.Kama angeamua kuongozwa na sheria basi pengine angelikufa na njaa.Lakini aliamua kuongozwa na roho wa Mungu ndani yake akala yeye na watu wakaokoka.
Kuasi ni kudisobey sauti ya Mungu ndani yako.Sio kudisobey sheria.
Nimeongea kwa ufupi sana.Hii opic ni kubwa mno.