Kama HAKi inatendeka, yeyote akishinda ni sawa.haki naana yek ni nini? ni kwa upinzani kushinda ndipo inakuwa haki?
Kwa taarifa yako haki duniani hakuna ila kuna maigizo ya haki ndio maana unaweza ukaua na ushahidi ukautengeneza na ukashinda kesi na kama uamini kamuulize Tundu Lissu amewatetea sana waarifu licha ya kwamba walifanya makosa lakini walionekana hawakufanya.Binafsi nilipoandika uzi wa Tanzania Kwanza watu walinishambulia na katika kunishambulia waliweka maneno HAKI na AMANI.
Hivi nini kitangulie, haki au amani? Kwa sababu penye vurugu hata hiyo haki haiwezi kupatikana.
Amani kwanza haki ndo ifateBinafsi nilipoandika uzi wa Tanzania Kwanza watu walinishambulia na katika kunishambulia waliweka maneno HAKI na AMANI.
Hivi nini kitangulie, haki au amani? Kwa sababu penye vurugu hata hiyo haki haiwezi kupatikana.
Huu uchambuzi ulitakiwa usambazwe kwa viongozi wote wa CCM, BAKWATA, CCT, TEC na midoli ya Lumumba.Unapiganaje kutafuta amani wakati wakati kupigana kwenyewe huondoa amani?!
Na hata kama ingekuwa watu wanapigana kutafuta amani, bado pia ulitakiwa kutafuta kwanini walipigana!!
Watu wanapohangaika kutafuta amani kwanza ndipo haki ichukue nafasi ni katika mazingira ambayo tayari amani imeshavurugika, na katika mazingira kama hayo, of course, no peace no justice!!!
Lakini katika nchi kama yetu tunatakiwa kutafuta na kutoa haki kwanza ili tusifikie kupigana kutafuta haki na hatimae kulazimika kutafuta amani kwanza ndipo haki itawale!!
Mababu zetu walipigana Vita Vya Majimaji sio kwa ajili ya kutafuta amani bali kutafuta haki ambayo ilipokonywa na Wajerumani na kuwafanya babu zetu kama viumbe dhalili!!
Kule Nigeria kulitokea vita vya wenyewe kwa wenyewe in the name of Biafra War! Watu wa Biafra hawakuanzisha vita ile kutafuta amani bali walianzisha kupigania kile walichoona kukiukwa kwa haki zao!!!
Enzi za ubaguzi wa rangi kule SA vurugu zilikuwa haziishi!!
Vurugu zile za SA hazikuwa za kutafuta amani bali za kutafuta hakl ambayo iliporwa na makabaru na kuwafanya watu weusi kuwa ni watu wa daraja la chini!!
USA nako kumekuwa zikitokea vurugu! Vurugu zile zinatokana na kile kinachodhaniwa mamlaka kutotenda haki kwa watu weusi na wala sio vurugu za kutafuta amani!!!
Watu wa CCM wamekuwa wakiwaita wale wale wanaowasaidia kwa majina mabaya kama vile Mabeberu! Hasira hizi za wana-CCM bila kujali kama zina mantiki au hapana hazitokani na wao kuamini kwamba Mabeberu wanavuruga amani nchini bali zinatokana na wao kuamini Mabeberu wanaingilia mambo ya ndani ya Tanzania wakati mambo ya ndani ya nchi ni haki ya kimsingi ya any sovereign state!!!
Itoshe tu kusema kwamba, more often than not, ukiona pahala amani imetoweka basi hapo kuna haki ama imeporwa au haitekelezwi!!!
Hata ndani ya nyumba, amani hutoweka pale haki baina ya wanandoa inaposigidwa... ama mwanamke kutotekeleza wajibu kama mwanamke na hivyo kumnyima mumewe haki yake kama mume, au mume kutotekeleza wajibu wake kama mume na hivyo kumnyima mkewe haki yake kama mke!!
HAKUNA AMANI PASIPO NA HAKI, na hata ikiwepo, inakuwa sio amani bai utulivu ulio chini ya mafuta ya petroli ukisubiri cheche ndogo tu ya moto petroli iripuke na utulivu na kuunguzia mbali utulivu!!
Tanzania tumekuwa na amani miaka nenda rudi!Kwa maana hiyo nadharia ya nini kiwepo kwanza hapa haifanyi kazi maana tayari amani tumekuwa nayo toka uhuru!Sasa kinachotakiwa ni haki ili kuendelea kuilinda hii amani ambayo imekuwepo!Wakati tunachangia tujaribu kuendana na uhalisia!Inahitaji akili kubwa sana kueleza kwa ufasaha dhana ya haki na amani.
1. Kuna nyakati watu hupigana ili kutafuta amani.
2. Vurugu sio kinyume/ (opposite of) cha amani.
Dhana ya Haki na Amani huwa aimuliwi kwa kuangalia kipi kinatangulia.
Kumbuka :- Amani ikiwepo inatoa nafasi kwa haki kutendeka, Haki ikiwepo inatoa uhuru na hakikisho la watu kufurahia amani.
Justice and peace is a two headed snake.
Ni kweli penye vurugu hakuwezi kuwa na haki, lakini jiulize, vurugu huletwa na nini?Binafsi nilipoandika uzi wa Tanzania Kwanza watu walinishambulia na katika kunishambulia waliweka maneno HAKI na AMANI.
Hivi nini kitangulie, haki au amani? Kwa sababu penye vurugu hata hiyo haki haiwezi kupatikana.
Kupigana huja mnapotofautiana, hasa mmoja anapomdhulumu mwingine haki yake. tukitaka watu wasipigane, tulinde haki zao.Mmh watu hupigana wakitafuta amani mbona sio kweli, kwani kupigana huja mnapokubaliana au kutofautiana?. Penye amani ndo Penye mafanikio, penye maisha. Amani huzaa haki, na haki huendana na wajibu.
Mkuu, Jambo la mke kumtimizia haki zake ni kitendo cha ujumla Sana!Haki ni mama wa amani. Hata ndani ya ndoa kama mume ukimtimizia mwanamke haki yake basi ndoa itakuwa na amani. Hata katika taifa, kukiwa na HAKI basi ujue na AMANI itashamili
Sent from my SM-J250F using JamiiForums mobile app
Kwanini huelewi bibie; ukumbuke mwanzo kwenye jamii hayo yote mawili (haki na amani) huwepo, kinachotokea mpaka tena kuanza kutafuta kimojawapo lazima pawe na sababu, na sababu yenyewe ni pale kundi moja kwenye jamii litakapoona linaonewa( halitendewi haki), hapo ndipo huanza mapambano ili kuidai hiyo haki yao, na mapambano hayo hatimaye husababisha kuvuruga amani, natumai mpaka hapo utakuwa umeelewa kipi huanza.Je bila Aman Kuna haki inaeza kutendeka maana moja laweza kuchelewa
Haki ikitendeka sehemu yoyote Amani inashamiri. Iwe ngazi ya familia au taifa haki ndio huleta aani. Na amani no kitu kilicho rohoni mwa MTU. Ukiona jamii inatamba tuna Amani na utulivu ,wakati kuna viashiria vya kutotendeana haki kati yao ujue hapo kuna kundi linalokandamiza jingine na hao wanaokandamizwa wantutkutia ndani na kuomba Mungu siku moja mambo yabadilike . hapo ndipo mkandamizaji hutamba tuna amani na utulivu. Unaweza usipambane na mkandamizaji Wa haki zako , kwa kujua tu huna nguvu za kupigana naye lakini rohoni unaomba siku moja mambo yabadilike ukiwa bado hai.Amani ni zao la haki, bila haki amani haitakuwepo