TUJITEGEMEE,
Nakubaliana na wewe kwa 101% kwamba it's almost IMPOSSIBLE kwa jamii yoyote ile kuwa na amani kwa 100%!
Hata hivyo, kuna uzuri mmoja unaoweza kutofautisha mahitaji na utolewaji wa AMANI na HAKI!!
Jamii yoyote ile ina mahitaji ya aina mbili za haki, ambazo ni Haki (Rights/Justice) za Kitaasisi na Haki (Rights/Justice) za Kibinafsi.
Haki za Kitaasisi ni kama ambavyo Vyama vya Upinzani vimekuwa vikiilalamikia serikali kutendewa au kutotendewa vile ambavyo ingepaswa kuwa! Kwa mfano, sote tulishuhudia JPM akipiga marufuku kufanya shughuli za kisiasa kwa hoja kwamba wakati wa kufanya siasa ulishapita na ambacho kiliwepo ni "Kufanya Kazi"!
Cha ajabu, agizo hilo likaonekana kuwa enforced zaidi dhidi ya Upinzani kuliko ilivyokuwa dhidi ya Chama Tawala!!
Kwa bahati mbaya sana, ukiukwaji wa Haki za Kitaasisi ndio wenye nafasi kubwa sana ya kuvuruga amani kwa urahisi zaidi ukilinganisha na zile Haki Binafsi!! Kwa maana nyingine, tusidhani threats hapa ni zile haki ulizosema za wabinafsi bali ni haki za kitaasisi ambazo haiwezi kuwa halali wale wanaozipigania haki hizo wakawa branded kwamba ni wabinafsi kwa sababu wanachopigania sio individual rights/justice bali institutional rights/justice!!
Lakini pia uzuri ni kwamba, ni rahisi ku-fulfill (kutoa) Haki za Kitaasisi in fully kuliko kutoa Haki Binafsi, hali inayoakisi hoja yako kwamba kwamba ni ngumu if not impossible kumridhisha kila mmoja!!!
Lakini ingawaje it's almost POSSIBLE kutoa as much as 100% of Haki za Kitaasisi, kwa bahati mbaya isiyo na uhalali wa kuwa bahati mbaya, hizi Haki za Kitaasisi huwa zinaathiri maslahi ya serikali isyo na taasisi imara ama directly au indirectly!!
Kwa mfano, kwa Vyama vya Upinzani kupokwa haki ya kuendesha shughuli za kisiasa for more than 4 years, kumeifaidisha sana serikali na chama chake!!! Na kama ndivyo, kuacha haki itendeke kwa upinzani kungeathiri maslahi ya serikali na chama chake ambayo imeyapata kutokana na ukiukwaji huo!!!
Sasa tabia hii ya serikali isiyo na taasisi imara kutegemea kulinda maslahi yake kwa kupoka haki za wengine, ndiko kunakosababisha kuvurugika kwa amani duniani kote!!! That explains my first argument kwamba No Rights/Justice No Peace, na hata inapoaminika kuna Amani, kimsingi inakuwa sio amani bali ni utulivu tu!!!
Kwa mfano, mambo mengi yanayovuruga amani kwenye nchi zingine hata Tanzania yamekuwa yakifanyika kwa miaka nenda rudi lakini kutokana na utulivu wa Watanzania, makundi husika yamekuwa yaki-sacrifce haki zao ili kuendeleza utulivu!!
Kwa mfano, yale aliyokuwa amefanya Jecha kule Zanzibar yalitosha kabisa kuifanya Zanzibar iiingie kwenye machafuko yasiyo na kipimo, na hatimae kuvuruga kabisa amani na utulivu uliokuwepo!!
Kama Zanzibar ingeingia kwenye hali kama hiyo, basi hata Bara nayo isingebaki salama!!!
Mfano huo wa Zanzibar na mingine kadhaa ni ushahidi tosha ni namna gani serikali imekuwa ikiiweka amani na utulivu wa nchi kwenye volatile situation kwa sababu tu zinaacha kutoa au zinapoka haki ambazo zinawezekana kabisa kuzitoa na kutegemea kuhubiri amani wakidhani amani ndio msingi mkuu na sio haki!!!
Serikali imekuwa ikichukulia utulivu wa Watanzania for granted huku wakisahau zipo nchi za Afrika ambazo hapo kabla zilikuwa very stable and peaceful pengine kuliko Tanzania lakini baadae amani zao zikavurugika kupita maelezo!!
Ivory Coast kwa mfano, kabla ya Mapinduzi ya Kijeshi ambayo yalitokea 1999, hii ilikuwa ni nchi ya kupigiwa mfano barani Afrika ! Ivory Coast ilikuwa stable kweli kweli tena pengine kuliko Tanzania but we all know nini hatimae kilitokea kwa zaidi ya miaka 10!
Ilianza kama masihara baada ya Henri Bedie kuingia Ikulu mwaka 1995! Ili kulinda madaraka yake, akaanza kuweka watu ndani hovyo hovyo kwavile tu walikuwa wanampinga huku aki-enforce indiginization(uzawa) principle ili kumdhibiti Alassane Quattara ambae alikuwa mpinzani wake mkuu huku asili yake ikiwa ni Burkina Faso!
Ulevi wa Henri Beddie akauhamishia hadi jeshini... Wajeda wakaona usitutanie, in 1999 wakampindua, na kuanzia hapo amani ya Ivory Coast ikavurugika moja kwa moja kwa sababu bila kutarajia, nchi ikadumbukia kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe!!
Sasa hapo utaona ni namna gani amani ilivurugika moja kwa moja baada ya Henri Beddie kupoka haki za wapinzani wake!!!
Na kwavile alichokuwa amepoka ni haki za kitaasisi, hii ni aina ya haki ambayo ni rahisi sana kuitoa lakini kwavile serikali zisizo na taasisi imara hutaka kuimarisha tawala zao kwa kupoka haki za wapinzani wao, ndipo hapo taabu inapoanza!!!
Serikali ikiwa inatoa haki, wala haitakuwa inatumia muda mwingi kuhubiri amani!! Lakini usipotoa haki, unaweza kila siku kuhubiri amani na bado amani inayohubiriwa ikavurugika beyond repair kwa sababu tu msingi mkuu wa amani ambao ni haki, umepuuzwa!!!