Uchaguzi 2020 Nini kitangulie, haki au amani?

Uchaguzi 2020 Nini kitangulie, haki au amani?

Binafsi nilipoandika uzi wa Tanzania Kwanza watu walinishambulia na katika kunishambulia waliweka maneno HAKI na AMANI.

Hivi nini kitangulie, haki au amani? Kwa sababu penye vurugu hata hiyo haki haiwezi kupatikana.
Penye haki vurugu haina nafasi kwani hata ikiwepo inadhibitika kwa urahisi. Ubaya ni kwamba ikiachiwa haki kutokuwepo kwa muda mrefu hadi ikazaa vurugu kuidhibiti huwa inachukua juhudi kubwa zaidi.
 
Binafsi nilipoandika uzi wa Tanzania Kwanza watu walinishambulia na katika kunishambulia waliweka maneno HAKI na AMANI.

Hivi nini kitangulie, haki au amani? Kwa sababu penye vurugu hata hiyo haki haiwezi kupatikana.
Penye haki sioni vurugu itatoka wapi.
 
Binafsi nilipoandika uzi wa Tanzania Kwanza watu walinishambulia na katika kunishambulia waliweka maneno HAKI na AMANI.

Hivi nini kitangulie, haki au amani? Kwa sababu penye vurugu hata hiyo haki haiwezi kupatikana.
Haki ndiye MAMA wa amani. Penye Haki amani huja automatically!!
 
Binafsi nilipoandika uzi wa Tanzania Kwanza watu walinishambulia na katika kunishambulia waliweka maneno HAKI na AMANI.

Hivi nini kitangulie, haki au amani? Kwa sababu penye vurugu hata hiyo haki haiwezi kupatikana.
Bila haki hakuna amani.
 
Mkuu, Jambo la mke kumtimizia haki zake ni kitendo cha ujumla Sana!

Lakini Haki inayozidi hapo ni tendo la ndoa linalokidhi matakwa ya kila mmoja,

Hilo tendo wengi hawalifanyi Kwa kulidhishana Kwa kuwa hawana Amani, Amani ni utulivu wa moyo, Ni utulivu unaozidi kiwango cha utulivu, na tendo la ndoa hunoga kukiwepo Amani ya moyo, (utulivu)

Amani ndio humpa mtu nguvu ya kutenda Jambo Kwa ukamilifu
Lakini kinachotangulia ni haki mkuu
 
Binafsi nilipoandika uzi wa Tanzania Kwanza watu walinishambulia na katika kunishambulia waliweka maneno HAKI na AMANI.

Hivi nini kitangulie, haki au amani? Kwa sababu penye vurugu hata hiyo haki haiwezi kupatikana.
Uwezi ukawa na amani bila haki.
 
Je bila Aman Kuna haki inaeza kutendeka maana moja laweza kuchelewa
Haki ndio msingi wa Amani. Huwezi kuwa na Amani kama huna Haki. Lakini pia, unaweza kuwa na Haki na ukakosa Amani. Haki kwanza, kisha Amani.
 
Binafsi nilipoandika uzi wa Tanzania Kwanza watu walinishambulia na katika kunishambulia waliweka maneno HAKI na AMANI.

Hivi nini kitangulie, haki au amani? Kwa sababu penye vurugu hata hiyo haki haiwezi kupatikana.
Haki ndo inaanza, amani ni tunda la haki Makaaya!
 
CHADEMA mtajuta kusimamisha msaliti wa Nchi Lissu apeperushe bendera ya CHADEMA Akiwaletea CHADEMA hata wabunge wawili mkatambike
Hapa haizungumzuwi CHADEMA wala idadi ya wabunge, sema tatizo lako Wewe ni speaker ndogo ya wamachinga, unaongea ulicho karirishwa tu!
 
HAKUNA AMANI PASIPO NA HAKI, na hata ikiwepo, inakuwa sio amani bai utulivu ulio chini ya mafuta ya petroli ukisubiri cheche ndogo tu ya moto petroli iripuke na utulivu na kuunguzia mbali utulivu!!
Asante sana Mkuu. Umedadavua vema.

Na mimi nina nyongeza!

Katika jamii. Tena jamii inayojumuisha watu wenye fikra tofauti, utashi tofauti, imani tofauti, milengo tofauti ya kisiasia, uelewa tofauti na mengine kama hayo ni vigumu sana jamii hiyo kuwa na absolute Amani ama 100% ya amani.

Mara nyingi, jamii inayooneka kuwa ina amani ukweli ina kuwa na asilimia kadhaa za amani na zinazobaki ni za utulivu na vurugu. Tukichukulia jamii kama taifa basi utakuta nchi nyingi tena zile zilizoendelea zina utulivu kwa asilimia 60%, amani 1% na vurugu 39%. Asilimia hizi nimezilenga kwa idadi ya watu. Maana amani inapimwa kwa vigezo vya muonekano na matendo ya watu wa jamii husika. Na hili la ukosefu wa amani inatokana ugumu wa kumridhisha kila mtu kwa maana ya kuridhika na kile kinachooneka ni haki yake! Wengi wana tamaa ya kupata zaidi wakidhani kuwa wao wana haki zaidi ya wengine.

Kwa Tanzania, asilimia hizi ubadirika badirika maana na sisi ni binadamu tupo dynamic ! Ila kwa ujumla mara zote Amani huwa ni asilimia tisini na tano, utulivu asilimia nne na vurugu asilimia moja. Na kwenye kubadilika kwa parameters hizi utokea mara zote kati ya vurugu na utulivu!!

Bahati mbaya asilimia tano ya vurugu na utulivu ndiyo ina sauti ya juu kiasi cha kupiga kelele hadi ng'ambo. Na wanapiga kelele kwa dhana ile ile ya kutaka haki zaidi ya wengine! Wako radhi kuwazamisha ile asilimia tisini na tano ya Amani ili watimize hitaji la ubinafsi wao.

Nashauri Watanzania tuendelee kuridhika na haki yetu halali na wale wabinafsi zaidi tuwafundishe na kuwaonyesha madhara ya kupenda haki inayozidi halali yako.

Asanteni. Karibu kwa hoja.
 
Binafsi nilipoandika uzi wa Tanzania Kwanza watu walinishambulia na katika kunishambulia waliweka maneno HAKI na AMANI.

Hivi nini kitangulie, haki au amani? Kwa sababu penye vurugu hata hiyo haki haiwezi kupatikana.
AMANI then Haki
 
Ukifuatilia utakuta hizo vurugu zimesababishwa na kuminywa haki mahali fulani.
 
Binafsi nilipoandika uzi wa Tanzania Kwanza watu walinishambulia na katika kunishambulia waliweka maneno HAKI na AMANI.

Hivi nini kitangulie, haki au amani? Kwa sababu penye vurugu hata hiyo haki haiwezi kupatikana.
Amani ni tunda LA Haki,watu wasipotendewa Haki hata uwalazimishe kulinda Amani ni ndoto.Tukihakikishiwa Haki Amani ni dhahiri.
 
Mashehe, Wachungaji na Maaskofu watahubiri kila neno ili amani idumu nchini kipindi chote cha uchaguzi. Mafanikio ya amani ni pale matendo ya HAKI yatakapo tawala kwa muda wote wa Kupiga, Kuhesabu na Kutangaza matikeo. Tofauti na kutenda HAKI hakuna kitakacho zuia hasira za raia watakao amini kuwa haki imepokwa. Mifano ya nchi zilizopoteza amini kwa kupuuza kutoa HAKI kipindi cha uchaguzi ni mingi. Mwenyezi Mungu atunusuru.
 
Amani ni tunda LA Haki,watu wasipotendewa Haki hata uwalazimishe kulinda Amani ni ndoto.Tukihakikishiwa Haki Amani ni dhahiri.
Bila shaka. Najua Biblia imesema hivyo mara kadhaa. Uhalisia wa leo unaonyesha hivyo hivyo. Tanzania ni mfano halisi. Hata tulipokuwa na utawala wa chama kimoja, viongozi waliaswa na walitekeleza kutenda haki. Walipoleta ujamaa walihakikisha kuwa huduma muhimu za jamii ni bure, km shule na matibabu. Na haki ilitendeka kwa kutokuwa na wanyonyaji wa wazi wazi kama wa Kenya na kwingineko. Mishahara ilijadiliwa na kuongezwa kila mwaka. Vyombo vya habari havikuwa huru lakini ilikuwa ruksa kushambulia utendaji mbovu wa serikali. Baada ya Mwongozo mwaka 1971 ndiyo kabisa mijadala huru vijijini iliwadhibiti watendaji wa huko na wa wilayani. Wafanya kazi wa miaka ya 70 ilikuwa ruksa kugoma na hata kuwakataa mameneja, na walifanya hivyo sana. Ujio wa vyama vingi ulikuta utamaduni wa kuchukia kumnyima mtu haki yake Tanzania, na ukaongeza haki ya kutoa maoni na kujumuika. Utamaduni wa haki haukuwa umekamilika Tanzania, lakini ulikuwepo. Ndiyo sababu ya amani ya miaka mingi. Iliundwa kwenye utamaduni wa haki. Sasa wengi wanalalamika juu ya kukosekana kwa haki. Viongozi wanatakiwa kutafiti ni kwa nini kuna madai hayo sasa zaidi ya wakati mwingine. Kuwaasa wananchi wadumishe amani ni sawa, lakini ni bora zaidi kudumisha haki. Kutishia kuwajeruhi watu kwa vyombo vya dola na kuwaweka rumande kwa sababu tu wameandamana eti ili kulinda amani hakuna mantiki. Amani ya namna hiyo, kama ni amani kweli, haiwi endelevu kwa kuwa kwa juu itaonekana kuwa 'wakorofi' wamedhibitiwa, lakini imejengwa kwenye ukandamizaji na ndani yake kuna fukuto muda wote.
 
TUJITEGEMEE,

Nakubaliana na wewe kwa 101% kwamba it's almost IMPOSSIBLE kwa jamii yoyote ile kuwa na amani kwa 100%!

Hata hivyo, kuna uzuri mmoja unaoweza kutofautisha mahitaji na utolewaji wa AMANI na HAKI!!

Jamii yoyote ile ina mahitaji ya aina mbili za haki, ambazo ni Haki (Rights/Justice) za Kitaasisi na Haki (Rights/Justice) za Kibinafsi.

Haki za Kitaasisi ni kama ambavyo Vyama vya Upinzani vimekuwa vikiilalamikia serikali kutendewa au kutotendewa vile ambavyo ingepaswa kuwa! Kwa mfano, sote tulishuhudia JPM akipiga marufuku kufanya shughuli za kisiasa kwa hoja kwamba wakati wa kufanya siasa ulishapita na ambacho kiliwepo ni "Kufanya Kazi"!

Cha ajabu, agizo hilo likaonekana kuwa enforced zaidi dhidi ya Upinzani kuliko ilivyokuwa dhidi ya Chama Tawala!!

Kwa bahati mbaya sana, ukiukwaji wa Haki za Kitaasisi ndio wenye nafasi kubwa sana ya kuvuruga amani kwa urahisi zaidi ukilinganisha na zile Haki Binafsi!! Kwa maana nyingine, tusidhani threats hapa ni zile haki ulizosema za wabinafsi bali ni haki za kitaasisi ambazo haiwezi kuwa halali wale wanaozipigania haki hizo wakawa branded kwamba ni wabinafsi kwa sababu wanachopigania sio individual rights/justice bali institutional rights/justice!!

Lakini pia uzuri ni kwamba, ni rahisi ku-fulfill (kutoa) Haki za Kitaasisi in fully kuliko kutoa Haki Binafsi, hali inayoakisi hoja yako kwamba kwamba ni ngumu if not impossible kumridhisha kila mmoja!!!

Lakini ingawaje it's almost POSSIBLE kutoa as much as 100% of Haki za Kitaasisi, kwa bahati mbaya isiyo na uhalali wa kuwa bahati mbaya, hizi Haki za Kitaasisi huwa zinaathiri maslahi ya serikali isyo na taasisi imara ama directly au indirectly!!

Kwa mfano, kwa Vyama vya Upinzani kupokwa haki ya kuendesha shughuli za kisiasa for more than 4 years, kumeifaidisha sana serikali na chama chake!!! Na kama ndivyo, kuacha haki itendeke kwa upinzani kungeathiri maslahi ya serikali na chama chake ambayo imeyapata kutokana na ukiukwaji huo!!!

Sasa tabia hii ya serikali isiyo na taasisi imara kutegemea kulinda maslahi yake kwa kupoka haki za wengine, ndiko kunakosababisha kuvurugika kwa amani duniani kote!!! That explains my first argument kwamba No Rights/Justice No Peace, na hata inapoaminika kuna Amani, kimsingi inakuwa sio amani bali ni utulivu tu!!!

Kwa mfano, mambo mengi yanayovuruga amani kwenye nchi zingine hata Tanzania yamekuwa yakifanyika kwa miaka nenda rudi lakini kutokana na utulivu wa Watanzania, makundi husika yamekuwa yaki-sacrifce haki zao ili kuendeleza utulivu!!

Kwa mfano, yale aliyokuwa amefanya Jecha kule Zanzibar yalitosha kabisa kuifanya Zanzibar iiingie kwenye machafuko yasiyo na kipimo, na hatimae kuvuruga kabisa amani na utulivu uliokuwepo!!

Kama Zanzibar ingeingia kwenye hali kama hiyo, basi hata Bara nayo isingebaki salama!!!

Mfano huo wa Zanzibar na mingine kadhaa ni ushahidi tosha ni namna gani serikali imekuwa ikiiweka amani na utulivu wa nchi kwenye volatile situation kwa sababu tu zinaacha kutoa au zinapoka haki ambazo zinawezekana kabisa kuzitoa na kutegemea kuhubiri amani wakidhani amani ndio msingi mkuu na sio haki!!!

Serikali imekuwa ikichukulia utulivu wa Watanzania for granted huku wakisahau zipo nchi za Afrika ambazo hapo kabla zilikuwa very stable and peaceful pengine kuliko Tanzania lakini baadae amani zao zikavurugika kupita maelezo!!

Ivory Coast kwa mfano, kabla ya Mapinduzi ya Kijeshi ambayo yalitokea 1999, hii ilikuwa ni nchi ya kupigiwa mfano barani Afrika ! Ivory Coast ilikuwa stable kweli kweli tena pengine kuliko Tanzania but we all know nini hatimae kilitokea kwa zaidi ya miaka 10!

Ilianza kama masihara baada ya Henri Bedie kuingia Ikulu mwaka 1995! Ili kulinda madaraka yake, akaanza kuweka watu ndani hovyo hovyo kwavile tu walikuwa wanampinga huku aki-enforce indiginization(uzawa) principle ili kumdhibiti Alassane Quattara ambae alikuwa mpinzani wake mkuu huku asili yake ikiwa ni Burkina Faso!

Ulevi wa Henri Beddie akauhamishia hadi jeshini... Wajeda wakaona usitutanie, in 1999 wakampindua, na kuanzia hapo amani ya Ivory Coast ikavurugika moja kwa moja kwa sababu bila kutarajia, nchi ikadumbukia kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe!!

Sasa hapo utaona ni namna gani amani ilivurugika moja kwa moja baada ya Henri Beddie kupoka haki za wapinzani wake!!!

Na kwavile alichokuwa amepoka ni haki za kitaasisi, hii ni aina ya haki ambayo ni rahisi sana kuitoa lakini kwavile serikali zisizo na taasisi imara hutaka kuimarisha tawala zao kwa kupoka haki za wapinzani wao, ndipo hapo taabu inapoanza!!!

Serikali ikiwa inatoa haki, wala haitakuwa inatumia muda mwingi kuhubiri amani!! Lakini usipotoa haki, unaweza kila siku kuhubiri amani na bado amani inayohubiriwa ikavurugika beyond repair kwa sababu tu msingi mkuu wa amani ambao ni haki, umepuuzwa!!!
 
Back
Top Bottom