Uchaguzi 2020 Nini kitangulie, haki au amani?

Uchaguzi 2020 Nini kitangulie, haki au amani?

CHADEMA mtajuta kusimamisha msaliti wa Nchi Lissu apeperushe bendera ya CHADEMA Akiwaletea CHADEMA hata wabunge wawili mkatambike
 
haki naana yek ni nini? ni kwa upinzani kushinda ndipo inakuwa haki?
Kama HAKi inatendeka, yeyote akishinda ni sawa.

Lakini kama mgombea wa upinzani anatekwa, au anakamatwa na polisi anabambikiwa kesi ya uzushi anawekwa ndani hadi muda wa kurudisha fomu upite, halafu mgombea wa CCM anatangazwa kupita bila kupingwa, hapo hakuna haki.

Mfano mwingine ni wasimamizi wa uchaguzi au wakurugenzi kuapisha mawakala wa CCM na kukataa kuapisha wale wa upinzani.

Matukio ya hivyo yamefanywa Sana na CCM Mwaka huu
 
Binafsi nilipoandika uzi wa Tanzania Kwanza watu walinishambulia na katika kunishambulia waliweka maneno HAKI na AMANI.

Hivi nini kitangulie, haki au amani? Kwa sababu penye vurugu hata hiyo haki haiwezi kupatikana.
Kwa taarifa yako haki duniani hakuna ila kuna maigizo ya haki ndio maana unaweza ukaua na ushahidi ukautengeneza na ukashinda kesi na kama uamini kamuulize Tundu Lissu amewatetea sana waarifu licha ya kwamba walifanya makosa lakini walionekana hawakufanya.
 
Binafsi nilipoandika uzi wa Tanzania Kwanza watu walinishambulia na katika kunishambulia waliweka maneno HAKI na AMANI.

Hivi nini kitangulie, haki au amani? Kwa sababu penye vurugu hata hiyo haki haiwezi kupatikana.
Amani kwanza haki ndo ifate
 
Haki haiwezi kupatikana kwenye machafuko

Lakini Haki, inapatikana tu pale panapokuwa na Amani

Kwa hiyo, Amani ndio kila kitu

Na hata hivyo, Mfumo wa maisha yetu yanaonyesha, Tulizaliwa pasipo kuzijua hahi zetu, Ila tulipopevuka ndipo tukaanza kuelewa haki

Hivyo, kitu kinachotangulia ni Amani, Kwa sababu kama tungelizaliwa wakati wa ukosefu wa Amani tungelikufaga pasipo kuelewa nini maana ya haki

Amani Kwanza, na ndipo haki itafutwe katika Hali ileile ya Amani
 
Haki ni mama wa amani. Hata ndani ya ndoa kama mume ukimtimizia mwanamke haki yake basi ndoa itakuwa na amani. Hata katika taifa, kukiwa na HAKI basi ujue na AMANI itashamili

Sent from my SM-J250F using JamiiForums mobile app
 
Dini ya kiislamu wanasema ni dini ya haki
Lakini sijawahi sikia mashekhe wa CCM Kama Alhad Musa, Kipizeo n.k wakiongelela uchaguzi wa haki zaidi ya Shekhe Ponda
 
Unapiganaje kutafuta amani wakati wakati kupigana kwenyewe huondoa amani?!

Na hata kama ingekuwa watu wanapigana kutafuta amani, bado pia ulitakiwa kutafuta kwanini walipigana!!

Watu wanapohangaika kutafuta amani kwanza ndipo haki ichukue nafasi ni katika mazingira ambayo tayari amani imeshavurugika, na katika mazingira kama hayo, of course, no peace no justice!!!

Lakini katika nchi kama yetu tunatakiwa kutafuta na kutoa haki kwanza ili tusifikie kupigana kutafuta haki na hatimae kulazimika kutafuta amani kwanza ndipo haki itawale!!

Mababu zetu walipigana Vita Vya Majimaji sio kwa ajili ya kutafuta amani bali kutafuta haki ambayo ilipokonywa na Wajerumani na kuwafanya babu zetu kama viumbe dhalili!!

Kule Nigeria kulitokea vita vya wenyewe kwa wenyewe in the name of Biafra War! Watu wa Biafra hawakuanzisha vita ile kutafuta amani bali walianzisha kupigania kile walichoona kukiukwa kwa haki zao!!!

Enzi za ubaguzi wa rangi kule SA vurugu zilikuwa haziishi!!

Vurugu zile za SA hazikuwa za kutafuta amani bali za kutafuta hakl ambayo iliporwa na makabaru na kuwafanya watu weusi kuwa ni watu wa daraja la chini!!

USA nako kumekuwa zikitokea vurugu! Vurugu zile zinatokana na kile kinachodhaniwa mamlaka kutotenda haki kwa watu weusi na wala sio vurugu za kutafuta amani!!!

Watu wa CCM wamekuwa wakiwaita wale wale wanaowasaidia kwa majina mabaya kama vile Mabeberu! Hasira hizi za wana-CCM bila kujali kama zina mantiki au hapana hazitokani na wao kuamini kwamba Mabeberu wanavuruga amani nchini bali zinatokana na wao kuamini Mabeberu wanaingilia mambo ya ndani ya Tanzania wakati mambo ya ndani ya nchi ni haki ya kimsingi ya any sovereign state!!!

Itoshe tu kusema kwamba, more often than not, ukiona pahala amani imetoweka basi hapo kuna haki ama imeporwa au haitekelezwi!!!

Hata ndani ya nyumba, amani hutoweka pale haki baina ya wanandoa inaposigidwa... ama mwanamke kutotekeleza wajibu kama mwanamke na hivyo kumnyima mumewe haki yake kama mume, au mume kutotekeleza wajibu wake kama mume na hivyo kumnyima mkewe haki yake kama mke!!

HAKUNA AMANI PASIPO NA HAKI, na hata ikiwepo, inakuwa sio amani bai utulivu ulio chini ya mafuta ya petroli ukisubiri cheche ndogo tu ya moto petroli iripuke na utulivu na kuunguzia mbali utulivu!!
Huu uchambuzi ulitakiwa usambazwe kwa viongozi wote wa CCM, BAKWATA, CCT, TEC na midoli ya Lumumba.
Kongole sana mkuu Chige .
Mungu akubariki.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Inahitaji akili kubwa sana kueleza kwa ufasaha dhana ya haki na amani.

1. Kuna nyakati watu hupigana ili kutafuta amani.
2. Vurugu sio kinyume/ (opposite of) cha amani.

Dhana ya Haki na Amani huwa aimuliwi kwa kuangalia kipi kinatangulia.

Kumbuka :- Amani ikiwepo inatoa nafasi kwa haki kutendeka, Haki ikiwepo inatoa uhuru na hakikisho la watu kufurahia amani.

Justice and peace is a two headed snake.
Tanzania tumekuwa na amani miaka nenda rudi!Kwa maana hiyo nadharia ya nini kiwepo kwanza hapa haifanyi kazi maana tayari amani tumekuwa nayo toka uhuru!Sasa kinachotakiwa ni haki ili kuendelea kuilinda hii amani ambayo imekuwepo!Wakati tunachangia tujaribu kuendana na uhalisia!
 
Binafsi nilipoandika uzi wa Tanzania Kwanza watu walinishambulia na katika kunishambulia waliweka maneno HAKI na AMANI.

Hivi nini kitangulie, haki au amani? Kwa sababu penye vurugu hata hiyo haki haiwezi kupatikana.
Ni kweli penye vurugu hakuwezi kuwa na haki, lakini jiulize, vurugu huletwa na nini?
Dhuluma huleta vurugu. Ukitaka utulivu na amani hakikisha kwanza kwamba haki ipo.
 
Penye HAKI vurugu yoyote haiwezi kutokea! Haki ndio msingi wa AMANI!
Hata viongozi wetu wa dini wanahubiri AMANI, wangeweka zaidi msisitizo kwenye kuhubiri HAKI badala ya kukimbila kuongelea AMANI!
Watu wanaambiwa wailinde AMANI tuliyo nayo badala ya kuwaambia tendeni HAKI muistawishe AMANI tulio nayo!
 
Mmh watu hupigana wakitafuta amani mbona sio kweli, kwani kupigana huja mnapokubaliana au kutofautiana?. Penye amani ndo Penye mafanikio, penye maisha. Amani huzaa haki, na haki huendana na wajibu.
Kupigana huja mnapotofautiana, hasa mmoja anapomdhulumu mwingine haki yake. tukitaka watu wasipigane, tulinde haki zao.
 
Amani ni tunda la haki.
Watawala wa kiafrica wangekuwa wanatenda haki kusingekuwepo na Vita afrika.
 
Haki ni mama wa amani. Hata ndani ya ndoa kama mume ukimtimizia mwanamke haki yake basi ndoa itakuwa na amani. Hata katika taifa, kukiwa na HAKI basi ujue na AMANI itashamili

Sent from my SM-J250F using JamiiForums mobile app
Mkuu, Jambo la mke kumtimizia haki zake ni kitendo cha ujumla Sana!

Lakini Haki inayozidi hapo ni tendo la ndoa linalokidhi matakwa ya kila mmoja,

Hilo tendo wengi hawalifanyi Kwa kulidhishana Kwa kuwa hawana Amani, Amani ni utulivu wa moyo, Ni utulivu unaozidi kiwango cha utulivu, na tendo la ndoa hunoga kukiwepo Amani ya moyo, (utulivu)

Amani ndio humpa mtu nguvu ya kutenda Jambo Kwa ukamilifu
 
Ukikosa haki yako utokuwa na amani ukiikosa amani utaitafuta kwa njia yeyeto ndo chanzo cha ugaidi, vikundi vya waasi, Vita vya wenyewe kwa wenyewe utasikia wenye mtindio wa kufikiri usingizia mabeberu chanzo cha Vita afrika na wanasahau msingi mkuu ni lzm haki isiwepo kwanza.
Watawala wa kiafrica ni mabingwa wa kuvunja haki za wananchi. Yote ni kwa sababu afrika haina mfumo sahihi wa haki wa Utawala thus baada ya Uhuru nchi nyingi za kiafrica watawala wao walifata mifumo ya kijamaa ambayo imezaa udikteta. Udikteta ni kuwanyima wengine haki ya maamuzi juu ya hatma yao.
 
Je bila Aman Kuna haki inaeza kutendeka maana moja laweza kuchelewa
Kwanini huelewi bibie; ukumbuke mwanzo kwenye jamii hayo yote mawili (haki na amani) huwepo, kinachotokea mpaka tena kuanza kutafuta kimojawapo lazima pawe na sababu, na sababu yenyewe ni pale kundi moja kwenye jamii litakapoona linaonewa( halitendewi haki), hapo ndipo huanza mapambano ili kuidai hiyo haki yao, na mapambano hayo hatimaye husababisha kuvuruga amani, natumai mpaka hapo utakuwa umeelewa kipi huanza.
 
Amani ni zao la haki, bila haki amani haitakuwepo
Haki ikitendeka sehemu yoyote Amani inashamiri. Iwe ngazi ya familia au taifa haki ndio huleta aani. Na amani no kitu kilicho rohoni mwa MTU. Ukiona jamii inatamba tuna Amani na utulivu ,wakati kuna viashiria vya kutotendeana haki kati yao ujue hapo kuna kundi linalokandamiza jingine na hao wanaokandamizwa wantutkutia ndani na kuomba Mungu siku moja mambo yabadilike . hapo ndipo mkandamizaji hutamba tuna amani na utulivu. Unaweza usipambane na mkandamizaji Wa haki zako , kwa kujua tu huna nguvu za kupigana naye lakini rohoni unaomba siku moja mambo yabadilike ukiwa bado hai.

Sent from my TECNO-J5 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom