Uchaguzi 2020 Nini kitangulie, haki au amani?

Amani bila haki ni kitu cha kufikrika . hatuna neno la kuelezaa hali hiyo ila kwa lugha rahisi ni ukosefu Wa vita au vurugu unapotamba eti una amani wakati hamtendeani haki.

Sent from my TECNO-J5 using JamiiForums mobile app
 
Umeielezea vizuri
 
Binafsi nilipoandika uzi wa Tanzania Kwanza watu walinishambulia na katika kunishambulia waliweka maneno HAKI na AMANI.

Hivi nini kitangulie, haki au amani? Kwa sababu penye vurugu hata hiyo haki haiwezi kupatikana.
Hakuna amani bila haki
 
Binafsi nilipoandika uzi wa Tanzania Kwanza watu walinishambulia na katika kunishambulia waliweka maneno HAKI na AMANI.

Hivi nini kitangulie, haki au amani? Kwa sababu penye vurugu hata hiyo haki haiwezi kupatikana.
Haki huleta amani
 
Amani ni tunda la haki.Bahati mbaya viongozi wetu wa dini wamemezeshwa amani amani, wamesahau haki.ukweli ni kwamba anayehubiri amani bila kuhubiri haki apoteza muda bure..
Wanaelewa vizuri kabisa ila wameamua tu kufanya fujo.
Hata ukiwaangalia usoni mwao ni aibu tupu imewajaa, maana wanajua kuwa wanatenda yaliyo kinyume kwa makusudi mazima.
 
Binafsi nilipoandika uzi wa Tanzania Kwanza watu walinishambulia na katika kunishambulia waliweka maneno HAKI na AMANI.

Hivi nini kitangulie, haki au amani? Kwa sababu penye vurugu hata hiyo haki haiwezi kupatikana.
Kwa mfano hapa Tz ,,amani bado ipo ila kuna vitendo visivyo vya haki ambavyo vinaweza vikapelekea amani kutoweka.
Kukiwa kuna haki na amani itakuwepo lakini ukiondoa haki unaweza pia kutowesha amani.
 
Msingi wa uubwaji wa huu ulimwengu tunaoishi leo ulikuwa ni HAKI..... na ndiyo maana kuna maneno tunasema Mwenyezi Mungu ni mwenye HAKI.... bila kutenda HAKI unatenga nafsi yako na Mungu..... Na ndiyo maana watu huapa kwa kuanza kwa kutamka neno HAKI..... kwa mfano.... Kama si HAKI yangu sawa tutaona...... nk.

Sasa ukishakuwa na HAKI basi Amani by default hufuatia...... HAKI ni tunda la AMANI..... maana penye HAKI upendo (amani) hutawala.

Sasa SHETANI huwa hataki kabisa kusikia neno HAKI...... na ndiyo tunasema kwamba msingi wa uubwaji wa dunia hii ulianzia kwenye HAKI.
 
Binafsi nilipoandika uzi wa Tanzania Kwanza watu walinishambulia na katika kunishambulia waliweka maneno HAKI na AMANI.

Hivi nini kitangulie, haki au amani? Kwa sababu penye vurugu hata hiyo haki haiwezi kupatikana.

Siku zote kulikuwa na amani, kwa bahati mbaya amani hii ina tafsiri ya ukondoo kwa wapinzani. Hiyo amani ndio imekuwa ikitumika kama sehemu ya kupora haki ya wapinzani. Sasa ngoja tushikane mashati ili haki ipatikane. Hapo ndio mtajua haki haiondoi amani.
 
Mkuu weka vizuri hapo juu, amani ni tunda la haki.
 
Binafsi nilipoandika uzi wa Tanzania Kwanza watu walinishambulia na katika kunishambulia waliweka maneno HAKI na AMANI.

Hivi nini kitangulie, haki au amani? Kwa sababu penye vurugu hata hiyo haki haiwezi kupatikana.
Utakuwaje na amani bila hako? Haki huzaa amani so
Haki then Amani
 
Ukondoo si amani. Haki ndio Kil kitu.
 
HAKI ndio msingi mkubwa wa AMANI, Amani hujengwa na haki.

Kati ya viongozi wa dini waliokuta Kongamano la Amani la Viongozi wa dini lililofanyika Dar ni kiongozi huyu[emoji116]pekee ndiye katika hotuba yake alieleza kwamba chimbuko la AMANI ni HAKI na USAWA.
[emoji1485]Kwanini viongozi wakiwepo wa dini wanaogopa kutamka HAKI? https://t.co/dRbZdyjHWz

(Kama sijakosea ni Sheikh KISHKI. Spelling ni sawa?)

...Habari njema kwa wote... inasema
Isaya 32:17

Na kazi ya haki itakuwa amani; na mazao ya haki yatakuwa ni utulivu na matumaini daima.

Tatizo liko wapi?
 
Bibi huyu anatakiwa apate TUZO ya kujitambua...... Pata NONDO ya dhana na AMANI kuelelea uchaguzi Mkuu.

"..everybody is crying now for PEACE,non is crying for JUSTICE.. " - PETER TOSH.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…