Umejenga hoja barabara, Mkuu. Asante sana. Hata hivyo, kuna fact check moja ya kuwekwa wazi pia kuna hoja umeiibua inayohitaji mjadala mpana sana hasa kuhusu Ivory Coast na Francophone countries kwa ujumla.
Fack check: Ni kweli ilihimizwa hapa nchini watu wafanye kazi, lakini kwa wanasiasia hawakuzuiwa kufanya siasa bali alielekezwa wafanye siasa kwenye majimbo yao ya uchaguzi. Na sababu ilitolewa kuwa baada ya miaka mitano watapimwa kwa siasa walizofanya kwenye majimbo yao.
Kuhusu suala la Ivory Coast: Nchi za Francophone kama ni suala la haki za kitaasisi nchi hizi karibu zote hazina haki taasisi! Kwa sababu nchi hizi hazijapewa haki ya jumla na Ufaransa kama Taasisi/nchi ya kujitegemea kwa uhuru zaidi . Tena kule ndiyo kuna utulivu asilimia 95 na vurugu asilimia tano hakuna chembe ya amani huko! Mfano wa haki ya nchi hizi iliyopokwa na Ufaransa ni mfumo mzima wa uendeshaji wa nchi katika mapato na matumizi ya nchi hizo. Central Banks za nchi hizo ni kama mawakala wa " Central Bank" ya Ufaransa. Kuna kitu kinaitwa " CEFA" ela itumikayo kwenye nchi hizo! Ni Ufaransa inapanga kiasi gani kitumike kwenye nchi fulani! Hapo kuna haki kweli ya kitaasi ya kinchi ambayo ni huru!? Sasa inapotokea, kiongozi wa mzalendo wa kiafrika na akataka kudai haki hii ya kitaasisi kwenye nchi hizo atatungiwa uzushi na kumpaka matope kiasi cha kufanyiwa hujuma hata inayoweza kugharimu maisha yake! Haya tumeyaona Burkina Faso. Walimuua Tomas Sankara wafaransa kwa hujuma kupitia kwa rafiki yake Tomas alikuwa ameibadili Burkina Faso ndani ya miaka minne na kuwa nchi inayoheshimika Barani Afrika na dunia kote! Nakuhakikishia ukifanyika uchunguzi sawa sawa, unaweza kukuta hata Henri Bedie alikuwa anafanya maandalizi ya kudai haki ya kitaasisi ya kinchi kutoka kwa Wafaransa ndiyo maana labda akaundiwa zengwe! Na silaha kubwa inayotumika ni "disinformation" kwa ku assassinate character ya mzalendo!
Ni hayo niliyotaka kukumbusha Mkuu.
TUJITEGEMEE,
1. Awali ya yote JPM hana mamlaka ya kukataza vyama vya siasa kufanya mikutano sehemu watakazo kwa sababu, hata Sheria ya Vyama vya Siasa yenyewe, tena ambayo ilifanyiwa mabadiliko ndani ya utawala wake inasema kwamba:-
Hiyo ndiyo sheria ya nchi ambayo inatoa HAKI kwa Vyama vya Siasa kufanya Mikutano ya Hadhara POPOTE PALE ndani ya Jamhuri!!
Lakini JPM kwa kulinda maslahi ya utawala wake, akavunja hiyo sheria na kupoka haki ya vyama kufanya mikutano POPOTE pale!
Na ndo maana nikasema, kuna mengi yaliyovuruga amani kwenye nchi zingine lakini hapa pia yanatokea!!! Ukiukwaji mkubwa wa sheria na haki wa namna hiyo mataifa mengine hawawezi kuvumilia hata siku moja!
Na kwa hakika, amani ya nchi hii hailindwi na Serikali bali inalindwa na Vyama vya Upinzani ambavyo hata pale haki zao zinapovunjwa wazi wazi, wao huamua kuwatuliza Wafuasi wao!
So, Upinzani Ndiyo Wanaolinda Amani ya Taifa Hili!
That's one but two, ingawaje unasema hawakuzuiwa kufanya siasa bali waliambiwa wafanye kwenye majimbo yao lakini agizo hilo haramu la JPM lilikuwa enforced dhidi ya upinzani wakati halikuwa enforced dhidi ya CCM!
Kila mmoja anafahamu mikutano ya hadhara iliyokuwa ikifanywa na akina Humphrey Polepole pamoja na Bashiru Ally!
NOW tell me, Polepole kawa Mbunge wa Karatu kupitia uchaguzi upi hadi akafanye mkutano wa hadhara huko?!
Kumbe wakati Upinzani wakizuiwa kufanya siasa za kitaifa huku mara nyingine wakiingiliwa na polisi hata wanapofanya mikutano ya ndani, CCM waliendelea kufanya siasa na mikutano ya hadhara!
Hilo la Francophone natamani kuingia kiundani lakini nachelea kutoak nje ya mada lakini itoshe tu kusema kwamba kama kupokwa haki na mataifa ya magharibi, karibu nchi zote za ulimwengu wa tatu zinapokwa haki hizo kwa namna moja au nyingine lakini hapa tunazungumzia haki zinazopokwa na watawala wa Kiafrika wengine tuliowachagua kwa kura zetu na wengine waliojinadi kuongoza Waafrika wenzao!!