Uchaguzi 2020 Nini kitangulie, haki au amani?

Uchaguzi 2020 Nini kitangulie, haki au amani?

Haki ikiwepo kwa maana kukiwa na mahakama huru watakao hakikisha kila mtu anapata haki yake na uwezo wa kuipata haki na kusaidiwa kupata haki watu wakiwa na imani na hukumu basi amani itapatikana yenyewe lakini ili kupata yote haya ni kuwa na katiba na sheria za kulinda haki ya kila mtu. Amani ipo hata kwenye nchi za madikteta wauwaji wanawatawala watu kwa hofu na amani ipo tu kwa nguvu ila amani ya ukweli ni matunda ya haki kwa wote.
 
Mmh watu hupigana wakitafuta amani mbona sio kweli, kwani kupigana huja mnapokubaliana au kutofautiana?. Penye amani ndo Penye mafanikio, penye maisha. Amani huzaa haki, na haki huendana na wajibu.
Kama hamjui haya maneno acheni mjadala.
Kwanza haki ndipo amani itawale
Kuna Haki
Amani na utulivu

Watu hupigania utulivu siyo amani.
Kundi moja hupigana kwa kuwa limedhurumiwa haki yake.
Kundi la pili hujibu mapigo ili kuendelea kudhurumu.
Hapo anayejibu mapigo hapiganii amani.

Akijitokeza mtu akawaweka chini na kusikiliza madai yao,bila shaka atamtaka anayedhurumu kumpa haki yake anayedai.

Akikubali hapo mapigano yameisha
HAKI IMEZAA AMANI NA UTLIVU.

KUNDI MOJA LINAPIGANIA HAKI
KUNDI LA PILI LINAPIGANIA DHURUMA
KUNDI LA TATU BAADA YA KUSIKILIZA PANDE MBILI LINAGAWA HAKI ILI AMANI IPATIKANE,HALIGAWI AMANI

KWANZA HAKI PILI AMANI
 
Unaniangusha, yani hujui vurugu hutokea pale ambapo panakuwa na uonevu/upendeleo?

Haki ikiwepo, amani nayo itakuwepo automatically.

Tanzania kuna amani ya kinafiki ambayo haijajengwa kwenye misingi ya haki, ni amani inayolazimishwa kwa mabomu ya machozi na kuweka watu ndani bila makosa, hasa pale wanapodai haki zao.
Tanzania pana utulivu wa woga siyo amani
Amani huja kwa kuridhika toka ndani ya nafsi,ikiwa mtu hajaridhika na hana la kufanya huyo hana amani bali utulivu wa kulazimishwa
 
Amani ni tunda la haki.Bahati mbaya viongozi wetu wa dini wamemezeshwa amani amani, wamesahau haki.ukweli ni kwamba anayehubiri amani bila kuhubiri haki apoteza muda bure..
Viongozi wa dini hawayajui maandiko kabisa
Wapo kwaajili ya sadaka tu.
 
Unaniangusha, yani hujui vurugu hutokea pale ambapo panakuwa na uonevu/upendeleo?

Haki ikiwepo, amani nayo itakuwepo automatically.

Tanzania kuna amani ya kinafiki ambayo haijajengwa kwenye misingi ya haki, ni amani inayolazimishwa kwa mabomu ya machozi na kuweka watu ndani bila makosa, hasa pale wanapodai haki zao.
Haki au uhakika wa kupata haki unapokuwepo AMANI huonekana. Ila ukiona kuna manung'uniko na harakati za kudai haki halafu vitsho au nguvu ya aina yoyote ikatumika kutuliza wanaodai haki kitakachojitokeza sio amani bali ni utulivu. Utulivu kuwepo haimaanishi amani au haki vipo. Kwa maana hiyo utulivu unaweza kuwepo lakini kukawa na manung'uniko na msongo wa mawazo. Kwa hiyo haki huzaa amani.
 
HAKI
Kwa Kigiriki inaitwa dikaiosyne, kutokana na neno asili dike yaani anayeelekeza na kwa hiyo pia mwongozo, utaratibu. Tofauti na nomos, yaani sheria inayoongoza wanyama pia, dike inahitajiwa na binadamu ili kuishi kwa utaratibu. Ni kinyume cha bie, ukatili, nguvu inayoangamiza. Dikaios (mwenye kujali haki), ni mtu anayemtendea kila mmoja haki yake. Dikaia zoe ni maisha ya kiutu yanayopingana na hybris (kiburi) na ushenzi.

Kwa Kilatini kutokana na neno jus, haki, linapatikana neno justus, mwenye kujali haki, na hatimaye justitia, iliyo adili la msingi la utulinalotufanya tumpatie mwingine anachostahili.

Maana ya haki inatofautiana Kwa kila utamaduni. Katika maana ya kwanza kabisa ambayo ilitafsiriwa na mwanafalsafa wa Ugiriki, Plato kwenye kazi yake Jamhuri. Kutokana na historia dhana mbalimbali zimegunduliwa.
..........................................
Amani ni hali ya raha na salama bila ugomvi; ni kinyume cha fujo au vita.

Mara nyingi hali za amani ya nje na amani ya ndani hutofautishwa.

Amani ya nje au amani ya kisiasa na kijamiiEdit

Amani ya kisiasa ni hasa kutokuwa na vita na mapigano kati ya nchi mbalimbali au kati ya vikundi ndani ya jamii. Kama kuna mgongano kutokana na tofauti ya upendeleo juu ya jambo fulani amani inatunzwa kama pande zote zinafuata sheria au kanuni za jamii bila kutumia mabavu.

Mara nyingi maana kuu ya "amani" ni hali ya kutokuwa vita kati ya nchi kwa sababu vita huleta uharibifu mkubwa kushinda aina nyingine za ugomvi.

Amani inaweza kutaja pia tendo la kumaliza vita kwa njia ya mapatano kati ya washiriki wa vita au pia kati ya washindi na washindwa wakikubali kumaliza uadui. (linganisha Amani ya Westfalia).

Tangu vita kuu za dunia kulikuwa na majaribio mengi kuhakikisha amani kwa njia ya mapatano kati ya nchi zote za dunia. Shirikisho la Mataifa lilianzishwa mwaka 1919 likashindwa kuzuia vita kuu ya pili ya dunia ikafuatwa na Umoja wa Mataifa ulio na shabaha ya kupunguza na kuzuia vita kwa njia ya ushirikiano.

Tunatakiwa kulinda amani ili kusonga mbele hata kiuchumi.

Amani ya ndani au amani ya kirohoEdit

Tangu kale watu waliona ya kwamba amani ya nje inaenda sambamba na amani ndani ya kila mtu. Penye hasira nyingi moyoni mwa watu ni vigumu kutunza amani ya nje.

Kwa sababu hiyo amani imekuwa jambo muhimu katika dini na falsafa.

Dini mbalimbali zina ujumbe kuhusu amani:

ndani ya roho wa mtu mwenyewe

kati ya Mungu na mwanadamu

kati ya watu

Credit : Wikipedia
Yaani umeboronga kwelikweli.
Yesu aliwaambia mafarisayo waoshekwanza kikombe cha chano ndani na nje nayo itakuwa safi.

Wao walijifanyia usafi wa nje(mavazi)na kujiita viongozi wa dini.

Nini maana ya usafi wa ndani?
HAKI NI MATENDO MEMA
BIBLIA INASEMA,HAKUNA AMANI KWA WABAYA,
Mwizi hatendi haki ndy maana hana amani na polisi.

Asiye mwizi ana amani na polisi kwakuwa anatenda HAKI .
KWANZA HAKI
 
Penye Amani sio lazima pawe na haki,ila penye haki automatically Amani itakwepo.Watu hupigania haki
 
Binafsi nilipoandika uzi wa Tanzania Kwanza watu walinishambulia na katika kunishambulia waliweka maneno HAKI na AMANI.

Hivi nini kitangulie, haki au amani? Kwa sababu penye vurugu hata hiyo haki haiwezi kupatikana.
Haki
 
Binafsi nilipoandika uzi wa Tanzania Kwanza watu walinishambulia na katika kunishambulia waliweka maneno HAKI na AMANI.

Hivi nini kitangulie, haki au amani? Kwa sababu penye vurugu hata hiyo haki haiwezi kupatikana.
#Amani, Uhuru au Haki: 1.AMANI ni hali ya raha na usalama bila ugomvi ni kinyume cha fujo na vita. Amani ya nje ya kikundi cha watu au jamii inaenda sambamba na amani iliyo ndani ya kila mtu hivyo hakuna msuguano kinzani unaosababisha ushindani wenye ghasia kutetea wanachokiamini.Ili amani ikamiliki hali zifuatazo ni sharti zionekane zikifanya kazi ipasavyo: i) Amani ndani ya roho na mtu mwenyewe; ii) Amani kati ya Mungu na mwanadamu na; iii) Amani kati ya watu na watu
2. UHURU ni hali kamili ya ndani ambayo mtu ameondolewa vifungo vyote vilivyomzuia asiwe mwenyewe kweli wala aitende anavyoona ni vema kutenda.Kwa kadri mtu au kikundi anavyohisi kuwa na vizuio katika kutenda, kutoa maoni chanya au hasi kwa nia ya kurekebisha kama anavyohisi hivyo anahitaji kupiga hatua ya ukombozi pengine kwa msaada kutoka kwa watu wengine, kimawazo, kimbinu na mwongozo ili hatimae ahisi vikwazo haviko tena hivyo kufanya chochote kisicholeta mgogoro wa nafsi, maslahi na mahitaji ya msingi ya kibinadamu bila bughudha ili mradi sheria hazivunjwi;
3. HAKI ni jambo au suala ambalo mtu anastahili au kitu anachostahili kuwa nacho sawa na mwingine kwa hadhi ya kibinadamu. Kwa tafsiri ya kisheria ni kile ambacho mtu anastahili kuwa nacho au kile anachoruhusiwa kufanya, au kile anachostahili kupokea kutoka kwa wengine kwa mjibu wa sheria.

NB: HAKUNA MWANSIASA MWENYE UWEZO WA KUTOA HAKI NA PASIWEPO MANUNG'UNIKO; haki hutolewa au kutambuliwa kwa mjibu wa sheria tu kupita vyombo vilivyoundwa kutoa haki kama Mahakama, kamisheni za maadili na tume kwa mjibu wa katiba ya nchi.
 
Binafsi nilipoandika uzi wa Tanzania Kwanza watu walinishambulia na katika kunishambulia waliweka maneno HAKI na AMANI.

Hivi nini kitangulie, haki au amani? Kwa sababu penye vurugu hata hiyo haki haiwezi kupatikana.
HAKI kwanza, halafu AMANI na mwisho FURAHA. Kukiwa na kutenda haki katika mambo mbalimbali watu watakuwa na amani. Na watu wakiwa na amani pia watakuwa na furaha maisha yanasonga mbele[emoji120][emoji120][emoji120]
 
Yaani umeboronga kwelikweli.
Yesu aliwaambia mafarisayo waoshekwanza kikombe cha chano ndani na nje nayo itakuwa safi.

Wao walijifanyia usafi wa nje(mavazi)na kujiita viongozi wa dini.

Nini maana ya usafi wa ndani?
HAKI NI MATENDO MEMA
BIBLIA INASEMA,HAKUNA AMANI KWA WABAYA,
Mwizi hatendi haki ndy maana hana amani na polisi.

Asiye mwizi ana amani na polisi kwakuwa anatenda HAKI .
KWANZA HAKI
Pumbavu kweli, hivi wewe mwenyewe ukisoma unaelewa ulichoandika?
 
Unaniangusha, yani hujui vurugu hutokea pale ambapo panakuwa na uonevu/upendeleo?

Haki ikiwepo, amani nayo itakuwepo automatically.

Tanzania kuna amani ya kinafiki ambayo haijajengwa kwenye misingi ya haki, ni amani inayolazimishwa kwa mabomu ya machozi na kuweka watu ndani bila makosa, hasa pale wanapodai haki zao.
Kwahiyo Kama unataka haki ya kufanya ushoga na kuandamana tusikupige mabomu ili tuitunze amani yetu??
 
Binafsi nilipoandika uzi wa Tanzania Kwanza watu walinishambulia na katika kunishambulia waliweka maneno HAKI na AMANI.

Hivi nini kitangulie, haki au amani? Kwa sababu penye vurugu hata hiyo haki haiwezi kupatikana.
#KIPI KIANZE |HAKI au AMANI: 1) HAKI-hakuna mwana siasa mwenye uwezo wa uhakikisho wa haki ispokuwa tu mamlaka halali za kisheria hivyo huwezi kuhakikisha haki imetendeka kama kuna msuguano kati ya pande mbili ambazo hazikubali nani ni nani mpaka wapelekwe kwenye vyombo ambavyo havikuwa sehemu ya kile kilichosababisha mgogoro. Wakifikishwa hapo pande zote mbili husikilizwa kwa usawa, hupokea ushahidi na marejeo ya sheria, kanuni na miongozo iliyotakiwa kuwasimamia nani kati yao amevunja ndipo ikithibika haki ya upande mwingine ndio yakinifu hupewa mhusika na asiyeridhika huelekezwa kukata rufaa. Kwa maelezo hayo ni wapi wana siasa wanaweza kutendeana haki?
2) AMANI-mwana siasa anawajibu mkubwa na ni sehemu ya kazi yake kuhakikisha anahamasisha na kusimamia utulivu wa wafuasi wake wasivunje sheria. Kwa hiyo mwenye wajibu wa kutoa haki hapo sio serikali tendaji ila tume teule ambayo ndio ina mamlaka hayo kwa vile watumishi wake ni wana sheria au majaji kwa taalumu. Kwa mtizamo huu utajua ni kipi kianze na nani na kipi kifuate ili kuhakikisha kila upande uridhike kwa namna ulivyotendewa na kwa kuzingatia sheria, taratibu, kanuni na miongozo ya haki na WAJIBU.
 
Back
Top Bottom