Nini kitatokea baada ya Magufuli kustaafu Urais?

Nini kitatokea baada ya Magufuli kustaafu Urais?

Habari wadau wa JF siasa.

Nimekuwa nikiwaza Sana sura ya nchi na hali ya nchi hii baada ya Rais Magufuli kumaliza mihula yake miwili. Je nchi itakuwaje kirushwa na kifisadi, kiuchumi, kisiasa, kijamii, kimaendeleo nk?

Ajaye atakuwaje na atatupeleka wapi jamii ya Kitanzania kipindi hicho kitakuwaje?
Vipi Ushapata muongozo wa kitakachotokea?

Cc: Mahandazi
 
Tutaendelea kama kawaida, maana kama rushwa bado ipo, kama ufisadi bado upo sema shida ni kwamba tofauti na kipindi cha JK bunge haliwezi kuyaongelea, Tanzania imejitoa kwenye uwazi hivyo mikataba siku hizi ni siri hatutakiwi kujua yaliyomo. Vyombo vya habari vimepigwa ganzi hakuna tena ile mijadara ya wazi na uandishi chokonozi.

Utashangaa mambo yatakayoibuka baada ya jamaa kumaliza awamu yake watu wakapata uwezo wa kuanza kuongea. Wale wale waliokuwa wanampamba kikwete aendelee leo hii ndiyo wanasema awamu iliyopita ilikuwa mbovu sana. Kila zama na mfalme wake.
Hatimaye madudu yameanza kuibuliwa na CAG.
 
1. Miradi mingi ambayo aliianzisha itasimama

2. Chattle kitabaki kijiji kama zaman tena enzi za nyerer kabisa

3. Uwanja wa chattle utakuwa eneo la kuchezea mpira na matamasha ya dini

4. Viongozi wengi wataonyesha uhslisia wa kipindi cha mzee magufuli..

Ntakuja baadae kidogo.. Naenda kwenye uzi wa kula tunda kimasihara
Rudi mkuu kama umemaliza kula kimasikhara
 
Mkuu tindo nimekusoma hapa kwenye utabiri wako. Yanayokea tunayaona
Amani na upendo wa kweli utarejea na sio hofu na nidhamu za kinafiki. Utawala wa sheria utarejea na sio sheria zinazomfurahisha rais. Ccm itarejea kuwa chama cha siasa, na sio kikundi cha dola kilichojificha kwenye koti la siasa kupitia madaraka ya urais. Uhuru wa vyombo vya habari utarejea na serikali itarudi kuwa ya uwazi. Bunge latarudi kuwa Muhimili unaojitegea na sio hekalu la kumsifia rais na kutii kila atakacho. Mahakama itarejea na kutekeleza wajibu wake wa kutoa haki, na sio kuwa taasisi ya kukosoa wote wasiomsujudia rais. chaguzi za nchi zitarudisha heshima yake, na sio kama sasa kuwa maonyesho ya ujinga wa mtu mweusi kwenye box la kura.
 
Mkuu heshima yako!
Sijambo Mkuu, tupeane pole kwa msiba mzito uliotukuta.

Kwenye maoni yangu nilisema haijawahi kutokea Rais kufikwa na umauti akiwa madarakani, lakini Mungu mwenyewe hujiamulia wapi na lini avune.

Hatimaye kwa mara ya kwanza imetokea, what else should we say?

Apumzike kwa amani😭🙏🙏
 
Na maisha yanaendelea vizuri sana. Tunahitaji katiba mpya
Katiba iliyopo ina mapungufu gani ?

Katiba ya Tanzania ya mwaka 1977 ni moja ya Katiba bora barani Afrika na Duniani kwa ujumla
 
Sijambo Mkuu, tupeane pole kwa msiba mzito uliotukuta.

Kwenye maoni yangu nilisema haijawahi kutokea Rais kufikwa na umauti akiwa madarakani, lakini Mungu mwenyewe hujiamulia wapi na lini avune.

Hatimaye kwa mara ya kwanza imetokea, what else should we say?

Apumzike kwa amani😭🙏🙏
Umefurahi?
 
Back
Top Bottom