Nini kitatokea baada ya Magufuli kustaafu Urais?

Yanayoendelea middle east kwa Sasa ndiyo yatakuja kutoka Africa 20 years to come. It will get even worse than this. Kama unaweza kuwatafutia makazi wanao nje ya hili bara this is the right time. Mark my words!!
Mkuu umenena sahihi... Sioni Hali yoyote nzuri huko mbeleni... Ni muda was kujipanga na kuhangaika.
 
👊👊
 
Hata anachofanya polepole kupokea matatizo ya watu kwenye simu channel ten ni utopolo mtupu jengeni mifumo imara itakayosimamia kwa haki sheria na taratibu za nchi kinyume na hapo ni sifa za kijinga mnataka kujipatia.
Wanaogopa Katiba mpya badala yake wanafanya vitu bila kufuata sheria.Mihemko team at their best.
 
Kwanza swala la Magufuli kustaafu futa kwenye kichwa chako sema akifa au akipinduliwa maana Magu hana tofauti na Kagame au Museveni

Kuhusu hali ya Nchi kama ataondoka kwa kifo hali ya Nchi itakuwa shwari tu maana kupata au kukosa tumeshazoea Watanzania ila kama ataondoka kwa kupinduliwa kutakuwa na machafuko kidogo na hali ya maisha itarejea kama kawaida
 
Mtu aliyetesa watu itaumiza akistahafu kwa amani
 
Sioni hata cha ajabu kaongea, ni common sense.
Umechukua mkopo tukakupa ukaenda kusoma udaktari ili ukimaliza uhudumie wananchi we unaenda binafsi kwa ajili ya maslahi si ungeenda akusomeshe huyo mwekezaji.
Ni ukweli mchungu.
Nasema uwongo jamani?
Kaka hapa kwenye Mkopo ni heri ukanyamaza tu maana kuna vitu haviko sawa kabisa,hili la Daktari aliyemaliza masomo akapata kazi Private sector sidhani km kuna ubaya,provided yupo ndani ya Tanzania na anawahudumia Watanzania, na kwa upande mwingine hata Bodi ya mikopo itanufaika zaidi kutokana na makato ya Mshahara wake "mnono"maana mkopo unakatwa 15% ya mshahara ghafi hii itasaidia wengine wanaosubiri kupata Mkopo!
 
Kwani anatakiwa kujiamulia mwenyewe?
Sijui kama umeuliza hili swali ukitaka kupata jibu!

Wewe unadhani ni nani anayo madaraka ya kumwamulia. Huyo mtu anazo bunduki na mabomu na mapolisi?
 
Ana hulka zote za kidikteta na ulevi wa madaraka. Ikitokea akakubali kweli kuiheshimu Katiba, basi tutatakiwa kufanya sherehe kila mtu kwa nafasi yake.

Maana ndani ya huu utawala wake, kama sisi watumishi wa umma; cha moto tunakiona. Ila lolote linaweza kutokea. Ni rahisi sana kwake kuendelea kubakia madarakani kupitia Bunge lililojaa mamluki wake kubadili kifungu cha sheria cha ukomo wa Urais,

Lakini pia kupitia ushawishi wa baadhi ya wananchi wenye njaa kuwezeshwa posho kidogo na hivyo kuingia mitaani kufanya maigizo ya maandamano ya kumtaka aendelee kubakia madarakani. Halafu na yeye atajitokeza kwenye vyombo vya habari na ile sura yake ya uongo ya upole na unyenyekevu, huku akijifanya ameguswa sana na hivyo kuamua kusikiliza sauti za Wanyonge za kumtaka kuendelea na utawala wake wa kibabe!

Mungu atuepushie mbali hii dhahama. Miaka 10 ya kudhulumiwa, kuteswa, kuuwawa, kutengwa, kubaguliwa, kudharauliwa, kukejeliwa, kutukanwa hadharani, kunyanyaswa, kuonewa, na kila aina ya uovu; INATOSHA!!
 
Ana hulka zote za kidikteta na ulevi wa madaraka. Ikitokea akakubali kweli kuiheshimu Katiba, basi tutatakiwa kufanya sherehe kila mtu kwa nafasi yake.
Hili nilikuwa na mpango wa kulianzishia mada yake ya kipekee kabisa. Ikitokea kwa sababu yoyote ile kutoka, hilo litakuwa ni jambo bora zaidi alilobakiwa kuwa nalo akilitimiza. Sioni kama kuna lingine lolote atakaloweza kulifanya linaloweza kuwa bora zaidi ya hilo katika uongozi wake wote.
 
Chato itarudi kua kijiji kama ivyokua na majengo yatakua magofu kama kule kalemii baada ya Mobutu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…