Ana hulka zote za kidikteta na ulevi wa madaraka. Ikitokea akakubali kweli kuiheshimu Katiba, basi tutatakiwa kufanya sherehe kila mtu kwa nafasi yake.
Maana ndani ya huu utawala wake, kama sisi watumishi wa umma; cha moto tunakiona. Ila lolote linaweza kutokea. Ni rahisi sana kwake kuendelea kubakia madarakani kupitia Bunge lililojaa mamluki wake kubadili kifungu cha sheria cha ukomo wa Urais,
Lakini pia kupitia ushawishi wa baadhi ya wananchi wenye njaa kuwezeshwa posho kidogo na hivyo kuingia mitaani kufanya maigizo ya maandamano ya kumtaka aendelee kubakia madarakani. Halafu na yeye atajitokeza kwenye vyombo vya habari na ile sura yake ya uongo ya upole na unyenyekevu, huku akijifanya ameguswa sana na hivyo kuamua kusikiliza sauti za Wanyonge za kumtaka kuendelea na utawala wake wa kibabe!
Mungu atuepushie mbali hii dhahama. Miaka 10 ya kudhulumiwa, kuteswa, kuuwawa, kutengwa, kubaguliwa, kudharauliwa, kukejeliwa, kutukanwa hadharani, kunyanyaswa, kuonewa, na kila aina ya uovu; INATOSHA!!